Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Matibabu ya SINUSITIS.
Sinus-Remedy-How-to-Treatment-Sinus-Infection-Without-having-Antibiotics-and-Stay-away-from-Sinus-Surgery-2459.jpg
Sinus-endoscope.jpg
 
mungu akuponye haraka na aendelee kukulia zito pia asante kwa kutupa taarifa kamili pia niwaombe watanzania tuache kuvumisha mambo
 
Na hizo treatment attempts hazikuwa za sinusitis,for 10 years hakujuwa,ama hawaku i diagnose.Na kwa mujibu wa Zitto,dalili ambayo ameitaja na inaendana na maelezo ya ugonjwa huu ni headache peke yake.Mengine hatujui.Inawezekana alipatwa na homa iliyosababishwa na sunsitis.Sasa sijui hiyo sinusitis ina uhusiano gani na malaria.Ndipo hapo sometimes ni kuchanganyana tu.

Mkuu mbona sikuelewi, kwani ZITTO anatuchanaganyana na kitu gani? tafadhali soma vizuri alivyo jieleza mbona maelezo yake yako crystal clear, kasema walimpima pale Muhimbili wakakuta ana malaria kwani hapo tataizo ni nini-ina maana hospitali bingwa nchini hawajuhi walisemalo? vile vile amesema alikuwa na tatazo la kupoteza fahamu wakati mwingine na alikuwa na tatizo hili muda mrefu sana lakini hakujuwa lilikuwa linasababishwa na kitu GANI - baada ya uchunguzi wa kina ndiyo kakutwa ana pia tatizo la Sinusitus ambalo anatakiwa afanyiwe operation.

Katika maelezo yako one could read between the lines kwamba huko sceptical na maelezo ya ZITTO sasa kama wewe unajuwa zaidi kinacho msumbuwa ZITTO basi tujuze sisi wana JF.
 
mimi nawapa big up Muhimbili, mtazunguka kooote kuliwa hela mwisho wa yote Muhimbili. Tafadhali tuzidi kuipa vifaa vya kutosha hospitl yetu kwani pale kuna VICHWA haswa

True ...na private hospitals nyingi ....huwalia wagonjwa pesa wakiona wanaanza kushindwa malipo wanawake refer muhimbili.....wakifa sifa mbaya inaenda muhimbili...alll in all wagonjwa wengi wanaenda muhimbili when it is already too late...
 
Siamini kama agakhani walishindwa kweli lakini it may be a trick

Siyo trick mkuu, hawa watu aidha hawajali au hawana watalaam wa kweli katika mahabara, mimi na familia yangu yamekwesha tutokea zaidi ya mara nne - wanakwambia huna malaria! ukienda Muhimbili au Hospitali nyingine unakutwa una malaria. Pale naona ni majengo tu na samani kuvutia wateja basi sasa hivi nafikilia mara mbili kabla sija enda pale, siyo kwamba nawasema vibaya lakini kuna tatizo pale - wanapenda sana kukulundikia midawa chungu mzima hili mwajili wako aingie gharama tu, lakini ukichunguza sana unakuta midawa yenyewe aina kazi yoyote ya muhimu.
 
Siamini kama agakhani walishindwa kweli lakini it may be a trick

Sidhani kama kuna trick, ni wagonjwa wengi wanaopima Malaria AKH hawaonekani na malaria. Wenyewe wanadai wanatumia technologia ya juu ambayo hata kama ulikuwa na malaria kwa week mbili nyuma wataweza kuiona lakini hilo limethibitishwa si kweli. Mimi nilipeleka mtoto akiwa na homa kali na anatapika, alipewa panadol syrup na antibiotic, tuliamua kufanya vipimo hosp zingine mbili zote waliconfirm kuwa ana malaria. Hatukutumia antibiotic, baada ya kutibu Malaria miezi zaidi ya sita imepita mtoto amepona kabisa.
miaka ya nyuma ni hosp hii hii ilivunja uchumba wa mtu kwa kusema ni muathirika wa Ukimwi wakati siyo kweli.
 
Daaaaaah! afadhali Mh Kabwe umetupatia taarifa kupata mwanga wa ilivokuwa na hali yako ya sasa. Ugua pole. Jah will guide you!

Una uhakika ni yeye?, kupewa tu historia ya kuanguka anguka wooote mmeamini nice2 ni Zitto, leo akifa bila kuthibitisha hii taarifa sitaamini milele!, hamjui utendaji wa Mafia nyie!
 
Kamanda tupo pamoja
Mungu ni mwema Asante kwa kututoa hofu Allah akupe afya njema ili urudi na uendelee na majukumu
 
Una uhakika ni yeye?, kupewa tu historia ya kuanguka anguka wooote mmeamini nice2 ni Zitto, leo akifa bila kuthibitisha hii taarifa sitaamini milele!, hamjui utendaji wa Mafia nyie!
nice2 ni zito. Na hii ni style yake ya kuandika. Na kwamba nice2 ni zito sisi tulijua siku nyingi. Wewe ndo unajua leo? any way, cha msingi hapa tumwombe apone. Period. We need you, kaka.
 
Kwa kweli inashangaza sana Kama hospital inayoaminika Kama Agakhan...inategemea panadol kumtibu mgonjwa...then we are finished...naweza kuamini wakati mgumu alioputia mheshimiwa Zitto,kwa kweli maumivu ya kichwa sio mchezo.....pole sana!

As of operation..especially ya kichwa ni ngumu pia ..it's a last resort hapa ndipo sala zinahitajika tena sana.......operation ya kichwa ni ngumu kuliko hata ya moyo(open heart surgery).....na Mara nyingi..Kama kunaweza kupatikana dawa hula bora zaidi kuliko operation........mtakumbuka kuwa hata rais wetu analo tatizo la kichwa .....nerves ....pamoja na Kutakiwa kufanya operation...ameamua Kuishi kwa dawa.....

So let's pray for our dude...mtu wetu Zitto....

KWA KWELI AGHAKHAN HOSPITAL WAMENISHANGAZA INA MAANA ANGEWA HATA KUFA YAANI HOSPITAL INAYOAMINIWA KUWA NZURI NA INAKURA SANA HELA ZA VIONGOZI WA SERIKALI KWA MAANA HIYO FEDHA YA WALIPA KODI HAINA HATA CITY SCAN!

tENA AGHAKAN BEI ZAO ZIKO JUU MNO!! nA TENA UKIENDA PALE NA BIMA YA AFYA NDIO BEIZ ZAO ZINAZIDISHWA KARIBU MARA TATAU YA BEI YA KAWAIDA!

INABIDI ICHUNGUZWE HASA KATKA BEI WANAMLIPISHA MTU MWENYE BIMA YA AFYA TUSIPOKUWA MAKINI HII HOSPTILA ITAIFILIZI BIMAYA AFYA TUTARUDI KULE!!!!!!!
 
Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

Mwanzo

Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Hali kubadilika

Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

Hali kuwa Mbaya

Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Sijafa

Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

Ndugu yenu

Zitto

Pole sana ndugu yangu na naibu katibu wangu. I sent you a prophetic word thru JF and asked close friends to bring it to you. Nimuhimu sana ukasoma ule ujumbe na kumwamini Mungu kwa operation hiyo. Naomba tufanye maombi ya makubaliano mimi na wewe kuomba rehema kwa Mungu hiyo operation iende vizuri. Lakini kumbuka kuwa spiritually the problem is already solved kwa maana siyo fatal tena kama ilivyokuwa mwanzoni. Manifestation ya God's healing inategemea imani ya mtu baada ya ile neema ya kwanza ya Mungu ku-spare your life mpaka ukafika India. Mtu yeyote asikudanganye nawe pia usione ilikuwa ni kawaida tu wewe kufika ukiwa mzima no ni neema na rehema za Mungu. Mungu mara zote hapendi kushare utukufu wake na mtu yeyote anataka sikuzote abakiwe mwenye kuheshimiwa na kuabudiwa ndiyo maana kila unapopata uhakika wa mkono wa mungu juu ya kitu chochote basi inampendeza yeye kama utashuhudia na siyo kuchukulia kama kawaida.

Niliandika kuanzia pale utaanza kupata relief ya ajabu na mwenye uhakika na hilo ni wewe mhusika whether this is true or just my feelings/hisia. Sasa iwapo moyoni unapata ushuhuda kuwa yes this was what happened then my dear brother agree with me you need to take a step of faith. Kabla ya operation if you think you need basi kumbuka kuomba rehema ya Mungu maana adui haendi mbali anapofukuzwa, bali husubiri nafasi ikitokea basi huita wenzake saba na ndipo hali ya baadaye huwa mbaya zaidi kuliko ile ya mwanzo.

Nimeendelea kufanya maombi kwaajili yako na leo nahitimisha maombi haya kwa ibaada pamoja na mchungaji wangu ambaye aliungana nami kukuombea wewe pamoja na baba yangu ambaye pia ni mgonjwa. Majibu ya Mungu ni kuwa; "Hutakufa bali utaishi uyatangaze matendo makuu ya Mungu".

Mungu akubariki huko uliko na neema yake iwe juu yako Amina!

http://www.youtube.com/watch?v=-DdgkvnsHjM&NR=1
 
Back
Top Bottom