Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Mungu akuponye kaka urudi sana na upasuaji huo pia Mungu asimame ukapate nguvu mapema tunakupenda sana kaka zitto tunakuombea pia sana nashukuru kwa maelezo yako tumeelewa na amani tunayo ila zaidi tunakuombea afya njema kaka
 
Pole sana ndugu Zitto kwa matatizo ispokua nina machache ya kujadili. Ninakumbuka wakati muheshimiwa rais alipotokea na tatizo la kuanguka pale jangwani kwenye campain wako waliotilia shaka uwezo wake wakuliongoza taifa.

Ktk maelezo ya ndugu Zitto kama ni maelezo yake kweli ameeleza kua anatatizo hilo la kuumwa na kichwa kwa takriban miaka kumi lakin hakuna aliemshauri ajiunzulu. Kulikoni?

In any case pole sana zitto na tunamuomba muumba aipe familia yako subira.
 
Pole sana mh. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na akuponye maradhi yote yanayokusumbua.
 
Mwenyezi Mungu mkubwa,ashukuruwe kwa kila jambo,kila mtanzania alistushwa na hali yako.kwa upande wangu nilistushwa na taarifa kuwa umeaga dunia,kwa kweli mimi pamoja na wapenda mabadiliko mkoani Shinyanga tulichanganywa na taarifa hii.Juhudi zako kwa mkoa wetu huu wa Shinyanga kila mmoja ni shahidi,umahiri wako katika kujenga hoja,na upiganiaji wa haki za wanyonge ndiyo bubujiko lililowakuta wana wa Shinyanga na vitongoji vyake.Nilipata taarifa hizi kutoka kwa mwendesha daladala lakini sikuamini kwani sikuwa na taarifa za ugonjwa wako.Naamini kila analopanga mwenyezi Mungu hakuna binadamu wa kulipangua,japo kila nafsi itaonja mauti.Mh. Zitto nakuatkia siha njema na Mungu akutangulie kwa kila hatua utakayopiga kuelekea hatua ya mabadiliko.sisi wana wa nchi hii tupo bega kwa bega kukusupport bila unafiki.Aluta continua mapambano bado yanaendeleaBy SAMMOSSES
 
So ina maana kama wange mdiagnose mapema,then angetakiwa kuzingatia haya.....

Kutokana na maelezo ya Zitto,tatizo hilo limekuwa likimsumbua na hakujuwa kuwa hiyo ni sinusitis hadi ilipogundulika juzi kabla ya kupelekwa India.

Na kwahivyo daktari huyo hakuona umuhimu wa kufuata ushauri huo hapo juu,ametoa ushauri wa surgery kabla hata hawaja jaribu kumtibu through those ways kama inavyoshauriwa.

Surgery ni last option kama walizingatia matibabu ya sinusitis na hayakufanya kazi.

Ama kumtibu malaria ndiyo wana maanisha kuwa walikuwa wakiitibu hiyo sinusitis?

Bado naona kuna ukurupukaji wa kiana,sijui wa kulaumiwa ni nani?

Tatizo alilonalo Zitto halikuwa tatizo la kusumbua watu vichwa na hata kutumia gharama zote hadi India.Inaonyesha kabisa tuko hovyo hovyo.

Hakuna taratibu za kufuatwa kama a civilised society!

Mtu anaumwa one thing lakini anatibiwa something else,halafu wanapogunduwa hilo,bado hawajaribu kushughulikia tatizo jinsi lilivyo,yani this time try to contain the sinusitis proplem before opting for a surgery which should be the last resort!Imenikumbushia sana ile issue ya mgonjwa aliyehitaji upasuaji wa mguu alipopasuliwa kichwa instead!Na ilikuwa hapo hapo Muhimbili!
Ndugu Mushi,

Nafikiri kuna sehemu muhimu ya maelezo ya Mh. Zitto yanamtoa lawamani Dr aliyeona akatibiwe India na Afanyiwe Operesheni.
Kwanza daktari aliyemuona amefanyakazi yake vizuri kwa kujua Zitto anaumwa nini na kuelewa ni matibabu gani anatakiwa yafanyike na kilichomkwaza ni zana za kufanyia hiyo operesheni hakuna na huko hakumfanyi yeye kutokuwa Dr Bingwa kwani ubingwa wake ameshauonyesha kwa kujua tatizo na kuelewa jinsi ya kutibu na pamoja na kukosa zana ameelewa wapi anaweza akapata huduma na kumpeleka huko na kama zana zingekuwepo angefanya kwani anaweza .Kwa mujibu wa mgonjwa tatizo lake lina zaidi ya miaka kumi na hivyo tayari ni sugu yaani Chronic hivyo hayo matibabu menginine hata ukifuata huo mtiririko wa kutibu yasingemsaidia na hicho nafikiri ndicho kilichopelekea na Dr Kuamua ufumbuzi ni operesheni na hili pia linathibitishwa na mgonjwa kupatwa na severe headache kama sign ya complication ya ugonjwa kwamba nasal drainage system yake imeziba suluhisho ni upasuaji na sio utumiaji wa madawa ambayo yanatibu Acute Sinusitis.Kitu kingine yeye mwenyewe mgonjwa hajawahi kwenda kutafuta huduma kwa Dr Bingwa hata mara moja zaidi ya kwenda Agakhan huko nyuma kwa matatizo mengine ya kiafya,Dispensary ya Bunge,na pengine zahanati ya chuo wakati alipopata tatizo hilo akiwa chuo.Tatizo ninaloliona mimi si weledi na utambuzi wa Madaktari Bingwa wetu bali kutokuwepo kwa vitendea kazi na hilo ni wajibu wa serikali ambao ndiyo wamiliki wa Hiyo Hospitali ya Taifa na wabunge ambao ndiyo wanatakiwa kuwasaidia wananchi kuomba serikali ifanye mwaberesho kwenye hiyo hospitali na ikiwemo ununuaji wa zana au vitendea kazi kwa ajili ya tiba kwa wananchi hasa ukizingatia wabunge ni wawakilishi wetu. .
 
Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

Mwanzo

Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Hali kubadilika

Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

Hali kuwa Mbaya

Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Sijafa

Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

Ndugu yenu

Zitto

Wishing you speedy recovery!
 
Angalau sasa nimekuwa mwepesi kwa taarifa hii, nakutakia afya njema Mwenyezi Mungu akujaalie urejee kwenye mapambano..
 
Pole Zitto. Hop utarudi nyumbani salama. Tunakuombea upone haraka.
 
Dah kila raia angekuwa anapewa huduma na attention kama hii......2015 lazima niingie kwenye ligi ya kuongeza thamani ya maisha.

Kila la kheri Muhishimiwa Zitto. Ukishapona usisahau kuwajengea uwezo hao wa Muhimbili pia. Inawezekana wajomba au wajukuu zako wasipate bahati ya kwenda India..who knows?
 
pole sana mheshimiwa,mungu atakupa nafuu inshaallah,jua tu kwamba kuna watanzania zaid ya milioni40 wanakuombea upone.
 
Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

Aga Khan wameshindwa ku-diagnose (kugundua) malaria???......

Nakutakia uponyaji wa haraka ndugu yangu Zitto.
 
Pole sana kamanda mungu akujalie afya njema ili uwahi kurudi kabla ya kikao cha bunge kuanza
 
pole sana mh, hope u wl be fine soon coz we pray 4 u and stl we need u, viongozi wengine wajifunze kuweka mambo wazi coz suala la kuumwa ni kwa binadamu yeyote ili kuondoa sintofahamu na suala zima la kuanza kupiga ramli katika zama hizi za science and technology. pole it will recover soon after surgery mkuuu
 
pole saaana kamanda zito mungu yu pamoja nawe utapona na kurudi salama. ila kwa nyie mnaopenda kwenda kupima malaria agha khan msithubutu nafahamu toka 2002 kwamba vipimo vya aga khan huwa havitambui malaria hata iweje utaambiwa huna malaria
 
Kwa mimi kutoka kwako napata jipya la kujifunza kwamba ukiwa kiongozi, kutoa taarifa kwa watu wako ni muhimu na hasa suala lenyewe linapohusu afya yako. Huu ni mfano wa kuigwa kwa sababu kama mtumishi wa watu (Public Figure) una wajibu kwa wapiga kura wako kwani wao wanakuchukulia kama kifaa muhimu na adimu hivyo kwa taarifa uliyotoa unawaweka katika hali nzuri na kuwapunguzia hofu. Ukizingatia sintofahamu nyingi zinazolikabili taifa hili kwa sasa.

Nakuombea afya njema, urudi salama na uendelee na moyo huo huo, na pia katika pilika zako ukumbuke na ujali kwamba wengi wa watanzania tuko nyuma yako kwa matumaini ya utendaji uliotukuka.

Kila la heri na mungu yuko nawe kwa mambo ya haki unayo na utakayokuwa unayatenda kwa niaba ya wananchi na tanzania yetu kwa ujumla, pengine muda wa ukombozi ni sasa na miongoni mwa machine za ukombozi tunazozitegemea ni pamoja na wewe. Hivyo umakini wako binafsi katika mienendo yako kwa ajili ya kutunza afya yako na usalama wako kwa ujumla ni jambo ambalo tunalitegemea na tunaomba uuone umuhimu wa hili. Na mungu atakusaidia...Amin
 
Ndugu Mushi,

Nafikiri kuna sehemu muhimu ya maelezo ya Mh. Zitto yanamtoa lawamani Dr aliyeona akatibiwe India na Afanyiwe Operesheni.
Kwanza daktari aliyemuona amefanyakazi yake vizuri kwa kujua Zitto anaumwa nini na kuelewa ni matibabu gani anatakiwa yafanyike na kilichomkwaza ni zana za kufanyia hiyo operesheni hakuna na huko hakumfanyi yeye kutokuwa Dr Bingwa kwani ubingwa wake ameshauonyesha kwa kujua tatizo na kuelewa jinsi ya kutibu na pamoja na kukosa zana ameelewa wapi anaweza akapata huduma na kumpeleka huko na kama zana zingekuwepo angefanya kwani anaweza .Kwa mujibu wa mgonjwa tatizo lake lina zaidi ya miaka kumi na hivyo tayari ni sugu yaani Chronic hivyo hayo matibabu menginine hata ukifuata huo mtiririko wa kutibu yasingemsaidia na hicho nafikiri ndicho kilichopelekea na Dr Kuamua ufumbuzi ni operesheni na hili pia linathibitishwa na mgonjwa kupatwa na severe headache kama sign ya complication ya ugonjwa kwamba nasal drainage system yake imeziba suluhisho ni upasuaji na sio utumiaji wa madawa ambayo yanatibu Acute Sinusitis.Kitu kingine yeye mwenyewe mgonjwa hajawahi kwenda kutafuta huduma kwa Dr Bingwa hata mara moja zaidi ya kwenda Agakhan huko nyuma kwa matatizo mengine ya kiafya,Dispensary ya Bunge,na pengine zahanati ya chuo wakati alipopata tatizo hilo akiwa chuo.Tatizo ninaloliona mimi si weledi na utambuzi wa Madaktari Bingwa wetu bali kutokuwepo kwa vitendea kazi na hilo ni wajibu wa serikali ambao ndiyo wamiliki wa Hiyo Hospitali ya Taifa na wabunge ambao ndiyo wanatakiwa kuwasaidia wananchi kuomba serikali ifanye mwaberesho kwenye hiyo hospitali na ikiwemo ununuaji wa zana au vitendea kazi kwa ajili ya tiba kwa wananchi hasa ukizingatia wabunge ni wawakilishi wetu. .

Ndugu Kazi ndiyo kipimo cha utu,sina shida yoyote na daktari huyo.Hata hivyo hapo chini nimekubandikia tena,ugonwa huo kuwa cronic unaweza kujulikana kwa dalili na si lazima muda kama unavyodai hiyo miaka 10.Dalili za cronic sinusitis ni hizo hapo chini...
At least two of the following signs and symptoms must be present for a diagnosis of chronic sinusitis:
  • Drainage of a thick, yellow or greenish discharge from the nose or down the back of the throat
  • Nasal obstruction or congestion, causing difficulty breathing through your nose
  • Pain, tenderness and swelling around your eyes, cheeks, nose or forehead
  • Reduced sense of smell and taste
Isipokuwa mtiririko huo wa kutibu ni wa cronic sinusitis,na hizo hapo juu ni dalili zake.Kwa hiyo miaka 10 hajawahi kupatiwa tiba yoyote ya sinuistis zaidi ya ile ya malaria.

Kwahiyo miaka 10 alikuwa anajuwa kuwa ni cronic sinutis?Jibu la wazi ni "no"
Nadhani daktari aliassume kuwa nyakati hizo Zitto alijuwa ni sinusitis inamsumbua.

Kiutaratibu,surgery huwa ni option ya mwisho.

Nakubaliana na hoja kwamba tuboreshe idaya zetu za afya na vitendea kazi.However sikubaliani na wewe kuhusisha miaka kumi ya kuuguwa kwake na cronic sinutis.Kitaalamu wanasema ina last 12 weeks despite treatment attempts...
Chronic sinusitis is a common condition in which the cavities around nasal passages (sinuses) become inflamed and swollen. Chronic sinusitis lasts 12 weeks or longer despite treatment attempts.
Also known as chronic rhinosinusitis, this condition interferes with drainage and causes mucus to build up. If you have chronic sinusitis, it may be difficult to breathe through your nose. The area around your eyes and face may feel swollen, and you may have throbbing facial pain or a headache.
Chronic sinusitis may be caused by an infection, but it can also be caused by growths in the sinuses (nasal polyps) or by a deviated nasal septum. Chronic sinusitis most commonly affects young and middle-aged adults, but it also can affect children.
Na hizo treatment attempts hazikuwa za sinusitis,for 10 years hakujuwa,ama hawaku i diagnose.Na kwa mujibu wa Zitto,dalili ambayo ameitaja na inaendana na maelezo ya ugonjwa huu ni headache peke yake.Mengine hatujui.Inawezekana alipatwa na homa iliyosababishwa na sunsitis.Sasa sijui hiyo sinusitis ina uhusiano gani na malaria.Ndipo hapo sometimes ni kuchanganyana tu.
 
Back
Top Bottom