Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Kwakuwa hamtaki tuulizie hali ya Mh Zitto,kwa vile anatoka CDM,basi tujuzeni hali ya Mwkyembe na Mwandosya,ila kwa akili ya kibinadamu ilikuwa ni jambo la busara tu kwa aliyepost uzi kutaka kujua hali ya kamanda.tutumie busara
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri Mh. Zitto na tunakuombea upone haraka. Ila nina swali kwa Dr Kimaryo, Namfahamu ni Dr mzuri sana wa ENT. Wakati anasoma pale KCMC, mbona sinusitis walikuwa wanazishughulikia sana? kwa nini hakushauri kwenda KCMC au KCMC nao wameanza kufulia?
 
Ningekuwa mimi baada ya kutoka huko Mhimbili na Aghakani ningeelekea kwa prof.Majimarefu.
 
...Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).
...Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.
...Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale.
... madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria


... nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ...Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. ... Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu.
Hivi ile kesi ya yule jamaa aliyeonekana ana VVU pale AK wakati hana, iliishia wapi?
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Zitto atoboa siri ya kinachomsibu [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Sunday, 30 October 2011 20:50 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

NI UGONJWA WA KIPANDA USO, UMESHAMWANGUSHA MARA NNE
Kizitto Noya na Fredy Azzah
Mwananchi
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amebainisha tatizo linalomsibu akisema madaktari wamemweleza kwamba anasumbuliwa na ugonjwa wa kipanda uso unaofahamika kitalaamu kama sinusitis ambao kwa hatua uliokuwa umefikia, tiba yake isingepatikana nchini.Kutokana na kubainika kwa maradhi hayo, amesema anatarajia kufanyiwa upasuaji wakati wowote kuanzia sasa huko India anakotibiwa.Zitto alieleza hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, katika ulingo wa wazi wa majadiliano ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika wenye zaidi ya wanachama 3,110.

“Tatizo lililogundulika ni sinusitis, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya, Dk Kimaryo (wa Muhimbili) akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' (upasuaji) na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni,” alisema Zitto.

Naibu Kiongozi huyo wa upinzani Bungeni, alisema kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo Dk Kimaryo alishauri apelekwe India ambako kuna daktari bingwa mpasuaji wa ugonjwa huo...
“Baada ya kuwa malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya dozi niliyopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza dozi hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.”

Juzi, Zitto alipelekwa India baada ya kufanyiwa uchunguzi wa maradhi yanayomsumbua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alibainika kuwa na vijidudu 150 vinavyosababisha ugonjwa wa malaria.
Sunusitis ni ugonjwa gani?

Akizungumzia ugonjwa huo, Dk Idd Mujungu wa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga alisema ni ugonjwa unaofahamika na wengi kama kipanda uso.

“Kwenye kichwa cha mwanadamu kuna matundu ya hewa ambayo kitaalamu yanaitwa simus. Kipanda uso kinaweza kuyaziba matundu hayo kama ni cha siku nyingi na ikifikia hatua hiyo, upasuaji ni lazima.”

Alisema dalili nyingine za kipanda uso ni mgonjwa kutokwa machozi, kichwa kuumwa sana, macho kuwa mekundu na kuwa na mafua makali.

Alianza kuugua miaka 10 iliyopita
Zitto alisema tatizo hilo lilimuanza takriban miaka 10 iliyopita na katika kipindi chote hicho, amepoteza fahamu na kuanguka mara nne.

“Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, mara ya pili Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001, lakini ilikuwa usiku.
Mara ya tatu nilikuwa chumbani Hall II, mara baada ya kutoka ‘prep’ (kujisomea), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge," alisema na kuongeza:

“Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa Ijumaa tarehe 20, (Oktoba, mwaka huu) Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa mamlaka za maji nchini.”

“Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya ikiwamo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.”“Siku ya Jumapili saa 11:00 jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla.

Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba dereva wa mheshimiwa Mhonga (Saidi Ruhwanya Mbunge wa Viti Maalumu Chadema), anifuate ili anisaidie kunifikisha nyumbani.”

“Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Aga Khan Hospital na nikapata huduma. Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku.

Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.”

“Nilipita Aga Khan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.”

“Siku ya Jumanne, niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini siyo vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi. Ilipofika saa 6:00 nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!” Alisema alipelekwa tena Hospitali ya Aga Khan na vipimo kubainisha kuwa alikuwa na joto la nyuzi 39.8 na kupatiwa matibabu.

Alisema usiku wa Jumatano hali ilikuwa mbaya na joto lilipanda tena kufikia nyuzi 40 na kichwa kilianza kuuma zaidi na kuongeza... “Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

”Alisema wageni waliofika kumjulia hali wakati hali inabadilika walikuwa Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC)... “Walishauri mara moja nihamishiwe Muhimbili.”

“Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi (William, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge) na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika chumba wanachokiita mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni alikuwapo hospitalini tayari,” alisema.Alisema usiku huo alifanyiwa vipimo upya... “Ikaonekana nina wadudu wa malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana daktari kijana Dk Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale mini IC
U.”
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Zitto atoboa siri ya kinachomsibu [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Sunday, 30 October 2011 20:50 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

NI UGONJWA WA KIPANDA USO, UMESHAMWANGUSHA MARA NNE
Kizitto Noya na Fredy Azzah
Mwananchi
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amebainisha tatizo linalomsibu akisema madaktari wamemweleza kwamba anasumbuliwa na ugonjwa wa kipanda uso unaofahamika kitalaamu kama sinusitis ambao kwa hatua uliokuwa umefikia, tiba yake isingepatikana nchini.Kutokana na kubainika kwa maradhi hayo, amesema anatarajia kufanyiwa upasuaji wakati wowote kuanzia sasa huko India anakotibiwa.Zitto alieleza hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, katika ulingo wa wazi wa majadiliano ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika wenye zaidi ya wanachama 3,110.

Tatizo lililogundulika ni sinusitis, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya, Dk Kimaryo (wa Muhimbili) akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' (upasuaji) na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni, alisema Zitto.

Naibu Kiongozi huyo wa upinzani Bungeni, alisema kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo Dk Kimaryo alishauri apelekwe India ambako kuna daktari bingwa mpasuaji wa ugonjwa huo...
Baada ya kuwa malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya dozi niliyopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza dozi hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Juzi, Zitto alipelekwa India baada ya kufanyiwa uchunguzi wa maradhi yanayomsumbua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alibainika kuwa na vijidudu 150 vinavyosababisha ugonjwa wa malaria.
Sunusitis ni ugonjwa gani?

Akizungumzia ugonjwa huo, Dk Idd Mujungu wa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga alisema ni ugonjwa unaofahamika na wengi kama kipanda uso.

Kwenye kichwa cha mwanadamu kuna matundu ya hewa ambayo kitaalamu yanaitwa simus. Kipanda uso kinaweza kuyaziba matundu hayo kama ni cha siku nyingi na ikifikia hatua hiyo, upasuaji ni lazima.

Alisema dalili nyingine za kipanda uso ni mgonjwa kutokwa machozi, kichwa kuumwa sana, macho kuwa mekundu na kuwa na mafua makali.

Alianza kuugua miaka 10 iliyopita
Zitto alisema tatizo hilo lilimuanza takriban miaka 10 iliyopita na katika kipindi chote hicho, amepoteza fahamu na kuanguka mara nne.

Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, mara ya pili Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001, lakini ilikuwa usiku.
Mara ya tatu nilikuwa chumbani Hall II, mara baada ya kutoka prep (kujisomea), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge," alisema na kuongeza:

Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa Ijumaa tarehe 20, (Oktoba, mwaka huu) Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa mamlaka za maji nchini.

Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya ikiwamo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.Siku ya Jumapili saa 11:00 jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla.

Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba dereva wa mheshimiwa Mhonga (Saidi Ruhwanya Mbunge wa Viti Maalumu Chadema), anifuate ili anisaidie kunifikisha nyumbani.

Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Aga Khan Hospital na nikapata huduma. Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku.

Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

Nilipita Aga Khan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Siku ya Jumanne, niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini siyo vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi. Ilipofika saa 6:00 nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana! Alisema alipelekwa tena Hospitali ya Aga Khan na vipimo kubainisha kuwa alikuwa na joto la nyuzi 39.8 na kupatiwa matibabu.

Alisema usiku wa Jumatano hali ilikuwa mbaya na joto lilipanda tena kufikia nyuzi 40 na kichwa kilianza kuuma zaidi na kuongeza... Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

Alisema wageni waliofika kumjulia hali wakati hali inabadilika walikuwa Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC)... Walishauri mara moja nihamishiwe Muhimbili.

Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi (William, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge) na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika chumba wanachokiita mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni alikuwapo hospitalini tayari, alisema.Alisema usiku huo alifanyiwa vipimo upya... Ikaonekana nina wadudu wa malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana daktari kijana Dk Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale mini IC
U.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Pole sana mh. Kabwe. Kwa ushauri wangu wa bure, usifanyiwe 'upasuaji' kwa kuchelea isije kuzalisha tatizo jingine. Uzoefu unatuonyesha, ugonjwa wa kipanda uso haujapata tiba ya kisawasawa hospitalini, ila dawa yake ipo kwenye tiba za mitishamba tu, tena kwa gharama nafuu kabisa ya shs. 2,000 tu za kitanzania. Kama utadhani ni utani muulize mzee (mtu mzima) yeyote anayeujua ugonjwa huo. Tunamuomba MWENYEZI MUNGU upate nafuu haraka.
 
tatizo kubwa la viongozi wote wa T hakuna mbaye alikwisha kukiri hadharani ya kuwa ameaathrika na vvu......................kila mmoja analaumu dalili za ugonjwa badala ya kiini chake........................wasichojua kama wakianza kujitokeza tutawaheshimu zaidi kwa kutusaidia kupunguza unyanyapaaji wa waathirika uliokithiri hivi sasa......................................kwa maoni yangu Zitto is a victim of hiv but he remains in the closet........................baada ya hii operesheni bado ataendelea kuumwa na kuanguka sasa sijui atasema imekosewa? Time is the best teacher here..............
 
Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

tuache uongo wajamani sinusitis haiwezi kumdondosha mtu kwenye mazingira yoyote.............................na hakuna sauti ya kichwa kutwanga ila kunakuwa na makelele................when lies told severally tend to strike us like the real gospel truth but it is not................
 
tuache uongo wajamani sinusitis haiwezi kumdondosha mtu kwenye mazingira yoyote.............................na hakuna sauti ya kichwa kutwanga ila kunakuwa na makelele................when lies told severally tend to strike us like the real gospel truth but it is not................

Anayeumwa ndiye anajua jinsi kichwa kinavyomuuma. Wewe ulipoumwa kichwa ulisikia makelele, mwenzio kakwambia kilikuwa kama vile kutwangwa. Hata mimi niliwahi kuumwa kichwakweli, kinakuwa as if kuna unapigwa nyundo. Mgonjwa anapoeleza tatizo lake, adanganye ili iweje?
 
Back
Top Bottom