Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nice 2, Oct 29, 2011.

 1. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana JF,
  Hii ni email kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe. Nimeona ni vyema niiweke hapa ili tuweze kujua kwapamoja hali yake inavyoendelea.
  Nawasilisha,
  Nice 2


  Ndugu zangu,

  Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

  Mwanzo

  Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

  Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

  Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

  Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

  Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

  Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

  Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

  Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

  Hali kubadilika

  Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

  Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

  Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

  Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

  Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

  Hali kuwa Mbaya

  Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

  Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

  Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

  Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

  Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

  Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

  Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

  Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

  Sijafa

  Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

  Shukran
  Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

  Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

  Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

  Ndugu yenu

  Zitto
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwenyenzi mungu akujaalie heri urudi kabla ya Bunge. Tunakuitaji
   
 3. C

  Cedar Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuombea kwa Mungu kaka, Inshaalah upasuaji huo utakuwa salama na wenye matokeo mazuri.
   
 4. b

  boybsema Senior Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  pole sana kamanda!Mungu yu pamoja nawe,tunakuombea upone mapema urudi kuchangamsha mjengoni.Get well soon kamanda!
   
 5. K

  Kibanikolo Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sanaa shujaa na mtetea wanyonge,mimi ni padri nilifanya ibaada upone mapema,na Mungu akuepushe na hatari zote .Mungu atakujaria wewe na wenzako wote walioenda kutibiwa huko india amini.
   
 6. S

  Shiefl Senior Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aksante Mh Zitto kwa taarifa hii. Ni matumaini na maombi yetu kuwa Mwenyezi Mungu atakupa nguvu za kutosha kuhimili hiyo sehemu ya mwisho ya matibabu yako yaani surgery.

  Siisi marafiki zako wapenda mabadiliko tuko nyuma yako tunakuombea kwa dhati kabisa.

  Mungu akutie nguvu upone haraka na kurudi nyumbani mapema kabisa ukatuwakilishe katika Bunge linalofuata.
   
 7. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu Akupe Maisha Marefu, Umjue, Umpende, umtukikie vema na siku moja tufike sote JUU kwake mbunguni
  Pokea Uponyaji kwa jina la Yesu Kristo!
   
 8. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ashukuriwe Mungu wa neema nyingi, pole kwa tatizo hil Mh Zitto. Wanamageuzi na wapambanaji na wasio wapambanaji tunakutakia heri katika huduma ya afya utakayopewa huko India. Mungu aliyewajalia uwezo wa kitabibu mabingwa wa tiba duniani atakupitisha hapa salama. Pole sana Kombredi
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  tunakutakia afya njema Zitto. Binafsi nakuchuukulia kama kijana wa kwanza Tz kuonyesha vijana ni chachu ya mabadilko. Tunakuombea bwana mdogo.
   
 10. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  pole sana mkuu.nakutakia upone haraka.samahani mkuu hii ndo id yako mpya?vipi umeonana na mwakyembe?anaendeleaje?msalimie mwandosya.tunashukuru kwa taarifa.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,346
  Trophy Points: 280
  shetani ameshindwa tunakuombea upone mapema ili urudi na uendeleze uzalendo wako wa kupambana kwa ajiri ya nchi hii ubarikiwe
   
 12. Mbavu mbili

  Mbavu mbili JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  pole kwa yote na tunashukuru kwa kuutoa hofu umma wa Tz...koz umesema ukweli kuwa nu ugonjwa sugu ulokusumbua hata kabla ya kuwa MP....thanks ...get recored soon
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Tunakuombea urudi salama, bado Watanzania tunakuhitaji, mchango wako ni mkubwa kwa Taifa hili.
   
 14. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ngoja tuone
   
 15. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mungu akupe neema ya Afya na awasaidie madaktari wanaoelendelea kukuhumia brother
   
 16. serio

  serio JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,929
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280
  wish you a quick recovery..
   
 17. gimmy's

  gimmy's JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 2,362
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  Pole mh zitto pia asante kwa taarifa ilio nyoofu na kuondoa sintofahamu iliojaa juu ya kuugua kwako,amin amin amin nakuambia mungu u pamoja nawe!
   
 18. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Get well soon our beloved one.Inshallah
   
 19. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mungu akusaidie upone haraka mkuu.
   
 20. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana kaka Kwa taarifa hii ya kina. Tunaendelea kumuomba Mungu aendelee kukusimamia ili upone mapema.
   
Loading...