Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Tunakuombea kwa mungu upone mapema, Taifa na wapenda mabadiliko tunakuhitaji
 
pole mheshimiwa, ila ni kweli aghakan hawakuona kitu? Je wasema walichokiona? Maana hapa biashara ya watu ipo matatani.
 
Pole sana! Ni kweli, uvumi huu umetutesa watu wa jimbolako! Mungu akusaidie ili upone salama! Maji na umeme Mahembe ni matunda yako, hakika Mungu akusaidie utuletee maendeleo zaidi ya hayo. POLE SANA JEMBE LETU!
 
Aghakhan hawawezi ku-detect Malaria!!!! Aghakhan hawawezi ku-detect Sinusitis!!! Aghakhan wana thermometers za homa tu!!!

Aghakhan!!!...
 
Pole sana bro mpiganaji,Mungu ni mwema atatenda muujiza upone haraka.
 
pole mheshimiwa, ila ni kweli aghakan hawakuona kitu? Je wasema walichokiona? Maana hapa biashara ya watu ipo matatani.

Waliona homa... wakamtandika panadol kwa kwenda mbele...
 
wana JF at least tumshukuru Mungu kwa kuweza kuwasiliana na Mh Zitto,hasa kwa kutuondoa hofu iliyokuwa imetanda miongoni mwetu hasa kwa kutokuwa na taarifa rasmi juu ya kile kilichopelekewa Mh Zitto apelekwe India,na kingine mazingira yaligubikwa na usiri mkubwa kiasi kwamba hatukuwa na taarifa sahihi.
nakutakia tiba njema na upate nafuuu haraka,huku tungali tunakusubiri utuongoze kwa mapambano na uwakilishi wako bungeni.
 
Pole sana na Mungu azidi kukutia nguvu upone na urudi kuendelea na michakato.
 
Hospital ya Aga Khan bana sijui ni vipimo gani wao walikuwa wanatumia
 
Ee baba mjalie mja wako,mpe nguvu,muepushe na kila hila za shetan mtie nguvu,na ujasiri,afanyiwe operation kwa uwezo wako,uwatie ma dr nguvu waweze kukuponesha kwa uweza wake,nayaomba aya kwa jina la baba na la mwana na roho mtakatifu.AMEN
 
Ugua pole ndugu Zitto na ufikishe salam kwa ndugu Mwakyembe.Naye augue pole.Inawezekana na yeye ni ugonjwa tu wa kawaida,tunawaombea.
 
Asante sana kwa taarifa hii muhimu sana:

1. Imetuondolea wasiwasi na sintofahamu iliyokuwa imetanda
2. Imefunua mengi hasa juu ya udhaifu wa hospitali ya Agakhan-kwamba pamoja na kurudia vipimo ilishindikana ku detect Malaria!
3. Imeondoa maswali juu ya hospitali yetu ya taifa: kwamba walishindwa kutibu malaria hadi ku refer India, kumbe kuna tatizo jingine.

Get well soon and long live.
 
Mungu akuponye kaka urudi sana na upasuaji huo pia Mungu asimame ukapate nguvu mapema tunakupenda sana kaka zitto tunakuombea pia sana nashukuru kwa maelezo yako tumeelewa na amani tunayo ila zaidi tunakuombea afya njema kaka
 
Pole sana KAMANDA wetu ZITTO ZUBEIR KABWE,MUNGU akuponye maradhi yanayokusumbua,akusimamie ktk UPASUAJI utakaofanyiwa,upone na na urudi salama nyumbani kututetea.
 
Tanzania tunayoitaka ni ile ya watu wanaothamini utu wa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa. Tunamshukuru Mungu kwa wote waliokuhudumia Mhe. Kabwe, na tunamwomba Mungu akuponye kwa wakati wake ili urudi uje tuendelee na mapambano ya kuikomboa nchi yetu toka mikononi mwa watu wasiothamini utu wetu, kwa kudhani kuwa wao pekee ndo wanaostahili.
 
Nakutakia afya njema. Usiwaze sana juu ya Bunge wakati huu, relax vya kutosha ili afya yako iweze kutengemaa
 
Kuna watu wenye roho mbaya kweli,mara kafa mara ana mdudu,binadamu ni viumbe wa ajabu sana,especially watanzania.Hizo rumours za kifo mtu anazianzisha kwa nia gani haswa?
 
Back
Top Bottom