Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
CCM wafanye yote wanayofanya ikiwemo kutumia propaganda na dola kubaki madarakani, ila waeleze tatizo la ajira na ugumu wa maisha pamoja na Katiba hii mbovu tulionayo, ndio vitu vitavyokuja kuwaondoa madarakani.
Hata hivyo, ili yatimie, lazima kwanza litokee jambo ambalo litatumika kama chanzo(kivuli) cha watu ku-riot ila kitachowasukumu watu kupambana na dola ni hayo mambo matatu hapo juu.
Leo hii reaction ya wananchi kuhusu tozo kwenye laini za simu ni indicator ya awali tu au ni mfano mmojawapo wa vitu vinavyoweza kuja kutumika kama kivuli tu cha kuamsha hasira watu walizonazo katika moyo yao(watanzania wana utulivu tu lakini hawana amani).
Katiba Mpya kwa upande wake, inaweza kuja kutumika kama chanzo kikuu cha wananchi ku-riot au kutumika kama kivuli katika kuamsha hasira za wananchi kupinga ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira hasa miongoni mwa vijana.
Ni swala muda tu kabla haya hayajatimia endapo tutaendelea kuzaliana huku tukiendelea kuwa na vipaumbele vibofu katika nchi.Kibaya zaidi, tumeshatumia vibaya rasilimali za nchi kupitia mikataba mibovu na matokeo yake tumeanza kuyaona kupitia hizi kodi za hovyo hovyo.
Wananchi, hasa vijana, wasio na ajira huku wakitambua rasilimali za nchi yao zimetumika vibaya kufaidisha watu wachache, hawataitaji tuition kuelewa umuhimu wa katiba wala mlio wa filimbi kukusanyika ili kudai katiba mpya au kuondoa watawala madarakani kwa gharama yoyote.
Hivyo, kuna wakati unakuja watawala mtalazimika kuacha kupambana na viongozi wa vyama vya upinzani na wanaharakati, na badala yake mtalazimika kupambana na wananchi waliuongana bila kujali tofauti zao za kisiasa, kidini, kikabila, n.k.
Aione Mama na aiweke kwenye file lake hapo Magogoni.