Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Miaka flani niko Bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nikaongea nae kuhusu kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nikatua Jackson Heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mimi kutafuta kazi, Marekani kazi zipo ila sasa kule ukisikia kazi ni kazini kweli full supervision unafanya kazi kwa muda wa saa 10 mpaka 12, hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyewe unalipwa kwa saa, kwa hiyo lazima ukomaee ila kazi tu zipo.

Baada ya muda kudunduliza hela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa Sandy Springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa kawaida, kila kitu ni hela yaani ukisikia capitalism kule ndo inakuwa practice [emoji817]

Suala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokuwa makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi TZ sababu za kifamilia.

Maisha ya Marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au una kipaji kitu ambacho kwa Watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao.

Kwenda Marekani hivihivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata hela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda Marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, uwe competent, hivihivi sikushauri hata kidogo.

California, New York, Illinois, Massachusetts na Washington hayo ni majimbo ya kuyaepuka, kodi na gharama za maisha ziko juu ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivyomiss Marekani ni exposure ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kuna kikampuni nitaenda kukifungua deleware kama domestic company, baadae Virginia na Texas kama foreign company.
Uzi mzuri sana huu.
Afadhali umeweka wazi maana kuna watu walio wengi hawajui hizi siri wanadhani ukitua marekani tu ndio tayari umeshatoboa ni mwendo wa kula bata na wakina Jay Z.
 
Mkuu, Mzuzu. Na members wote mliochangia,Hizo green card sijui lottery mnapataje ? ,Naomba kama zinapatikana mtandaoni muweke hapa link pamoja na maelezo ili mimi na vijana wengine tujaribu bahati yetu ya maisha hapa

Ningesema natanguliza shukrani,lakini huo msaada ni mkubwa sana nitakuja nazo hizo shukrani (joke😁)
 
Mkuu, Mzuzu. Na members wote mliochangia,Hizo green card sijui lottery mnapataje ? ,Naomba kama zinapatikana mtandaoni muweke hapa link pamoja na maelezo ili mimi na vijana wengine tujaribu bahati yetu ya maisha hapa

Ningesema natanguliza shukrani,lakini huo msaada ni mkubwa sana nitakuja nazo hizo shukrani (joke😁)
www.dvprogram.state.gov
 
Fursa za kusoma ni nyingi, ni uwezo wako tu, na siku hizi applications ni mtandaoni tu.Niliingia Marekani kwa student visa.
Mkuu,naomba unielekeze hatua kwa hatua mwanzo mpaka mwisho na mimi,nina degree, hata nikija huko nikasomea course yoyote ni sawa tu hata kama ni diploma, cha muhimu mimi lengo langu ni kuja huko kutafuta maisha
 
Ahsante Mkuu ila haigunguki
Screenshot_20221023-190416.png
 
waende Russia [emoji635][emoji635][emoji635] huko. Kila Siku mmekaa mnainanga [emoji631][emoji631][emoji631] cha ajabu mnataka kwenda kuishi huko .
Baniani mbaya kiatu chake kisiwe dawa .
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mkuu,naomba unielekeze hatua kwa hatua mwanzo mpaka mwisho na mimi,nina degree, hata nikija huko nikasomea course yoyote ni sawa tu hata kama ni diploma, cha muhimu mimi lengo langu ni kuja huko kutafuta maisha
Nenda Urusi mkuu.
 
Binafsi nipo USA miaka 20 sasa. Mwanzo ilikuwa changamoto sana.. hasa kupata green card. Kweli maisha yalibadilika nilipoipata. Bila ya hio green card au uraia full.. USA mtu utateseka sana. Ukiwa na green card lakini...
1. unasoma bure degree ya kwanza... na nyingine scholarships kibao..
2. ukishasoma kama ulivyosema ndio unapata kazi nzuri..
3. ukiugua.. unapata asilimia kubwa tu mshahara wako vizuri..
4. ukipoteza kazi.. unalipwa pia fidia nzuri tu kila mwezi.. nk.
5. Unasafiri kwenda bongo bila kikwazo... nk.

Binafsi huku matumizi nimeweka chini. Upuuzi wa kushindana na WaTz wengine kununua nyumba na kubadili magari kila siku sifanyi. Investments zangu ni Tz. Na hazijaniangusha kamwe.
Wewe ni wa kipekee na uliondoka bongo ukiwa unajitambua sana waliowengi kwa miaka hiyo 20 uliyokaa hawajui hata kuelezea kitu kwa ufasaha.
 
Kule wanaita disco yaani chumba kimoja full kina toilet, Jiko,unalala hapo hapo yaani kitanda usiku mchana unakigeuza kochi.kwa mwezi kuanzia sh laki saba za tza au trump 350.ndo SAwa huku na chumba cha elf 70 kwa mwezi.Kwa mwezi ukosi kuingiza elf 2
Disco au studio?!
 
Kama Mange Kimambi
Sijui maisha ya Mange Kimambi mkuu, lakini Marekani ukiwa na makaratasi (kibali halali) cha kuishi Marekani ni vigumu kuishi kwa kuunga Unga, kwa taarifa za mitandaoni Mange aliolewa na Mmarekani, kama huyo aliyekuwa mumewe alimtengenezea kibali, basi yuko US kihalali hivyo anaweza kufanya kazi, hicho ndio kitu kikubwa Marekani, na pia kama alizaa na yule mtalaka wake, ujue anapata Child support.
Najui huyu dada hapendeki kwa wengi, lakini ukweli ni kwamba hatujui ukweli kama anaishi kwa kuunga unga.
Uzoefu wangu na Marekani ni kuwa, ukiwa na vibali halali, yaani unaweza kufanya kazi, hiyo inaweza kabisa kukuwezesha kuhimili maisha, mambo ya kujirusha hayo ni mipangilio ya mtu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom