Nyie ndugu punguzeni tabia isiyofaa. Tujenge tabia ya kutiana moyo. Nachukulia mfano hapo kwetu Tanzania, kuna baadhi ya wanafunzi hufeli ktk level tofauti tofauti, kuanzia elimu ya msingi, form two, form four, form six na hata vyuo watu wana disco ktk shule na vyuo tunavyoamini ni bora, kinachofanyika watu hutafuta namna rahisi zaidi ya kuendelea ndiposa wanatafuta vyuo mbadala au shule inayoweza kumchukua,kuna shule mbovu sana huko nyumbani, kuna vyuo vibovu sana huko nyumbani tena taasisi hizi nyingi ni za private, wao wanajali sana pesa. Vivyo hivyo hata huku China, kuna vyuo vya namna hiyo, unakuta karo ni ndogo na elimu ya hovyo, vinazoa kila mtu hii ipo hasa kwa wanafunzi wanaosoma undergraduates wengi vyuo sio vizuri.Hii haina maana kwamba China nzima wanatoa elimu mbovu,hapana. Mimi nikilinganisha elimu niliyopata huko bongo na hapa hasa ya vitendo, huku wamepiga hatua sana huenda mara 4 na zaid,tatizo ninaloliona kwa post graduates, kama utasoma kizembe, walimu hawana shida kabisa watakuacha umalize,urudi nchini kwako ila kwa wanafunzi wao wako very strick hawana mchezo,lakini kama ukiamua kusoma kwa bidii, kwanakupa support yote, utapata kila kitu na utajua vitu vingi sana. Watu wengi wamemaliza elimu za masters ulaya mfano Norway, Uholanzi hata marekani hawajui hata kuandika scientific papers wala hawajwahi kupublish kazi yake aliyowahi kuifanya hata ukimuuliza Sci. ni nini hajui kabisa.Mimi najivunia kusoma nchini China. Kuna issue ya kurudi nyumbani ukiwa na hela au unarudi bila kitu, kabla ya kwenda kusoma nchi yoyote lazima ufikiri sana unaenda kwa sababu unataka kwenda kusoma na umepata ufadhili wa kusoma elimu ya juu au unaenda kutafuta pesa. Swali hilo litakuongoza kuchagua nchi ya kwenda. Kwa china baadhi ya majimbo watu wanaruhusiwa kufanya kazi, pengine wanaruhusiwa kufanya kazi na kuishi mpka miaka minne baada ya kuhitimu (yaani hawawezi kukupa visa ya kazi na ya kusoma pamoja, lazima ucancel mojawapo). Ukija kusoma huku unawaza pesa unaweza kurudi nyumbani umechanganyikiwa. Kuna vijana wengi wamefanikiwa kwa kufanya biashara kati ya China na DSM, wengine wana makampuni n.k . China ina vyuo vikubwa tu bora mfano Tsinghua University, Peking University n.k elimu bora inaambatana na maendeleo, tujipime maendeleo yetu na China kisha turudi kudharau elimu yao.