Ushauri kwa wasanii na Organisers: Miaka 30 ya Bongo Fleva.

don-mike

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
753
Reaction score
1,505
Kabla sijaenda moja kwa moja kwenye mada husika, tour zinazofuata naomba mzingatie yafuatayo:

Gangster With Matatizo (GWM) waje waimbe – YAMENIKUTA
Big Dog Pose(BDP)
waje waimbe – MA-JOB-LESS
Mwana FA
usiache kuimba – Haina Fagio
Fid Q
usiache imba – Sihitaji Marafiki
GK
usiache imba – Tuko Pamoja na Miiko 10 ya RAP.
Solo Thang & Mr Paul
& Bob Rudala mfanye basi hata live performance over the internet iwe broadcasted jukwaani, tutashukuru sana.
Esther Wasira aje atuburudishe na – Sheila.
Unique Sisters mabinti wa Kipozi waje watuburudishe na Baishoo ft MackDizo, Kwa Sababu Gani, n.k
K-Basil & D’Knob – Mtoke kidogo kwenye madhabahu, Mje Msalimie Jukwaa. D’knob tunahitaji sikia ukiimba tena Elimu.Com, baada ya hapo ruksa kurudi madhabahuni.
Madee usiache imba – History.
Organisers Mchukueni na Mike Tee, tunahitaji kusikia swaga zake za kitambo, fleva ya pekee. Mrudisheni huyu kwenye spotlight, ni kati ya wachache ambao performance moja tu inaweza m-kickstart akaendelea na mbanga zake.
Vitali Maembe aje atuimbie – Sumu ya Teja, Salama, Litle town Bagamoyo, Kudu, n.k Hawa wanaharakati msiwatenge, kama huyu ni free spirit, hanaga shida na mtu. Yani hatokuja kwenye show alafu aka-behave kama Dudubaya.
Nyabinghi apewe zoezi la kuimba nyimbo kadhaa za Ngwair, iwe special session ya kumuenzi Ngwair, mtonyo ufike kwa familia yake na producer wake.
Ikiwezekana huko live kuwe na Namba za Kuchangia kumsapoti msanii husika, MiXX by YAS changisha inaweza Fanya hilo. Kuna watu wanaangalia mbali ila wangependa support wasanii wanaowakubali, sasa msanii akiwa anaerform, Changisha Namba yake inawekwa pia.
Bizman aje hata once tupate sikia – Ametoroka Mpenzi Wangu.

Sasa niende moja kwa moja kwenye mada.

Kwa miaka kadhaa soko la burudani Tanzania lilidorora. Wasanii wachache wa A-List ndio walikuwa wametawala kwa kufanya show za corporate. Ukitoa hao A-list, wapiga show wengine ni hawa wadogo zetu wa Singeli ambao wana niche yao (soko lao maalumu).

Lakini ujio wa Miaka 30 ya Bongo Fleva umeamsha kitu kingine. Naamini sasa ukurasa mpya wa burudani Tanzania umefunguliwa. Opportunities za kibiashara zipo ndani na nje ya nchi, especially Uganda, Congo, Rwanda, Burundi, Kenya na Zambia.

Ushauri wangu kwenu wasanii wote — na naongelea wote, Bongo Hip Hop, Bongo Fleva, R&B ya Bongo, Singeli, Mchiriku na Taarab:

TAKE THIS MOMENT SERIOUSLY.
Hii hype inaweza kuwa ya muda mfupi kama industry haitabadilika, lakini mkitumia momentum hii vizuri, mnaweza kujenga soko ambalo linaweza kuleta pesa nyingi kwa wasanii, promoters, producers, DJs, dancers, videographers, fashion designers, event companies, venues, media na brands.

TAFUTENI PROFESSIONAL CHOREOGRAPHER.
Jifunzeni tena kucheza na kulitawala jukwaa. Kuna shows ambazo muziki ni mzuri, melody ni nzuri, sound ni nzuri, beat limetulia na mashairi ni mazuri — lakini kuwaangalia wasanii mki-perform inachosha na inaboa. Basi tu tuliwamiss, na bado tunawapenda. Ndio maana mnaona hii hype. Sasa tumieni hii nafasi vizuri.
Tafuteni watu wanaojua choreography wawafundishe movements zinazoendana na nyimbo zenu. Msanii usije tu na microphone; performance yenyewe iwe sehemu ya burudani.
Kifupi tumechoka kusikia mkisema “mnanisikia”, ‘mikono juu”, “tuimbe wote” n.k. Watu wanakuja kwenye show zenu kupata burudani, na nyie ndio watoa burudani.

FANYENI MAZOEZI YA MWILI MUWE FIT.
Fanyeni mazoezi miili irudi kuwa ya kisanii, mpate pumzi ya kutosha jukwaani, Muweze kuimba, kucheza na ku-interact na audience bila kuchoka. Na kama mnapenda kuvaa pamba kali jukwaani, fanyeni mazoezi mpaka hizo pamba zikae vizuri kwenye miili yenu. Angalieni wadogo zenu, miili yao almost wote imekaa kisanii, kwakuwa mnataka kurudi ulingoni basi hamna namna.

FANYIENI MAZOEZI LIVE BAND NA LIVE PERFORMANCE.
Sio kila show DJ awe ana playback. Jengeni uwezo wa kuimba na ku-perform na live band, hii itatengeneza nafasi kubwa sana ya kubadilisha perception ya audience kuhusu muziki wa Tanzania. Muziki wetu una nyimbo nyingi zenye melody, instruments na vocal arrangements zinazoweza kuwa show kubwa sana zikipelekwa live. Inatia aibu msanii kushinda imba wimbo wako mwenyewe simply sababu hujajiandaa.

TENGENEZENI UBUNIFU NAMNA YA KUINGIA NA KUTOKA KWA STAGE.
Msanii usifikirie tu playlist ya nyimbo utazoimba, event planner akishakupa dakika utazotumia basi kwenye hizo dakika chache tenga muda wako kubuni namna utavyoingia, utavyoanza imba, namna transition ya nyimbo moja hadi nyingine, namna utavyoaga jukwaa n.k, Mashabiki wanataka experience tofauti tofauti.
mf.

Kuna show Ferouz alimuweka Doto Magari kwenye Machera, ikafanya show i-trend, watu wakiulizwa wanakumbuka nini Mwanza Tour, ni rahisi kuanza na hili tukio.
  • Juzi juzi hapa Ahmedy Ally aliingia na Simba uwanja wa taifa, miaka nenda rudi haitosahaulika
  • Ally Choki aliwahi ingia na farasi, waga haisahauliki na miaka imekimbia sana.
Show nzuri inapaswa kuwa kitu ambacho mtu anakumbuka hata baada ya kuondoka ukumbini.

RUDINI STUDIO, TENGENEZENI NYIMBO MPYA PIA MFANYE COLLABO NA WASANII WA NDANI NA NJE YA NCHI.
Tengenezeni nyimbo mpya, pia hakikisheni nyimbo zenu za zamani zinarudiwa tena studio kabla hamjazipandisha kwenye platforms tofauti tofauti, yani huko spotify, youtube, apple music, etc kuwe na nyimbo zenu zenye quality.
Kama msanii unatakiwa kuwa na Team inayotengeneza Content zako, hapa utaweza tengeneza narrative itayokuuza sokoni na kukutangaza, deals nyingi pia zitazaliwa kupitia content zako.
Jifunze market za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo na Zambia zinahitaji muziki wa aina gani, usijifungie tu ndani ya mipaka ya Tanzania.

MANAGEMENT TEAM YAKO IJENGE BIASHARA, SIO KUSUBIRI SHOWS.
Management yako iwe na watu professional kwenye booking, contracts, accounting, branding, sponsorships, merchandise, publishing, royalties, endorsements na international opportunities viwe sehemu ya mfumo.

TICKETING DATA.
Hakikisheni show zote mnazofanya ticket zinunuliwe online, hata kama ni agent anauza basi auze kupitia online platform. Na Data zinazopatikana kama namba za simu na emails, muweze zitumia mnapoandaa shows nyingine. Mfano leo msanii akitaka rudi Fanya show Arusha, hata kama anarudi peke yake, basi aweze tumia message watu waliohuzuria shows za wasanii wa nyuma. Tayari platform itaweza toa DATA za nani alikuwa ordinary, VIP na VVIP. Kama kuna offer ya kukata ticket mapema, au kukata ticket kwa group, au ku-upgrade kutoka Ordinary Kwenda VIP to VVIP, hizi data ndio zinatakiwa msaidia msanii, asianze na upya wakati tayari ana mtaji.

BRANDS & MERCHANDISE ZIANZE KUWA SEHEMU YA MUSIC BUSINESS ECOSYSTEM.
Wasanii msifikirie sponsorship kama ndio suruhisho la kufanya mambo yenu yaende.
Brand partnership & Merchandise ndio suruhu ya kipato cha kudumu. Sector nyingi sana zinahitaji huduma yenu mfano: Fashion, Telecom, Banks, Fintech, Beverages, Automotive, Airlines.Hotels, Insurance, Technology, Travel.
Hakikisha una professional image, audience data na measurable results.

Mf: Dudubaya anauza TShirt kupitia matamasha haya, akijipanga vizuri, mauzo ya Tshirt zake uraiani yanaweza zidi pesa anayoingiza kwa show.
Mf. Afande Sele – Kweli yupo mtaani kila siku anatupa tafakuri kupitia Each One, Teach One. Sasa kama angekuwa na Management ya Kueleweka, basi angepiga sana ela za wauza Mbegu, Mbole ana Miche...maana mazingira anayofanyia content zake yanazingatia sana utunzaji wa mazingira na kilimo. Hapo sana ndio anahitaji Team ya kuproduce content zenye quality ambazo anaweza zitumia kwenye deals negotiation.

KNOW YOUR RIGHTS & BOUNDARIES.
Jifunzeni kuhusu: Master rights, Publishing rights, Performance rights, Mechanical royalties na Sync licensing.
Msanii usisaini kitu kwa sababu tu umeambiwa ni deal nzuri. Elewa unachouza na unachobakiza.

TENGENEZENI CONTENT KILA SIKU, SIO WAKATI WA HII TOUR TU.
Zama zenu mlikuwa mnapambana mtengeneze Music Video nzuri mkijua Video ndio itawapeleka mjini, siku hizi mambo yamebadilika, sasa soko linataka mtengeneze video za behind the scenes, rehearsals, dance challenges, live performances, interviews, studio sessions, fan interactions na lifestyle content.
Jamii inahitaji sababu ya kuendelea kukufuatilia hata kama hujatoa wimbo mpya.

JENGENI TEAMS ZENYE WATAALAMU, SIO MARAFIKI TU.
Kwa level mlizofika mnahitaji manager, accountant, lawyer, booking agent, PR, social media/content team, creative director, choreographer, stylist producer na production team.
Sio lazima wote wawe full-time mwanzo lakini kila function iwe na mtu anayejua anachofanya.

MSIUZE CATALOGUE ZENU.
Miaka 30 ilikuwa historia na imeacha legacy kubwa. Sasa mpo ambao mshaanza uza catalogue zenu. Kamwe msiendelee, achene hilo mara moja. Hizo Catalogue ndio zitaendelea wabeba na kuwaamulia hatma za maisha yeu.
Jenga nyimbo 100 hit songs ambazo miaka 30 ijayo bado zinaweza kuchezwa. Nnyimbo zinazoweza kutumika kwenye movies, series, adverts na documentaries.

Kwa sababu mwisho wa siku, msanii unaweza kuacha kufanya shows — lakini catalogue yako inaweza kuendelea kufanya biashara.

PONGEZI:
Nikupongeze sana MADEE, sijui kama unafahamu fika ukubwa wa hili dude uliloliamsha, yani nikama viwanda vya music Tanzania vimepewa stimulus package, kwa mtu yoyote mwenye jicho la biashara tayari anaweza ona wai pa kujiingiza na kupiga ela, ndio maana mkimuona BABU TALE anacheka na kuruka jukwaani jua anafurahia kwamba hata ubunge ukifa, basi huku nje ana wigo mpana wa kupiga hela zaidi ya kiinua mgongo cha ubunge.

Ile inayoitwa MUSIC INDUSTRY ECOSYTEM sasa inaweza sukwa na upya kwa kuzingatia hali ya sasa na ajila legit nyingi sana zikatengenezwa na watu wakajiajiri na kuajiriwa kupitia hawa hawa wasanii.

KARIBU KWENYE UKURASA MPYA WA BURUDANI.
 
Hatuwataki wasanii.

Waende kwa maccm wenzao
 
Back
Top Bottom