Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Mkuu naomba nitofautiane kidogo na wewe, nafikiri ni vyema tukajadili ni kiwango gani cha msamaha tunamaanisha.
Hata usamehe vipi hauwezi kusahau kilichotokea isipokua kama umesamehe kwa nia njema na kwa dhati, hata ukukumbuka inakua haikupi shida wala kukusumbua, huo kwa mtazamo wangu ndio msamaha wa kweli.

Kama leo umenifanyia jambo baya likaniumiza na nikaamua kukusamehe, sitaweza kusahau hilo tukio ila hata kama nikikumbuka halinipi kinyongo na wewe, na wala haliathiri mahusiano na yetu. Nakubaliana na wewe kwamba hiyo hali sio kila mtu anaiweza.
Kusamehe inawezekana lakini kusahau ngumu. Kuna mtu alinikosea nilikutana naye baada ya miaka mingi na ilibidi niishi naye eneo moja na kukutana ilikuwa karibu kila siku. nilijifungia chumbani na kumwomba Mungu nimsamehe mtu guys niwe huru.
Katika hali ile ya kutulia na kumwomba Mungu nilijikuta natetemeka na kutoka jasho king sana. Nilijisikia huru
Kesho yake nikamsalimia akajibu na kubabaika sana.

Alianza kuwa karibu na kunitendea wema kwenye masuala kadhaa ambayo nilifaidika kwa kiasi fulani.

Hatuishi karibu kwa sasa ila hata ninapokumbuka sijisikii vibaya. Niko huru.

Kusamehe hasa kwa aliyekutendea jambo zito sio jambo la kusema tu namsamehe. Ni jambo ambalo lazima kujitoa kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ea22182088793d94f7d1d66b1dddcb77.jpg

Hii ya leo ni tofauti kidogo na mada zetu zile , hii inahusika na kulipa kisasi.
Katika maisha bila kujali unaamini nini hakuna jambo jema kama kusamehe! Msamaha hukusaidia mengi mpaka kifo na maisha yanayofuata baada ya kifo iwe reincarnation au rebirth nk !msamaha hukufanya uwe mwema mwenye furaha ya kweli usiye na makunyanzi rohoni na usoni.
Mwenye msamaha ana nuru usoni , msamaha ni tiba, msamaha ni mafanikio msamaha ni amani na ni upendo.
Lakini je kama huamini katika msamaha? Kama unayemsamehe hasameheki? Na je kama ni mbabe mjuaji na dhulumati mkubwa?je kama anakuletea dharau kwa hali yoyote ile hata uwe msamehevu kiasi gani? Usiishi na maumivu! lipa au lipiza..!
Msamaha wako usikushushe msamaha wako usikufanye kiumbe dhaifu na mnyonge, utu wako ni muhimu heshima na dhima yako ni vitu vya kulinda na kuzingatia mno...ukishindwa kabisa kusamehe ukizidiwa na viwango vya uvumilivu wa kibinadamu usiumize roho yako andaa kisasi.
Kama ilivyo kwa msamaha ile nafuu unayoipata kwenye kusamehe basi ndivyo ilivyo hata kwenye kisasi! Kisasi humpa mtu faraja na amani ya moyo huridhika kuona amefanya jambo baya kwa mtu mbaya.
Tunaishi na wajuaji wengi kwenye jamii tunaishi na watu wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wao ni zaidi kuliko wewe...wao ndio wanaijua pesa kuliko wewe. . . . usimpe nafasi mtu wa namna hii atambe...ni lazima umfundishe ajue kuwa maisha yana pande nyingi...kisha mfundishe kwa maumivu makubwa maumivu atakayodumu nayo mpaka kifo.
LAKINI maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua... Fanya kile kitakachokupa nafuu ya rohoni na afya ya akilini kwakuwa uamuzi ni wako na mwisho utabaki wewe kama wewe..
Visasi misamaha na malipizi vitabaki kuwa uamuzi binafsi kutokana na imani yako hofu yako na huruma yako.
kusamehe ni kitendo cha hekima na upeo mkubwa wa kuchanganua makosa ya mwenzio ili maisha yasonge mbele kwasababu hakuna asiyekosea. Ikiwa wewe ni mtu wa kulipa kisasi je moyo wako utafurahi pale utakapomkosea mwenzio naye akaamua kulipa kisasi? Kama jibu ni hapana basi tuishi kwa kusamehe.
 
kusamehe ni kitendo cha hekima na upeo mkubwa wa kuchanganua makosa ya mwenzio ili maisha yasonge mbele kwasababu hakuna asiyekosea. Ikiwa wewe ni mtu wa kulipa kisasi je moyo wako utafurahi pale utakapomkosea mwenzio naye akaamua kulipa kisasi? Kama jibu ni hapana basi tuishi kwa kusamehe.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
mwenye huruma hana BAHATI hapo unampa m2 msamaha basi yeye anjipanga ili mda mwingne asifanye makosa na wewe ndo utakua umekwisha kama sio kuachwa na maumivu makari zaidi ya mwanzo
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji19][emoji19][emoji19]
 
Kuna wakati inabidi tuangalie na upande mwingine kwakuwa msamaha ni kitu cha kiimani zaidi sasa mtu asiye na imani umwambie asamehe atakushangaa sana BTW kuna baadhi ya imani zinahamasisha visasi, mfano kwenye satanism hawajui kitu kinachoitwa msamaha
c732d8c867816bbf31678dd0a529083e.jpg
Kuna ukweli

Ili kuondoa uchungu ts either forgive or revenge

Mi nikiweza i revenge
Nisiloweza ndo nasamehe
 
Umenikumbusha jambo hapa, kuna jamaa last year nilimkopesha bidhaa akanizungusha pesa hakunilipa nikamsamehe deni ila kwa masharti simuuzii bidhaa hata akija na cash. Kupanga ni kuchagua.
Hongera sana total cutoff
 
Mie kuna mtu nashindwa kumsamehe na nashindwa kusahau nikifika kwenye kulipa kisasi dini inakataza nimebaki njiapanda.Hili jambo ni kweli na usiombe likakukuta.
Sisi wala mbwa huku nakuvizia nikuue au nichome nyumba yako ukiwa umelala umelala humo ndani then nikijua umekufa na Mimi najimaliza kwa njia nayojua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom