Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Msamaha ni udhaifu... Ukiwa mtu wa kusamehe bas utakufa mapema tu coz maumivu ya kukosewa/kudhulumiwa huwa hayaishi na hayatoisha hata ufanyeje na mwisho wa cku utakata tamaa na kuona kwanin unaonewa wew tu kila cku, Na nature jinsi ilivyo itakutafuna na udhaifu wako mpaka ufe BUT Kisasi ndio kina-mfanya mtu aione thamani yake, Kujiamini na kuishi kwa furaha na amani coz unajua kabisa kwamba No one can mess around with you
 
Point
 
ea22182088793d94f7d1d66b1dddcb77.jpg

Hii ya leo ni tofauti kidogo na mada zetu zile, hii inahusika na kulipa kisasi.

Katika maisha bila kujali unaamini nini hakuna jambo jema kama kusamehe! Msamaha hukusaidia mengi mpaka kifo na maisha yanayofuata baada ya kifo iwe reincarnation au rebirth nk !msamaha hukufanya uwe mwema mwenye furaha ya kweli usiye na makunyanzi rohoni na usoni.

Mwenye msamaha ana nuru usoni , msamaha ni tiba, msamaha ni mafanikio msamaha ni amani na ni upendo.

Lakini je kama huamini katika msamaha? Kama unayemsamehe hasameheki? Na je kama ni mbabe mjuaji na dhulumati mkubwa? Je kama anakuletea dharau kwa hali yoyote ile hata uwe msamehevu kiasi gani? Usiishi na maumivu! lipa au lipiza..!

Msamaha wako usikushushe, msamaha wako usikufanye kiumbe dhaifu na mnyonge, utu wako ni muhimu heshima na dhima yako ni vitu vya kulinda na kuzingatia mno. Ukishindwa kabisa kusamehe ukizidiwa na viwango vya uvumilivu wa kibinadamu usiumize roho yako andaa kisasi.

Kama ilivyo kwa msamaha ile nafuu unayoipata kwenye kusamehe basi ndivyo ilivyo hata kwenye kisasi! Kisasi humpa mtu faraja na amani ya moyo huridhika kuona amefanya jambo baya kwa mtu mbaya.

Tunaishi na wajuaji wengi kwenye jamii tunaishi na watu wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wao ni zaidi kuliko wewe. Wao ndio wanaijua pesa kuliko wewe. . . .

Usimpe nafasi mtu wa namna hii atambe, ni lazima umfundishe ajue kuwa maisha yana pande nyingi kisha mfundishe kwa maumivu makubwa, maumivu atakayodumu nayo mpaka kifo.

LAKINI maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Fanya kile kitakachokupa nafuu ya rohoni na afya ya akilini kwakuwa uamuzi ni wako na mwisho utabaki wewe kama wewe.

Visasi, misamaha na malipizi vitabaki kuwa uamuzi binafsi kutokana na imani yako hofu yako na huruma yako.
Hapa nakuunga Mkono
 
Umena vyema mkuu binafsi siamini katika visasi visasi vinaumiza sana vitakufanya huishi kwa hofu coz utakuwa na muendelezo the best thing in kugive up and forgive and walk away

Unachoongea ni kweli ila kuna vitu vinaumiza sana hasa makazini we unafikir ni rahis kuvumilia wenzio wanapeana tu mashavu ya ku Songa na kua matajir wewe Upo tu apo ofisin kama mlingot huonekan wala hushirikishwi kitu mbona wenyewe wanavokufanyia hayo hawaishi kwa hofu wala hawakuwazii...

Binafsi sema hao watalaam wenyewe siku hizi hakuna lkn wangekuwepo wa uhakika tungenyooshana tu
 
Kama kisasi huwezi kulipa kisasi wapige majungu kwa boss, wakurugenzi, mameneja, sema hata uongo 😀
 
Back
Top Bottom