Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,655
- 729,745
Hii ya leo ni tofauti kidogo na mada zetu zile, hii inahusika na kulipa kisasi.
Katika maisha bila kujali unaamini nini hakuna jambo jema kama kusamehe! Msamaha hukusaidia mengi mpaka kifo na maisha yanayofuata baada ya kifo iwe reincarnation au rebirth nk !msamaha hukufanya uwe mwema mwenye furaha ya kweli usiye na makunyanzi rohoni na usoni.
Mwenye msamaha ana nuru usoni , msamaha ni tiba, msamaha ni mafanikio msamaha ni amani na ni upendo.
Lakini je kama huamini katika msamaha? Kama unayemsamehe hasameheki? Na je kama ni mbabe mjuaji na dhulumati mkubwa? Je kama anakuletea dharau kwa hali yoyote ile hata uwe msamehevu kiasi gani? Usiishi na maumivu! lipa au lipiza..!
Msamaha wako usikushushe, msamaha wako usikufanye kiumbe dhaifu na mnyonge, utu wako ni muhimu heshima na dhima yako ni vitu vya kulinda na kuzingatia mno. Ukishindwa kabisa kusamehe ukizidiwa na viwango vya uvumilivu wa kibinadamu usiumize roho yako andaa kisasi.
Kama ilivyo kwa msamaha ile nafuu unayoipata kwenye kusamehe basi ndivyo ilivyo hata kwenye kisasi! Kisasi humpa mtu faraja na amani ya moyo huridhika kuona amefanya jambo baya kwa mtu mbaya.
Tunaishi na wajuaji wengi kwenye jamii tunaishi na watu wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wao ni zaidi kuliko wewe. Wao ndio wanaijua pesa kuliko wewe. . . .
Usimpe nafasi mtu wa namna hii atambe, ni lazima umfundishe ajue kuwa maisha yana pande nyingi kisha mfundishe kwa maumivu makubwa, maumivu atakayodumu nayo mpaka kifo.
LAKINI maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Fanya kile kitakachokupa nafuu ya rohoni na afya ya akilini kwakuwa uamuzi ni wako na mwisho utabaki wewe kama wewe.
Visasi, misamaha na malipizi vitabaki kuwa uamuzi binafsi kutokana na imani yako hofu yako na huruma yako.