Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Habari wapendwa wa MMU,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote.

Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanyabiashara kwahiyo kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani.

Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend.

Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi katika pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! Nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao.

Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaiyo nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tu. Nimemtafuta sana, jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei.

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu ninayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.
Wanaume wa Dar hao katika ubora wao
 
Acha kujifariji so unafurahia matatizo ya mwanamke mwenzio kisa we hupendwi? Hupendwi bibi wee
Duuh nimesoma comment zako lkn nimeshindwa kukuvumilia mbona unamshambulia mwanamke mwenzio wakati weww ndio ungemfariji kipindinhiki kigum kwake? Yes kuna.makosa kafanya lkn si hivyo unavyomfanyia bwana unamtonesha vidonda
 
Mie sio fisi... Mi ni binadamu & nna utashi. Natongozwa daily na watu wa nguvu tu... Sema tu kupenda hakuchagui.
Huenda ni kweli kwamba baada ya x wa kwanza hukuwahi kupenda kwa dhati tena ila ninachokiona wewe ni mwanamke.mzuri sana mrembo uliyeumbika vzr na umekuwa ukitumia nafasi hiyo kuwachuna watu na kuwadanganya waliojitokeza wote kwa dhati.

Kwa kuwa hukuwa na hisia za kupenda kwa dhati ilikiwa ndio advantage yako ndio maana na wengine wameendelea kurudi kukuulizia.msimamo wako.
Now karma is f...king.
 
Nimechelewa kwenda lunch kwa ajili ya comment za watu na majibu ya mtoa mada.

all in all nimegundua mtoa mada sio mgeni sana humu ameweka tu new ID or

mtoa mada ni mstarabu kuliko mnavyomfikiria.

Hii ni kwa sababu, majibu yake humu ndani ni ya kistaraabu according to me.

Asanteni.
&according to me mtoa mada anaweza kuwa ni wewe.
 
Eboh! Kwani nimekataa? Kwani ye ndio wa kwanza? Na wala sio wa mwisho. Nimetuma post ili nishauriwe jinsi ya kukabiliana na hali nnlonayo. Najua kwamba hanipendi, nimeshaona picha na kuisoma namba. Nimependa kwa dhati na hio ni shida yangu, sio yake. Sijipendekezi na wala sitajipendekeza kwake. Kilichonisukuma kumtafuta ni hisia zangu za mapenzi. Hizo ndio napambana kuzi-overcome. Nikiweza, nachapa lapa. Kwani dushe, pesa na umaarufu ni kwa ajili yake tuu? Mapenzi hayachagui ndugu. Soo, please don't judge me.
Mkuu, naona tatizo la wanao ku judge lipo kwenye maneno uliyo tumia kuwaslisha mada yako na baadhi ya response zako. Maneno kama, mtu maarufu,... Mwenye uwezo,..... Mwana Siasa,..... Ndo chanzo cha comments za aina hiyo.
 
Sikuwahi kutegemea kama nitashobokea mtu maarufu, haukuwa mpango wangu na kweli nilijizuia sana. Ila mapenzi yakija hayaangalii status, sura, rangi, kabila, umri wala nini. Don't judge me, u don't know me.
Haya yakishatokea ndio utamsikia mwanamke akisema mapenzi hayaangalii sura, status, rangi, kabila wala nini, lkn wakati ukiwa under 27yrs i guess you could'nt say this.
Anywaysa pole sana
 
Mpaka nimalize kusoma comment zote 360+ kwa akili yangu kali kama sumu ya nyoka ntakuwa nishakuelewa wewe ni mtu wa aina gani na.pengine haya yanayotokea ni matokeo ya tabia yako mwenyewe, blame no body neither the maa.

Bibie...Kupenda mtu inachukua muda. Sikurupukagi hata siku moja. I take my time to see if there's chemistry or not. Mie sio mwanamke wa kushobokea mtu kisa pesa & umaarufu. Nimezaliwa kwenye pesa, najua kuzisaka hazinipi kiwewe. Na kama kudate matajiri, nimedate... ningekuwa nawehuka na utajiri si ningeshaolewa long time? Halafuu naanzaje kumtafuta mtu ambaye sijampenda? Alinitongoza yeye na kuniomba nafasi kwa adabu kabisaaa. Hio ni baaada ya kuona sishobokei chenchi zake au umaarufu wake. U feel me? Hunijui, don't judge me!
 
Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo.

HUYO ATAKUWA MSAGA SUMU.Tafuta maziwa Dada kashakunywesha sumu kasepa
Au mkuu wa mkoa huyu nini halafu atakuea ni ccm naana ndio wenye pesa za.kuvulia chupi dada za watu
 
Hahahha talking from experience, kumbe na wewe yalikukuta?? Hicho ndio tunaita kuwa so selective mwisho wa siku unavua sana chupi.
Hongera maana itakuwa ulivua sana lkn mwisho wa siku somo umelielewa. That is nature, God created creatures to obey orders and rules from which it was created. When you go against then you must face the quencequences
Imewahi kunitokea na nimeshajifunza my dear.Unachotakiwa kuwa makini ni uhakikishe mwanaume amekupenda yeye.Sio amekutamani .Amekupenda
Tena na wewe ulivyo na msimamo ukipata anayekupenda hatobanduka nakwambia ukweli kutoka moyoni mwangu.
Mwanaume akifa akioza kwako you love him back kuliko kusubiri utayempenda wewe.Huyo ni imaginary husband hayupo duniani.Hata mimi naelekea kuolewa na mtu anayenipenda sana ila mimi nampenda kawaida.Naamini ndoa itakuwa nzuri coz hatanisababishia kichaa.
 
You are so obsessed with money that where your trap is, you think money can give you all things.
Sure! Nimeghairi kabisaa swala la mahusiano kwa sasa. Nimeamini hakuna cha mapenzi wala nn. Pesa mbele! Kwa sasa, nazichanga tu. Nikizikusanya za kutosha, watakuja tuu. Siki hizi wanaume hawaangalii tena sura, shepu, tabia, na vile vigezo vingine. Naona kibao kimegeuka, hata wanaume wanaangalia pochi kama imejaa au la. Soo, wacha nisake maela. Nkishakuwa nazo, nami ntafanya kuwatumia tu... Wai!
 
MMU ina hazina ya watu wenye mpaka.jicho la tatu, umeonaeeh anaonekana anadharau na huyo man amefanya kurevenge ukizingatia hakua kapuku kama wengine.
Muretee Unasema Mi sijawai pendaaa Thubutu...mbona we naona hujapenda mpaka unashika Simu unaandika Mimi nilipata Love insane....uchizi Wa mapenzi....nikasimama Na Masomo...iyooo iilikuwa kitambo...sasa kwa kuyajjua mambo hayoo yalicyoo ndoo Maana nikkakwambia straight bila hayaa..halafu my Sweety friend Murete ni kwamba una matter sijasema huwezi pata hapana la hasha unapata but chances zinapunguaa Unajifananisha.Na Akina JLo. mwenzangu hukoo.Ni Developed Country..Na Hapa Ni Developing country.
don't dare to Compare my Diaaaa...Halafu..usijidanganyewala usisemee Eti Hajakwambiaaa angekwambiaa tu.Upo Dunia Gani my love...sasa huyo Ndo aliyekuacha kuliko hata waliokwambia...kifupi IPO ivi..we Kuna wanaume huwa hauwapendi au unawapuuza huwa hata ukiona SMS zao au calls zao hujisumbui.nao..unaona...so that shit man of yours is gone for good...
 
Mkuu, naona tatizo la wanao ku judge lipo kwenye maneno uliyo tumia kuwaslisha mada yako na baadhi ya response zako. Maneno kama, mtu maarufu,... Mwenye uwezo,..... Mwana Siasa,..... Ndo chanzo cha comments za aina hiyo.
Mkuu... Nimemuelezea huyu mtu kwa sifa hizo kwa kuwa ninatoa picha halisi yake ili nishauriwe na sio kuhukumiwa. Ningetoa mtazamo wake mwingine lakini sijui zaidi ya huo. Sijaishi nae wala kudate nae nipate nafasi ya kujua upande wake mwingine was maisha. Kwa hio, kumpa mtu sifa nisizojua ni kusema uongo ambao usingenisaidia. Yamkini hata mawaidha mengi ya wadau yangekuwa tofauti.
Asante
 
Haya yakishatokea ndio utamsikia mwanamke akisema mapenzi hayaangalii sura, status, rangi, kabila wala nini, lkn wakati ukiwa under 27yrs i guess you could'nt say this.
Anywaysa pole sana
Nimejielezea saaana mkuu. Lakini naona bado unaendelea kunihukumu. Ni mwanaume huyox2 alinitenda na kufanya nisipende tena kwa dhati. Sawa, mie mzuri. Kama wanakuja wenye uwezo, mie niwakatae kisa nilitendwa? Nawakubali, nawatumia kweli kweli. Na vilex2, sikuwa tayari kuolewa before 30. Tena kwa kweli, nilibadilisha mawazo pale nlipopatana na huyu maarufu nlipoamini uongo wake. Otherwise, ndoto za kuolewa sikua nazo at all... Haikuwa priority na pia sio hata sasa.
Asante
 
Kwa kweli stori yako inasikitisha lkn no way yameshatokea
Lkn ushuei ni huu, usijitamkie maneno mabaya juu ya nafsi yako, sio vzr kujiapiza eti wewe hutapenda tema kwa sasa hutaki mpenzi na Mungu anaweza akamleta mtu sahihi kipindi hikihiki.
Nimejielezea saaana mkuu. Lakini naona bado unaendelea kunihukumu. Ni mwanaume huyox2 alinitenda na kufanya nisipende tena kwa dhati. Sawa, mie mzuri. Kama wanakuja wenye uwezo, mie niwakatae kisa nilitendwa? Nawakubali, nawatumia kweli kweli. Na vilex2, sikuwa tayari kuolewa before 30. Tena kwa kweli, nilibadilisha mawazo pale nlipopatana na huyu maarufu nlipoamini uongo wake. Otherwise, ndoto za kuolewa sikua nazo at all... Haikuwa priority na pia sio hata sasa.
Asante
 
Kama vile husivyo na hisia na wale wanaokupenda kweli waliotayari kupeleka posa,ndivyo hivyo huyo maarufu hasivyo na hisia na wewe.Na hapo ndipo linatimia lile neno maarufu kuwa unapopendwa hupendi na unapopenda hupendwi.Huo ndio mchezo wa mapenzi ulivyo mtamu
Swali! Nna uhakika gani wako serious?! Jee kama nao ni matamanio tu yanawatuma kutoa ahadi hewa? Pia, inawezekana wapo siriaz kweli, lakini mimi sijavutiwa na hata mmoja. Kwanini nijipe adhabu kisa nataka ndoa? Sio lazima ndugu yangu. Anaweza mtu akatoa posa kabisa alafu akaghairi tena huoni hilo litaniumiza zaidi? Tena sio mimi tu, hilo hadi familia litawaumiza.
Asante
 
You are so obsessed with money that where your trap is, you think money can give you all things.
I'm not at all.. I've been raised in a wealthy family. I saw it's ups & downs at some point where money is involved. I know the hardships of surviving without a penny. I am just airing my views here that now I'd better keep working hard because I realised that in today's world one is worthy when he/she is rich. So abeg, yes define me however you want but that's my stand. But money is not everything in this world. We only need it to live a life of satisfaction. No body likes to be poor, even yourself!
 
Mkuu miezi 8 ni midogo? Maanake mi nimekuja kumgawia utamu baada ya miezi 8. Tena ilibidi aunde story kwamba gari yake imegongwa, driver wake atadili nalo ili apande langu. Otherwise, inawezekana asingekaa akaona papuchi yangu ng'o!
Murete
Nimekusoma inaonekana wewe bado mtoto kimaisha.
Unaongea nini sasa hapa??!!
Hiyo inaitwa... "Ningejua"
Wewe nakushauri tafuta mtu ambaye kwa watu watamuona mshamba ila wewe uwe una mpenda kikubwa lakini sana yeye awe anakupenda utafurahia maisha. Achana na watu maarufu na hao dada zako walikuuza.
Hukutakiwa kujirahisisha vile.
 
Murete
Nimekusoma inaonekana wewe bado mtoto kimaisha.
Unaongea nini sasa hapa??!!
Hiyo inaitwa... "Ningejua"
Wewe nakushauri tafuta mtu ambaye kwa watu watamuona mshamba ila wewe uwe una mpenda kikubwa lakini sana yeye awe anakupenda utafurahia maisha. Achana na watu maarufu na hao dada zako walikuuza.
Hukutakiwa kujirahisisha vile.
Asante kwa busara zako Kiraka. Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom