Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Mkuu asante kwa mchango wako. Hayo ni maono yako na nnayahesimu. Ilaa, ucheap wangu uko wapi? Au labda ni kwa vile nilitafutiwa baadae na mtu wangu, dadangu? Coz mimi sikukumbuka hata kuchukua namba yake in the first place. Na hata nlipoipata sikuanza mimi kumtafuta. Je, ningemkubalia na kumpa shoo the same day aliyonitongoza ungeniitaje kwa mfano?

Angekuita "Whore"
 
Sasa unafiki na uchawi unatokea wapi? Kisa nimekwambia ni bora mwanaume akupende? Hayo ni mawazo yangu .......kama unayaona hayafai unayaacha tu.

Na hata ndiyo naweza kuwa na mwanaume anayenipenda mie nisimpende mana hata biblia inasema wanaume wapendeni wake zenu....na wanawake waheshimuni waume zenu........mie nitamweshimu ila jukumu la kunipenda ni lake yeye mwanaume.....

Ndiyo maana unalilia hapa mana unachukua jukumu la mwanaume ..... Wewe unatakiwa kumweshimu.

NB.
Umenikuta sijazimua.....

Murete
Nakuomba chukua point hapa hata kama hutaki.
 
Hahaaaaa Murete bila maneno makali huwezi msahau huyo mjinga mjinga, af siku nyingine usijitoe mzima mzima hivyo, mapenzi yashaisha kitambo

Si kweli akipata atakayempenda nae ampende kwa moyo wote.
 
Good observation na ndio tulipo sasa afanyeje?
Hata hivyo hapa sote hakuna tunachokijua maana kasema tu jamaa kakaa kimya sasa mtu anakaaje kimya bila sababu yoyote from nowhere tu mtu ana mute.
 
Swali! Nna uhakika gani wako serious?! Jee kama nao ni matamanio tu yanawatuma kutoa ahadi hewa? Pia, inawezekana wapo siriaz kweli, lakini mimi sijavutiwa na hata mmoja. Kwanini nijipe adhabu kisa nataka ndoa? Sio lazima ndugu yangu. Anaweza mtu akatoa posa kabisa alafu akaghairi tena huoni hilo litaniumiza zaidi? Tena sio mimi tu, hilo hadi familia litawaumiza.
Asante
Kama vile ambavyo wewe haujavutiwa na hao wanaotaka kupeleka posa na hupendi kujipa adhabu kuishi na mtu husiye mpenda ndivyo yule mchumba maarufu tajiri hajavutiwa na wewe na hapendi kujipa adhabu ya kuishi na mtu hasiyevutiwa naye.Ukisema sasa utajuaje kama hao wapeleka posa wako serious sasa hutaolewa wewe!.Basi kapige ramli ili ujue kabisa wako serious au hapana.
 
Tatizo lililopo apa Dar es salaam Tanzania. Au sehemu nyingi za mjini ni kwamba wanawake wanataka kushindana na wanaume na ndio maana wengi wanaachwa #Solemba# mkipendwa mnazingua sana mnatakiwa kufanya wanaume wawe watumwa wenu
Mfano mzuri angalia madada zetu wa apa Dar es salaam walivyozibuka vichwa unaenda kumtambulisha kwenu kila mtu anabaki kichwa kinagonga unakuta mwanamke Mlevi, mmbeya, msengenyaji, mgomvi mgomvi, mjeuri na anataka kwenda na Wakati kila nguo na simu inayotoka anataka awe nayo. Alafu kingine anataka akale viepe vya beka ataki kupika yeye saloon na club kwenda mbele na makampani ya mashoga zake. Yaani apa Dar es salaam. Tunaoa basi lakini wanawake vichwa vimezibuka tayari.
Mdogo wangu Mr. Blue bayser kapata mke bora tumpongeze jana tarehe 15.04.2016 kafunga ndoa
 
Hahahha talking from experience, kumbe na wewe yalikukuta?? Hicho ndio tunaita kuwa so selective mwisho wa siku unavua sana chupi.
Hongera maana itakuwa ulivua sana lkn mwisho wa siku somo umelielewa. That is nature, God created creatures to obey orders and rules from which it was created. When you go against then you must face the quencequences
Sijawahi kuwa selective na yaliyonikuta hayahusiani na kuvuliwa chupi mkuu usikariri.Usilolijua ni kama usiku wa giza usipende kutoa conclusion kwenye comment ya mtu usiyemjua.Asante.
 
Nimejielezea saaana mkuu. Lakini naona bado unaendelea kunihukumu. Ni mwanaume huyox2 alinitenda na kufanya nisipende tena kwa dhati. Sawa, mie mzuri. Kama wanakuja wenye uwezo, mie niwakatae kisa nilitendwa? Nawakubali, nawatumia kweli kweli. Na vilex2, sikuwa tayari kuolewa before 30. Tena kwa kweli, nilibadilisha mawazo pale nlipopatana na huyu maarufu nlipoamini uongo wake. Otherwise, ndoto za kuolewa sikua nazo at all... Haikuwa priority na pia sio hata sasa.
Asante
Kuolewa hisingekuwa priority husingekuja kulia huku dada.Wewe kaa subiri ushauriwe,tatizo lako unataka watu waongee unavyotaka kusikia watu wakiongea tofauti unasema wamekuhukumu.
 
Jamaa alicheza kama Pele, kaweka mpira kichwani kaususha kifuani kauseti chini kaburuza mpira kafunga goli!! Dada siyo lazma kuolewa bhana jikite kwenye busness zako uje uwe Malkia Wa Nguvu
 
Kama vile ambavyo wewe haujavutiwa na hao wanaotaka kupeleka posa na hupendi kujipa adhabu kuishi na mtu husiye mpenda ndivyo yule mchumba maarufu tajiri hajavutiwa na wewe na hapendi kujipa adhabu ya kuishi na mtu hasiyevutiwa naye.Ukisema sasa utajuaje kama hao wapeleka posa wako serious sasa hutaolewa wewe!.Basi kapige ramli ili ujue kabisa wako serious au hapana.
Mh! Haya.
 
Kuolewa hisingekuwa priority husingekuja kulia huku dada.Wewe kaa subiri ushauriwe,tatizo lako unataka watu waongee unavyotaka kusikia watu wakiongea tofauti unasema wamekuhukumu.
Sawa Musigaji. Nawasikiliza. Asante kwa ushauri
 
Habari wapendwa wa MMU,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote.

Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanyabiashara kwahiyo kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia. kwa akili hizo badala ya kumchuna we unaona wanaume wanapenda ndoa....... asilimia kubwa wanaume hawapendi ndoa

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani.

Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend.

Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi katika pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! Nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao.

Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaiyo nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tu. Nimemtafuta sana, jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei.

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu ninayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.
 
We hutumii akili unatunia hisia....we unasubiri statement ndio ujue msimamo wake.. .we jua huna chako hana ti.e na weae jiongezeee pata potea we fursa jaribu zote sie wanaume hatuoi tu mpaka tuwe settled......amka we sio wa miaka 18
 
Hata hivyo hapa sote hakuna tunachokijua maana kasema tu jamaa kakaa kimya sasa mtu anakaaje kimya bila sababu yoyote from nowhere tu mtu ana mute.

Mimi ni mwanaume nakuhakikishia huyo jamaa hakuwa na nia na bibie. Na kukaa kwake kimya ndio jibu lake hataki kumuumiza bibie au anataka baadae arudi tena kugonga. Lakini kwa uhakika hana mpango nae.
 
Mimi ni mwanaume nakuhakikishia huyo jamaa hakuwa na nia na bibie. Na kukaa kwake kimya ndio jibu lake hataki kumuumiza bibie au anataka baadae arudi tena kugonga. Lakini kwa uhakika hana mpango nae.
Inawezekana!
Ila kama ni kuniumiza ameshaniumiza, amenivuruga full. Sidhani ataweza kurudi tena kwa kweli. Hata shetani atamshangaa.
 
Kama mwNaume nakujulisha kuwa hataki kukutamkia ili usiumie sana ila hana time na wewe naungana na kiraka
 
Kama mwNaume nakujulisha kuwa hataki kukutamkia ili usiumie sana ila hana time na wewe naungana na kiraka
Sawa mkuu, ila anachofanya ni sawa na kuua kwa kunyonga badala ya kutumia bastola. Kusema kweli angesema tu ingenipa ahueni kubwa sana kuliko kukaa kwake kimya. Maumivu ya ukimya wake ni makali na ya mateso kuliko angesema straight.
Asante kifimbo!
 
Back
Top Bottom