Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Inawezekana!
Ila kama ni kuniumiza ameshaniumiza, amenivuruga full. Sidhani ataweza kurudi tena kwa kweli. Hata shetani atamshangaa.
Murete
Wewe hujui inaonekana... sasa kwa taarifa yako huyu jamaa ni mmoja wa watu ambao wanaweza kuja kukugonga hata kama utakuwa mke wa mtu.
Ata rudi atakupa sababu mujarabu ya ukimya huu utalainika atakula mzigo.
 
Asee... Mpaka ifikie wakati huo, atakuwa kageuka adui mkuu. C unajua when love turns to hate? Labda arudi saivi, but a few months ahead he'll be my no.2 enemy. Si Utani, naelekea kumchukia mnoo...
 
Huyu sio msaga sumu kweli maana alikua bega na lowasa au atakua motochini na magufuli
 
Last Activity: Apr 13, 2016 at 4:10 PM
Joined: Monday
Messages: 2
Likes Received: 1
Trophy Points: 3
Gender: Female
Birthday: October 11
Hivi ulisema wewe ni msomaji mzuri wa JF?
Msomaji mzuri as Guest then akajiunga ili achangie...rudia kusoma tena...
 
Habari wapendwa wa MMU,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote.

Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanyabiashara kwahiyo kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani.

Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend.

Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi katika pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! Nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao.

Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaiyo nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tu. Nimemtafuta sana, jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei.

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu ninayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.
Network search...
 
Mkuu hakurudi tena... Ilaa, kuna wakati alinivuruga kidogo. Aliandaa party nikaenda kumpa support kama watu wengine tu. Huko nlimkuta na huyo girlfriend wake but akawa na wasiwasi sana. Hakutulia kabisa siku ile. Alidhani nitaenda kumchafulia party yake but mi sikua na mpango huo. Alipoona najichanganya na wala sileti vurugu akaanza yeye kuzingua. Akaninyima nisicheze na guys wengine kisa anaona wivu. Na ali-admit kabisa kwangu. Mi nikavunga. Since that day....
Hatua ya kwanza...kaa kimya...mchunie...alafu ngojea reaction yake...akiwa kimya na wewe kaa kimya....na akiendelea kuwa kimya basi ujue hukua na chako.....sepa!!
 
Hatua ya kwanza...kaa kimya...mchunie...alafu ngojea reaction yake...akiwa kimya na wewe kaa kimya....na akiendelea kuwa kimya basi ujue hukua na chako.....sepa!!
Asante mkuu.
Nimenyamaza, nimemuachia Mungu. Yeye ndio hupanga, cc ni kuchagua tu
 
Pole sana dada,, sipendi kuhukumu lakini napata mashaka sana. Alichogundua jamaa kaona hukumpenda yeye ila umependa story zake kutoka kwa ndugu zako,, uliyasaliti maamuzi yako ya kukaa kimya kwa mtu aliyekudharirisha kwa kukutongoza leo na kuomba gemu leo akiamini jina lake mjini litamsapoti

Na jamaa kama alivosema ana mtu wa dhati ambaye ni chaguo la moyo na wewe alikutaka ili kukamilisha dhambi ya binadam si mkamilifu kwa kukutamani ila kwenye kipimo haumo kabisaaaaa,
Haiwezekani aliyekutamani kwa kuzima moto wa hitaji la siku moja uwe mke, hata siku moja aseee kwani alijua wewe ulivo unastahili kwa matumizi ya jojo,, nakula sasa hivi ikishaliwa inatemwa tena hutupwa kwenye chombo cha taka kisichohitaji kumbukumbu isijechafua sakafu kwani mabaki ya jojo ukikosea pa kulitupa huganda mahali pale, kama wewe ulivotaka kuganda kwake,
Ujue kabisaaaa ulishatumika na umebaki kama mabaki kwake dizaini ya jojo,, sasa hakukutupa ila alikupa kazi ya gundisha magazeti kwenye mageto ya ya washikaji njia inayotumika sanaa huko kijijini,, sasa amesakafia moyo wake na kaamua kutumia super glue badala ya wewe mabaki ya jojo japo alama za jojo hazitoki hata wewe nadhani umebaki kichwani mwako ila hakukumbuki

Take action, ukizingatia umri wako uko nje ya sifa za kuoa kwani umebakiza miaka 12 tuuau kumi na na tano kusitisha uwezo wako wa kuzalisha mayai,, hivo yawezekana kapiga hesabu kaona bora usepe ila wewe hujiongezi na kosa sio lako no la moyo wako ulioshawishiwa na ndugu zako

Onyo
Siku zote simamia msimamo wako ndio mungu hua amepanga ufanyeje hivo, lakini akiingilia mwingine unapoteza uelekeo,, cha kufanya fanya haraka kutafuta mwingine azibe pengo jamaa kashasepa

Kama ungekua moyoni mwako ulipomwambia unatolewa posa angehaha yeye wewe ungeona jinsi alivo na juhudi

Ikumbukwe kua
Mwanaume hua anajivunia alichotafuta kwa jasho sio kilichojireta akishaamini kilienda kama ulivofanya wewe ulienda akaamini umetoka umerudi anatimiza wajobu tuuuu sio kukiamini tena
 
Asante kwa mawaidha mkuu
 
Sawa mkuu, ila anachofanya ni sawa na kuua kwa kunyonga badala ya kutumia bastola. Kusema kweli angesema tu ingenipa ahueni kubwa sana kuliko kukaa kwake kimya. Maumivu ya ukimya wake ni makali na ya mateso kuliko angesema straight.
Asante kifimbo!
Nimekupata pia mkuu upo sWa.....akiwa kimya inabidi upande wa mwanamke ujue maana nadhani ashajua....jPo angeambiwa ingekuwa poa n clear
 
huyo mtu maarufu huu ujumbe ungeupeleka kule jukwaa la CELEBRITY angepata ujumbe wako kuwa unamtafuta
 
Duh unauliza kitu gani hapo mbona uliachwa long sana sema jamaa anatamani aendelee kumega kiaina siku zikisogea mbele
 
Duh unauliza kitu gani hapo mbona uliachwa long sana sema jamaa anatamani aendelee kumega kiaina siku zikisogea mbele
Ndio maana ya kukaa kimya[emoji15] ?!
 
Wanawake bhana me hata siwaelewagi

We first time amekutongoza akaomba game bado hujamjua huyo jamaa ni wa aina gani. Anakuambia anagirl friend anampenda bado hujajua tu kusudi, mwisho wa siku ameomba game simple jamaa limegegeda afu apokei cm zako bado hujajua. Alafu unamiaka 33 we itakuwa mchaga unataka ela za huyo jamaa
 
Back
Top Bottom