Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Oooiii utajua wewe endelea kungangania after short piriod njoo tupe mrejesho umefkia wapi na loshuuko wako!
Ndio maana niko hapa kupata mawazo ya watu tofauti mkuu. Siwezi kung'ang'ania nisipopendeka. I'm still hot & sexy. I'm brave too... Haya ni mapito tu.
 
Hawezi kukuoa wewe sababu wewe ni cheap nadhan ndo maneno magumu ambayo inabidi uyakubali hlf uyafanyie kazi.... 1st day kakutongoza hlf kataka kukulala siku hiyo hiyo I wish ungeingia kwenye kichwa chake ujue alikuchukuliaje mpk akakufuata na approach hiyo ya kidharau kias icho au labda unaonekanaje? Safi ulimkataa sasa ulivyo mpuuzi friends wame kidanganya kichwa chako kwamba jamaa ni expensive go get him ni sawa kusema kwamba unampenda Najua wanawake hawajui wanachokipenda ila in short Najua mnapenda mwanaume expensive sasa unapataje kitu expensive while u ar cheap sasa hapo ndo hamjuagi mfanye nn na hasa tatizo lako ndo hilo nkushauri hv inabid ujue kua expensive na kutetea thamani yako full stop, mapenzi ni game tu una laki mfukoni unataka kumiliki benzi we kichaa?unamfutaje mtu aliye kuchukulia wewe kua ni demu wakutongozwa Leo na kugongwa Leo eti unadai thamani yako kwake! Hata nguo ya mtu ukitaka ipate kwa bei rhs njooo kidharau hv as if huna shida nayo uone unavyoipata kirahisi sasa toka na approach yako ya kipuuzi hivo hivo nenda mliman city ishushe thamani nguo uone km itakusaidia kupunguzwa bei..... Huu mwimbo na imba kila siku ht kwa dada zangu home acheni upuuzi jueni thamani zenu hizo hisia zenu bila akili mtagongwa mpk mkome na ndoa ng'oooo
 
Milk is everywhere yesterday, today, tomorrow, always, now and then!..... Should i keep a cow???? Wanawake acheni hako katabia ka kutoa papuchi mapema, inatuwekea ugumu sana sisi wanaume kuoa!...... Acheni hiyo tabia, siyo issue kabisa!..... Mnasababisha waoaji wanapungua!!
Mkuu miezi 8 ni midogo? Maanake mi nimekuja kumgawia utamu baada ya miezi 8. Tena ilibidi aunde story kwamba gari yake imegongwa, driver wake atadili nalo ili apande langu. Otherwise, inawezekana asingekaa akaona papuchi yangu ng'o!
 
Ni rahisi kwa mwanamke kumwambia mwanaume bila chenga kwamba hamuhitaji, hamtaki tena ama wavunje mahusiano, ila kwa mwanaume huu ni mtihani mgumu sana, ila ukiona kimya kingi ndio hvo gari imeacha njia.
 
Mkuu miezi 8 ni midogo? Maanake mi nimekuja kumgawia utamu baada ya miezi 8. Tena ilibidi aunde story kwamba gari yake imegongwa, driver wake atadili nalo ili apande langu. Otherwise, inawezekana asingekaa akaona papuchi yangu ng'o!
Baada ya dada yako kukushauri kuwa umpende ndo ilipita hiyo miezi nane kabla ya kumpa utamu au hiyo miezi nane ni kutokea kule mwanzo alivyokutongoza ukakataa?
 
mh...ndg waswahili wanausemi wao unaosema
'kupenda si kazi,kazi kumpata anaye kupenda'
mi ninavyo ona hapo huyo mtu maarufu hakupendi,hivyo we sema tu na moyo wako uache kujipendekeza kwake,na kuhusu huyo mwingine ambae humpendi,'usiolewe na mtu
ambae humpendi kwani ndoa ni mkataba wa kudumu,'haya ni mawazo yangu tuu.
 
Hawezi kukuoa wewe sababu wewe ni cheap nadhan ndo maneno magumu ambayo inabidi uyakubali hlf uyafanyie kazi.... 1st day kakutongoza hlf kataka kukulala siku hiyo hiyo I wish ungeingia kwenye kichwa chake ujue alikuchukuliaje mpk akakufuata na approach hiyo ya kidharau kias icho au labda unaonekanaje? Safi ulimkataa sasa ulivyo mpuuzi friends wame kidanganya kichwa chako kwamba jamaa ni expensive go get him ni sawa kusema kwamba unampenda Najua wanawake hawajui wanachokipenda ila in short Najua mnapenda mwanaume expensive sasa unapataje kitu expensive while u ar cheap sasa hapo ndo hamjuagi mfanye nn na hasa tatizo lako ndo hilo nkushauri hv inabid ujue kua expensive na kutetea thamani yako full stop, mapenzi ni game tu una laki mfukoni unataka kumiliki benzi we kichaa?unamfutaje mtu aliye kuchukulia wewe kua ni demu wakutongozwa Leo na kugongwa Leo eti unadai thamani yako kwake! Hata nguo ya mtu ukitaka ipate kwa bei rhs njooo kidharau hv as if huna shida nayo uone unavyoipata kirahisi sasa toka na approach yako ya kipuuzi hivo hivo nenda mliman city ishushe thamani nguo uone km itakusaidia kupunguzwa bei..... Huu mwimbo na imba kila siku ht kwa dada zangu home acheni upuuzi jueni thamani zenu hizo hisia zenu bila akili mtagongwa mpk mkome na ndoa ng'oooo
Mkuu asante kwa mchango wako. Hayo ni maono yako na nnayahesimu. Ilaa, ucheap wangu uko wapi? Au labda ni kwa vile nilitafutiwa baadae na mtu wangu, dadangu? Coz mimi sikukumbuka hata kuchukua namba yake in the first place. Na hata nlipoipata sikuanza mimi kumtafuta. Je, ningemkubalia na kumpa shoo the same day aliyonitongoza ungeniitaje kwa mfano?
 
When communication is weak mhhhhhh.....haiwezekani MTU anayekupenda kwa dhati asikutafute hata kwa siku mara moja.......hata hivyo alishakuambia ana mtu huoni alitaka kamchezo tu??? Kwa status yake hakuna muoaji hapo...let him go for good
 
Baada ya dada yako kukushauri kuwa umpende ndo ilipita hiyo miezi nane kabla ya kumpa utamu au hiyo miezi nane ni kutokea kule mwanzo alivyokutongoza ukakataa?
Mkuu Behaviourist. Hii ni tokea mtongozo wa mwanzo kabisa, kule msibani.
 
mh...ndg waswahili wanausemi wao unaosema
'kupenda si kazi,kazi kumpata anaye kupenda'
mi ninavyo ona hapo huyo mtu maarufu hakupendi,hivyo we sema tu na moyo wako uache kujipendekeza kwake,na kuhusu huyo mwingine ambae humpendi,'usiolewe na mtu
ambae humpendi kwani ndoa ni mkataba wa kudumu,'haya ni mawazo yangu tuu.
Amina! Hili nalizingatia pia
 
Last Activity: Apr 13, 2016 at 4:10 PM
Joined: Monday
Messages: 2
Likes Received: 1
Trophy Points: 3
Gender: Female
Birthday: October 11
Hivi ulisema wewe ni msomaji mzuri wa JF?
Usikurupuke uonekane mjanja. Mtu anaweza kua msomaji mzuri ila hajajiunga. Imenchukua mwaka mzima mpaka kuamua kujiunga humu, huo ni mfano wangu. So muache dada wa watu na punguza ujuaji
 
Duh poleh sana mwaya
Asante mwaya. Haya ni majaribu ya shetani tu. Anahakikisha mtu hupati furaha... Ila, wazungu wana kausemi kao kanasemaa KARMA'S A BITCH. Sasa hivi huyo girlfriend wake yuko jela ana kesi isiyokuwa na dhamana. Mungu hachelewi kulipa.
 
Mkuu Behaviourist. Hii ni tokea mtongozo wa mwanzo kabisa, kule msibani.
Loooooooh!!!...... Baada ya kurudiana nae aliomba utamu baada ya mda gani?(i normally study behaviour of human beings so as to understand their mind-objectives and aims)
 
Habari wapendwa wa mmu,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote. Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanya biashara kwa hio kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani. Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend. Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi ktk pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao. Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaio nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tuu. Nimemtafuta sanaaa... jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei..

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa... huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu nnayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.

Pole for the everything... What I can say huyo si wako.. As hard as it is I'm sorry you have to let him Go... I can see you truly love him but he doesn't belong to you... Huyo jamaa knew your weaknesses and hana msimamo na sidhani kama alitaka kukuowa from the beginning... Just for you to track him because of your sister and friend it was the biggest mistake you did... Common now let a man to track you down first and ask you the first date and not you , beautiful... In the beggining you were not suppose to listen your sister or friend , ilitakiwa ujisikilize wewe na maamuzi yako na usimamie maamuzi yako ... Okay hayo yalishatokea tuyaache ... For now move on with your life how? Praying and fasting if you can , do your hobbies, go to the gym , work extra hours , volunteer ili tuu mawazo ya huyo celebrity yasiwepo... Delete all his contacts , block him everywhere .... So you dont get confusion ... About the new guy mama take it slow . if you can ask him to wait if he truly loves you , he will waiting for you ..... Nafikiri as you keep praying and fasting you will get a clear direction., Good luck.. Thanks..
 
Mitihani hii ya mahusiano kila mtu ana ya kwake. Mara nyingi kimya huwa kina mshindo mkuu, angalia asikupotezee muda wako, umri hausubiri mtu
 
Hawezi kukuoa wewe sababu wewe ni cheap nadhan ndo maneno magumu ambayo inabidi uyakubali hlf uyafanyie kazi.... 1st day kakutongoza hlf kataka kukulala siku hiyo hiyo I wish ungeingia kwenye kichwa chake ujue alikuchukuliaje mpk akakufuata na approach hiyo ya kidharau kias icho au labda unaonekanaje? Safi ulimkataa sasa ulivyo mpuuzi friends wame kidanganya kichwa chako kwamba jamaa ni expensive go get him ni sawa kusema kwamba unampenda Najua wanawake hawajui wanachokipenda ila in short Najua mnapenda mwanaume expensive sasa unapataje kitu expensive while u ar cheap sasa hapo ndo hamjuagi mfanye nn na hasa tatizo lako ndo hilo nkushauri hv inabid ujue kua expensive na kutetea thamani yako full stop, mapenzi ni game tu una laki mfukoni unataka kumiliki benzi we kichaa?unamfutaje mtu aliye kuchukulia wewe kua ni demu wakutongozwa Leo na kugongwa Leo eti unadai thamani yako kwake! Hata nguo ya mtu ukitaka ipate kwa bei rhs njooo kidharau hv as if huna shida nayo uone unavyoipata kirahisi sasa toka na approach yako ya kipuuzi hivo hivo nenda mliman city ishushe thamani nguo uone km itakusaidia kupunguzwa bei..... Huu mwimbo na imba kila siku ht kwa dada zangu home acheni upuuzi jueni thamani zenu hizo hisia zenu bila akili mtagongwa mpk mkome na ndoa ng'oooo
Akhsaaante saaana...
 
Sijui unataka akuambie vp,anakupa viashiria vyote kwamba hakutaki na hataki mawasiliano na wewe lakini wewe unaonekana kinganganizi.Mtu mwenye nia ya kukuoa na mwenye mapenzi ya dhati kweli atakwambia ana girlfriend?yaani red flags alishakupa tangia mwanzo lakini unazipuuza.Tatizo moyo ukipenda ngumu kuusemea.Huyo atakuja kukuumiza shost kuliko unavyotarajia,we achana nae kama kuna plan B anza nayo.
 
Back
Top Bottom