Ukifa, hutatamani tena kuishi duniani!

Ukifa, hutatamani tena kuishi duniani!

Bado haujaelewa mantiki ya swali langu naona.

Ninachotaka kufahamu ni uhakika gani ulio nao juu ya hiki ulicho kisema?

Kwa sababu umeongea ukiwa na uhakika sana, nahitaji tu kufahamu je una experience ya hiki ulicho sema?

Je una mtu yoyote labda aliyewahi kuwa marehemu then akawa hai akakudokeza haya?
Ninauhakika mkubwa sana kwani naona viumbe hai wakifa Kila kukicha na hawarudi tena.
 
Unaona wakifa kila kukicha ?

Una uhakika gani huwa hawarudi tena?

Unawezaje kujigawa duniani kote mpaka kuwa na uhakika wa kuwa huwa hawarudi tena?
Yeah, ninawaona Kila kukicha, miti inakatwa, wadudi wanakufa, wanyama wanakufa, nk.

Kwa mfano, mbwa wangu alikufa mwaka 2007 nikamzika, mwaka 2024 nilipafukua pale nilipomzika nikakuta mifupa yake, hii inadhihirisha kuwa tangu alipokufa bado hajarudi katika hali ya uhai.

Sina haja ya kuzinguka Dunia nzima wakati mabaki ya viumbe wanaokufa viko maeneo ninakoishi.
 
Tafsiri ya neno kifo kwako ni ipi?
 
Jibu langu ni sijui, sijui kama ukifa ndo mwisho wa kila kitu sababu kama binadamu ni nishati na nishati haiwezi haribika bali ina badili asili hivyo huenda kufa ndio sababu ya nishati kubadili asili na kuwa kitu kingine au huenda inaenda kwenye dimension nyingine
Pia sijui huenda kufa kweli ni mwisho wa kila kitu sababu hakuna ushahidi wa maisha baada ya kifo
 
Hebu nifundishe hiyo sayansi ya roho japo kidogo.
Jambo lolote usilolijua ni kama vile halipo. Hata sayansi ya kawaida kuna sehemu kubwa ya mambo hufanyika huku wanasayansi hawajawahi kuona wanachojihusisha nacho. Mfano wanasayansi wanajua sana kuhusu uwepo wa electrons ambazo hata kwa kutumia darubini hazionekani, lakini wanasayansi wanaweza ku-calculate speed ya electron na idadi yake katika atom fulani e.g. Helium atom, n.k.

Kumbe kutoonekana kwa kitu sio kutokuwepo kwake. Huu ndio msingi wa sayansi ya kiroho. Kutoka hapa unahitaji darasa ndefu kuweza kuona kuwa kuna uwepo wa roho na viumbe vya kiroho na tena utaelewa kuwa roho ndio uwepo msingi na halisi zaidi hata ya uwepo wa kimwili. Mwanadamu ni kiumbe mwenye akili na ufahamu (conciousness), je haya yalitoka wapi? Kwa kifupi kuna uwepo usioonekana na uwepo huu ndio uwepo wa kiroho na ndio unaofanya mengine yote yawezekane.
 
Kifo ni mwisho wa shughuli za kibayolojia za mwili (moyo kusimama, ubongo kuacha kufanya kazi).
Ila haisemi kama ndio mwisho wa ufahamu, na mwanadamu ni ufahamu pia hivyo huenda ufahamu ndio unao endelea kuishi
 
Jibu langu ni sijui, sijui kama ukifa ndo mwisho wa kila kitu sababu kama binadamu ni nishati na nishati haiwezi haribika bali ina badili asili hivyo huenda kufa ndio sababu ya nishati kubadili asili na kuwa kitu kingine au huenda inaenda kwenye dimension nyingine
Pia sijui huenda kufa kweli ni mwisho wa kila kitu sababu hakuna ushahidi wa maisha baada ya kifo
Ukifa umepotea mazima. Hakuna peponi wala mbinguni.
 
Back
Top Bottom