Njombe: Afisa Kilimo ahukumiwa Kwenda jela Miaka 5 au Faini ya Tsh. Laki 5 kwa kuomba na Kupokea Rushwa ya Elfu Kumi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Rashid Mustapha Makocha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 10,000 (Elfu Kumi)

Akisoma hukumu katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isaac Mlowe amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea #Rushwa na kosa la kumshawishi Mkulima ili aweze kumsajili kwenye Daftari la Wakulima ili awe mnufaika wa Mbolea ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali

Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini.

Chanzo: TAKUKURU
 
Mambo mengine ni ya kuchekesha kweli kwenye nchi hii!! Wakurugezi tunasikia wametumbuliwa kwa kuiba mamilion ya shilingi, lakini husikii kinachoendelea baada ya hapo, CAG Ameibua madudu mazito mabilioni ya shiling yametafunwa lakini htusikii hizo hela zikirudishwa serikalini, wala wahusika kuchukuliwa hatua, kama takukuru mpo kwa kutenda haki, tunatamani na haya mengine yakishugulikiwq!

Rai: mtumishi wa umma Tosheka na mshahara wako, jua kwamba mwajiri wako wa kwanza ni Mungu huyo ndiye boss wako, kutoridhirika na maisha yako na kutosheka na maish yako, kutawapeleka wengi motoni maana chochote unachokifanya unaweza kufikiri serikali haikuoni, hamna mtu anayekuona lakini Mungu muumba mbingu na nchi anakuona, ipo siku utakaposimama mbele zake wakati huo hapa duniani umeishakuwa maiti, hapo ndipo utakapotafuta japo sekunde moja ya kurudi duniani kurudisha pesa za watu ila utakuwa too late! Tuache wizi watumishi wa umma! Umeajiriwa na mshahara wa 500,000/= panga mambo yako vzr, muombe Mungu akupe hekima ya kutumia hiyo hela kwa furaha na kwa utoshelevu tuache kujidhadharisha kwa vifedha vidogovidogo vya aibu! Tukumbuke kuna watu waliokuwa na fedha walifanya walichokitaka lakini Leo duniani hawapo kama walikuwa ni wezi wa mali za umma! Niwahakikishie kuwa saiv wanachemka motoni ndugu zangu! Itakufaidia nini ukipata ulimwengu wote, ukipata magari yote, wanawake wote, pesa zote na mwisho wa siku ukaishia kwenda kuchemka motoni kama samaki??? Huwezi mficha Mungu uovu wako! Hawa ni watu wachache waliokuwa ni watumishi wa umma na wenye fedha zao Leo hii duniani hawapo, wingi wa mali zao haukuzuiq kifo na kama walikuwa wezi wa mali za umma Leo hii na dakii wanachemka kwenye moto huu hapo chini

1: Reginald mengi
2: benerd membe
3: Hayati John pombe magufuli
4: kijazi
5: mrema

Unaweza kuongezea na wengine unaowajua wewe!! :
 
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Rashid Mustapha Makocha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 10,000 (Elfu Kumi) Akisoma hukumu katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isaac Mlowe amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea #Rushwa na kosa la kumshawishi Mkulima ili aweze kumsajili kwenye Daftari la Wakulima ili awe mnufaika wa Mbolea ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini. Chanzo: TAKUKURU
 
kweli huo ulikua ni mtego na jamaa kajaa kizembe sana …

buku kwa milioni moja wakati wenzie wanapiga ma bilioni faini malaki tu ?
 
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Rashid Mustapha Makocha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 10,000 (Elfu Kumi)

Akisoma hukumu katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isaac Mlowe amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea #Rushwa na kosa la kumshawishi Mkulima ili aweze kumsajili kwenye Daftari la Wakulima ili awe mnufaika wa Mbolea ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali

Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini.

Chanzo: TAKUKURU
Hahahaha
TAKUKURU inahangaika na vifaranga huku ikiipitia mbali tipoti ya CAG.

Wanasubiri maagizo. Lakini hao madogo wanachukuliwa hatua kali kwa sababu wanafanya makosa madogo madogo
 
Rushwa ni adui wa haki na hata hiyo adhabu ni stahiki ila how come adhabu uwa zinawalenga watu wa chini tu,mijizi mikubwa inaachwa ikiendelea kudunda tu mitaani
 
Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini.

Chanzo: TAKUKURU
Hapa inaonyesha kuna hukumu ya kosa la kwanza na kosa la pili,
Je mshtakiwa sio kwamba anatakiwa kulipa milioni moja ( 1,000,000 ) au kwenda jela miaka 10 kwa hukumu zote mbili?

Naomba kueleweshwa.
 
Mambo mengine ni ya kuchekesha kweli kwenye nchi hii!! Wakurugezi tunasikia wametumbuliwa kwa kuiba mamilion ya shilingi, lakini husikii kinachoendelea baada ya hapo, CAG Ameibua madudu mazito mabilioni ya shiling yametafunwa lakini htusikii hizo hela zikirudishwa serikalini, wala wahusika kuchukuliwa hatua, kama takukuru mpo kwa kutenda haki, tunatamani na haya mengine yakishugulikiwq!

Rai: mtumishi wa umma Tosheka na mshahara wako, jua kwamba mwajiri wako wa kwanza ni Mungu huyo ndiye boss wako, kutoridhirika na maisha yako na kutosheka na maish yako, kutawapeleka wengi motoni maana chochote unachokifanya unaweza kufikiri serikali haikuoni, hamna mtu anayekuona lakini Mungu muumba mbingu na nchi anakuona, ipo siku utakaposimama mbele zake wakati huo hapa duniani umeishakuwa maiti, hapo ndipo utakapotafuta japo sekunde moja ya kurudi duniani kurudisha pesa za watu ila utakuwa too late! Tuache wizi watumishi wa umma! Umeajiriwa na mshahara wa 500,000/= panga mambo yako vzr, muombe Mungu akupe hekima ya kutumia hiyo hela kwa furaha na kwa utoshelevu tuache kujidhadharisha kwa vifedha vidogovidogo vya aibu! Tukumbuke kuna watu waliokuwa na fedha walifanya walichokitaka lakini Leo duniani hawapo kama walikuwa ni wezi wa mali za umma! Niwahakikishie kuwa saiv wanachemka motoni ndugu zangu! Itakufaidia nini ukipata ulimwengu wote, ukipata magari yote, wanawake wote, pesa zote na mwisho wa siku ukaishia kwenda kuchemka motoni kama samaki??? Huwezi mficha Mungu uovu wako! Hawa ni watu wachache waliokuwa ni watumishi wa umma na wenye fedha zao Leo hii duniani hawapo, wingi wa mali zao haukuzuiq kifo na kama walikuwa wezi wa mali za umma Leo hii na dakii wanachemka kwenye moto huu hapo chini

1: Reginald mengi
2: benerd membe
3: Hayati John pombe magufuli
4: kijazi
5: mrema

Unaweza kuongezea na wengine unaowajua wewe!! :
Kwanini uwataje Hawa? Kulikua na namna ukaandika bila kuwataja hawa.
 
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Rashid Mustapha Makocha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 10,000 (Elfu Kumi)

Akisoma hukumu katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, Isaac Mlowe amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea #Rushwa na kosa la kumshawishi Mkulima ili aweze kumsajili kwenye Daftari la Wakulima ili awe mnufaika wa Mbolea ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali

Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini.

Chanzo: TAKUKURU
Hapo TAKUKURU wamekula kama LAKI MOJA au MBILI.
 
saana yani.

acha aende na maji maana huo ni uzembe wa kiwango cha fly over.

mimi mwenyewe hata kwa mtego wa 100,000 huwezi kuninasa.

tena Afisa kabisa ?🙌
Mbinu hizi, mara nyingi zinatokana na ahadi.

Unamwambia mtu nipe kiasi fulani, anakujibu kwa wema tu, njoo kesho.

Halafu anaenda TAKUKURU anapewa hiyo pesa na wanaweka mtego.

Akikuletea hiyo pesa ukaipokea ndio kwisha.
 
Back
Top Bottom