JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu Amiry Luwiso na Ashirafu Awadh waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya kuongoza genge la uhalifu kwa njia ya mtandao na kujipatia zaidi ya Sh milioni 280 kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja baada ya kukiri mashtaka yanayowakabili.
Hukumu hiyo iitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo baada ya washtakiwa hao kutimiza masharti ya makubaliano ya kukiri kosa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Akiwasomea hukumu hiyo, Hakimu Mazengo alisema mahakama imetoa hukumu hiyo kwa kuzingatia kitendo cha washtakiwa hao kukiri mashtaka yao bila kuisumbua mahakamani na kwa kuzingatia makubaliano kati yao na DPP.
Chanzo: Habari Leo