Ruvuma: Ukikutwa unamiliki silaha kinyume cha Sheria Faini Milioni 10 au Jela miaka 15 au vyote

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linaendelea kuwakumbusha wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuendelea kutumia vizuri msamaha uliotolewa na Serikali ambapo atakaye salimisha kwa hiari hatachukuliwa hatua yeyote wala kuulizwa maswali. Silaha hizo ni pamoja na zile za wamiliki waliofariki ambazo ndugu zao bado wanazo majumbani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilya amesema msamaha wa kusalimisha silaha kwa hiari ulianza toka Septemba 1, 2023 na mwisho ni Oktoba 31, 2023. Hivyo hadi sasa zimebakia siku 07 za usalimishaji.

Endapo silaha hizo hazitasalimishwa katika muda wa msamaha uliotolewa na Serikali, Operesheni ya Nchi nzima itakapoanza wanaomiliki silaha hizo watakamatwa na kufikishwa mahakamani na wakipatikana na hatia kifungo chake ni Miaka 15 Jela au faini ya Shilingi Milioni 10 au vyote kwa pamoja.
0ef7a203-d1fe-4b31-933b-7fa444631d8a.jpeg

Amesema “Nichukue nafasi hii kuwataka wananchi wote ambao mpaka sasa hawajaweza kuzisalimisha silaha hizo watumie fulsa hii kuzisalimisha kwenye Vituo vya Polisi, Ofisi za Serikali za mitaa, kwa watendaji wa kata au Ofisi za vijiji zilizo karibu nao kabla ya muda wa msamaha huo kumalizika.

“Natoa rai kwa wale wote wanaotaka kujaribu kuingiza ng’ombe Mkoani Ruvuma kinyume na taratibu waache mara moja kwani Ruvuma sio salama kwao badala yake nawashauri wafate taratibu za kupata vibali kutoka katika mamlaka za Mikoa husika vitakavyo waruhusu kuingiza mifugo hiyo na kuweza kuonyeshwa maeneo sahihi ya kuendesha shughuli hizo za ufugaji.”
 
Back
Top Bottom