HIVI this kind of colonial-master behavior will ever come to an end.
Kwani ni lazima twende Uingereza. Hatuwezi kufanya jambo ambalo litawaonesha sisi hatuna shida nao hata kidogo.
Kwa mfano, kila Mtanzania akilenga kumpeleka mtoto wake kusoma Uchina, Uarabuni, India, Korea kusini, Japani, Malaysia, Australia, New Zealand jamaa wataendelea kutunyanyasa hivi kwa visa kweli?
Waingereza wanatufanyia dharau ya wazi kwa kuona sisi masikini, wenye shida, tunawahitaji wao. Na wao eti hawatuhitaji sisi. Ni ushuuuzi tu kwao!
Kama ndio hivyo tukae mkao wa Rwanda basi. Kwanza, tuamue kuwa lugha ya kufundishia sasa ni Kijapani na Kiarabu.
Lugha zinazofuatia ni Kihindi, Kichina, Kireno na Kihispania halafu Kiarabu.
Na lugha ya shughuli zote za kitaifa na kimataifa ikiwa kupata cheti cha chekechea hadi Chuo Kikuu ni Kiswahili au Kizaramo au Kinyamwezi au Kigogo au.....
TUONE MPAKA hapo kama ni wao waingereza watatuhitaji sisi au sisi ndio tutawahitaji wao!!!
HAPA wanataka kutuambia wenzao ni Kenya na sisi ni watumwa tu kwao!
Wafanya kama vile Microsoft walivyofanya kuwatumia Watanzania kuandaa software zake kwa Kiswahili na kisha kuzipa software hizo hadhi na heshima ya kwamba ni za Kenya na sio Tanzania. Upuuzi mtupu!!!