Ujumbe kwa Waislamu wenzangu

Ujumbe kwa Waislamu wenzangu

Ndio huyo huyo wa tanga nimekumbuka.

Sitaki kuzungumzia zaidi kuhusu huyu sheikh, jinsi anavyokufurisha waislamu wenzie na kujiona yeye na dhehebu lake wapo sahihi,Allah amuongoze. Nampenda na nakupendeni kwa ajili ya Allah ndugu zangu waislamu.
Heri ndugu Allah atuongoze sote
 
Hekima na usalafy wa kina mafuta na humeyd ni baina ya mashariki na magharibi.

Kuna yule mzee wa mombasa anaitwa abuu hashim fuatilia alipokuwa anamraddi salim barahiyan kuhusu kuramba tupu hukmu yake,kamkejeli sana salim barahiyan,abuu hashim ni mtu mzima lakini anakosa busara na ustaarabu.

Juzi juzi abdallah humeyd kamsema ndugu othman maalim kwamba ni mtu muongo kweli tena asema kwa dharau na kejeli,ilikuwa inatosha asemw kwamba kisa hiki hakikuthibiti lakini akaona haitoshi akamzulia mwenzie uongo,bila kujua pengine mwenzie hajafikiwa na hoja juu ya kisa cha musa kutaka kupewa funguo ya rizki.

Abdallah humeyd kwa vile ni salafi akamsema kwamba othman maalim ni mtu muongo bila hata aibu yoyote.

Abdallah humeyd anawavunjia heshima watu kistaarabu kwa sababu ya ongea yake ya taratibu lakini na yeye ni walewale tu.

Naomba mfikishieni salamu ndio maana kila siku masalafi wanakatana na mapande na kutahadharishana kwa sababu wamekosa hekima na busara na swabru katika ulinganizi.
Kila kitu ni lazima kiwekwe mahala pake. Na kila mtu ni lazima apewe haki yake bila ya kudhulumiwa.

Niishie hapo.
 
Assalam alaykum warahmatullahi wabarakatuh

TUFANYE NINI PINDI TUKIKUTA COMMENTS ZA KUMTUKANA ALLAH NA MTUME WAKE AU UISLAMU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII?

SHEIKH ABUL KHATWAAB ABDALLAH HUMEID حفظه الله

Naam naomba niwasilishe kile ambacho kidogo Allah alichonijaalia

Ujumbe huu mahsusi kwa watu wa mitandao.

kwenye Mitandao humu hutokea mijadala mingi inayohusu Kuuliza au kuelezea imani tofauti.

Ila sana mijadala hii huishia kwenye chuki kubwa baina ya watu ambao hata hawajuani.

Tahadhari ninayotoa kwa Ndugu zangu waislamu msipende kujadiliana na mtu ambae hataki kuelimishwa ambae amekuja kwa nia ya chuki kuhusu Uislamu wetu.

Allah anasema katika Qur'an yake

6:108.
Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.

Kulingana na Aya hio ni bora zaidi ukaachana na mijadala ambayo itapelekea Allah kutukanwa

Otterhound adriz FaizaFoxy
Tukiwatukana, tupigeni mawe tu hakuna namna
 
Unataka kuniambia kama maandamano hayajaruhusiwa katika uislamu hiyo maana yake ni kwamba ni halali muislamu aliyeandamana kuuliwa sio ?
Kwanza kuna aya gani au hadithi gani iliyoharamisha watu kuandamana?

Utawala wa Al-saud baada ya kuona watawala wa nchi mbalimbali za kiarabu wanatolewa madarakani kwa njia ya maandamano ndio wakawalazimisha masheikh wao kutoa fatwa za kuharamisha maandamano ili kuulinda utawala wa Alsaud kuendelea kubaki madarakani.
 
Tizama kwenye Qur'ani yoooteee kma utakuta walau aya kipande inayoruhusu maandamano pia hpo nyuma nilimpa mafundisho uyo mwenzako lkn akawa kichwa ngumu tizama post yngu ya nyuma huko nimeelezea
 
Idd el haji inaangukia siku ya Jumapili
Hivi hamuwezi kuisogeza iangukie siku ya kazi tupumzike?
 
Idd el haji inaangukia siku ya Jumapili
Hivi hamuwezi kuisogeza iangukie siku ya kazi tupumzike?
Uislamu unakwenda na muandamo wa mwezi kwaio sisi hatuna tarehe fixed ya sikukuu za kiislamu
 
Kwanza kuna aya gani au hadithi gani iliyoharamisha watu kuandamana?

Utawala wa Al-saud baada ya kuona watawala wa nchi mbalimbali za kiarabu wanatolewa madarakani kwa njia ya maandamano ndio wakawalazimisha masheikh wao kutoa fatwa za kuharamisha maandamano ili kuulinda utawala wa Alsaud kuendelea kubaki madarakani.
Hapa sio tu umesema kuwa huo uongozi wa Al Saudi ulikuwa unawatumia wanachuoni katika maslahi yao ya kisiasa.

Bali pia ulichokisema kina maana kuwa wanachuoni wetu wanaufanyia umma khiyana kwa kuificha haki, maana wanaharamisha yale aliyoyahalisha Allah.

Ni dhimma iliyoje!? sasa sijui unahakika kiasi gani na hiki unachokisema, maana maneno ni mazito haya.

Katika Quran Allah subhaanahu wataa'la anatuamrisha kuwatii viongozi, na mtume swalla llahu allaihi wasallam ametusisitiza hilo, na maulamaa wamejaalia hilo kuwa ni msingi katika misingi ya dini.

Na maandamano ni kinyume cha hivyo, sasa sijui ulikuwa unataka aya au hadithi ya aina gani ili kujua jambo hilo halifai.
 
Kwanza kuna aya gani au hadithi gani iliyoharamisha watu kuandamana?

Utawala wa Al-saud baada ya kuona watawala wa nchi mbalimbali za kiarabu wanatolewa madarakani kwa njia ya maandamano ndio wakawalazimisha masheikh wao kutoa fatwa za kuharamisha maandamano ili kuulinda utawala wa Alsaud kuendelea kubaki madarakani.
Hata Tanzania maandamano bila kibali ni haramu.
 
Tizama kwenye Qur'ani yoooteee kma utakuta walau aya kipande inayoruhusu maandamano pia hpo nyuma nilimpa mafundisho uyo mwenzako lkn akawa kichwa ngumu tizama post yngu ya nyuma huko nimeelezea
Tizama Qur'an yooooooooooote kama utakuta walau aya kipande inayoruhusu matumizi ya smartphone
 
Tizama Qur'an yooooooooooote kama utakuta walau aya kipande inayoruhusu matumizi ya smartphone
Upo sahihi....
JamiiForums-1494678070.jpg

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom