Kukamatwa kwa Sheikh Ponda na fursa ya kuwaunganisha Waislamu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
KUKAMATWA SHEIKH PONDA NA FURSA YA KUWAUNGANISHA WAISLAMU NA KUWAPAMBANUA NA KUWATENGANISHA WANAFIKI WASALITI NA WAZANDIKI

Dkt. Abdillah Sambalaa

Masomoni Uganda.

Niwape moyo ndugu zangu waislamu wa Tanzania wenzangu hasa wale wenye mrengo wa kuupenda uislamu wao katika nyanja zote katika siasa uchumi na kijamii na kuupenda uislamu kuwa na nguvu na wapendao kupinga dhulma unyanyasaji na ubaguzi na wenye kuupenda umoja na mshikamano wa WAISLAMU Tanzania na duniani kwa ujumla.

Najua sio waislamu wote wanaunga mkono katika hayo kwani wengi uislamu wao umeishia kuswali na kufunga na kwenda hija wao haiwashughulishi kuona waislamu kwanini wapo nyuma kiuchumi na kijamiii haiwashughulishi kuona kwanini waislamu wanabaguliwa katika elimu,ajira na utumishi uongozi na madaraka kwao sio jambo muhimu wapo waislamu wengi haiwashughulishi na kwa nini Mali za waislamu ikiwemo majumba ya waqfu ,viwanja hata mashamba ya waislamu yanauzwa kiholela na kuwafanya waislamu hawana cha kujivunia ni kama vile waislamu wamekuja Tanzania miaka ya 2000 wakakuta ardhi imejaa wakakosa kumiliki chochote.

Kwa kulijua hilo najua kuwa wapo waislamu wasioshughulishwa kabisa na kukamatwa sheikh PONDA na huenda wapo wanao ona ni sawa tu.Waislamu hawa sio wa kuwalaumu bali ni kuwaombea dua Allah awaoneshe haki kwani wengi wao hawana maarifa mazuri na hawajitambui lakini wengi wao pia wananufaika na mfumo huohuo unaolalamikiwa kumkamata Sheikh PONDA.

Hata Mimi mpaka nikiwa nasoma shahada ya pili chuo kikuu cha DSM nilikua bado sio mwelewa wa kuona na kuhoji kwanini nchi hii waislamu ni wengi sana kuliko jamii zingine lakini ni wachache sana kwenye kila fursa za serikali kuanzia kuchaguliwa kuendelea na masomo kuanzia sekondari hadi chuo kikuu pia kwenye ajira na uongozi katu sikuwahi kuwaza wala kujua ni kwanini.

Lakini pia nilikua nawaona wachochezi sana masheikh wanaopigia kelele ubaguzi na kutaka usawa baina ya watanzania katika fursa za serikali.

Nilikua karibu na baadhi ya masheikh wenye madaraka na waliokaribu sana na viongozi wa chama na serikali.

Masheikh wangu hawa walikua wanapenda kunikataza kuwasikiliza Sheikh Ilunga Kapunga, Sheikh Kundecha, Sheikh Ponda na wengine.

Hawakuwa wakiniambia sababu lakini walikua wakiniusia sana kuwa hawa watanipotosha.

Nikiwa nasoma UDOM Mara kadhaa sheikh Ilunga alipokuja kuongea na wanafunzi Mimi sikuhudhuria na nilikua napambana sana na wanafunzi wenzangu wanapoelezea mada walizosikiliza.

Wakati nakaribia kumaliza chuo UDOM yalianza malalamiko ya wasiokua waislamu kwamba UDOM Kuna udini sana waislamu watumishi na wanafunzi wamekua wengi sana kuliko kawaida. Lakini Mimi nilikua nawatafuta kwa tochi waislamu hao kwani walikua wachache mno lakini kwasababu nilikua sijitambui sikuona kama ile ilikua ni propaganda dhidi ya waislamu.

Nilipokua chuo kikuu UDSM nilipata bahati ya kukisoma kitabu maktaba ya chuo *MUSLIMS AND THE STATE IN TANZANIA* kilichoandikwa na Profesa Hamza Njozi, kitabu kile kilinianzishia safari mpya ya maisha yangu na kuipa thamani elimu yangu.

Niligundua kabla ya kusoma kitabu kile nikua MTU msomi mjinga na niliyepoteza muda mwingi kusoma bila kupata maarifa.

Niligundua kwamba wale masheikh wangu kwanini walikua wananikataza nisiwasikilize baadhi ya masheikh kumbe walikua wananikatia mawasiliano kunizuia kujifunza mambo ya uislamu kwa upana zaidi.

Kutoka katika kile kitabu nilikutana na masahibu mengi yaliyowakumba waislamu kutoka serikalini na ushahidi wake usio na shaka kwa madhira hayo.

Nilishangaa kuona mambo hayo hayasemwi japokua mengi yamekuwa ndiyo yakipiganiwa kwa muda mrefu na shura ya maimamu kwa kupazwa sauti na masheikh kama Sheikh Ponda, Sheikh Ilunga na wengine.

Kutoka katika kitabu kila *MUSLIMS AND THE STATE IN TANZANIA* nikapata hamasa na hamu ya kujifunza zaidi na kufanya utafiti zaidi ndipo nilipokuja kukutana na kitabu kingine Mimi nakiita ni *SAIKOLOJIA YA KUITAMBUA UHURU NA UKOMBOZI WA TANGANYIKA* Kitabu cha MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES (1924 - 1968) kilichoandikwa na Sheikh Mohamedi Saidi hapa sasa ndiyo nilijiona mjinga zaidi kwani mengi yaliyopo mule ni mambo ya kweli na halisi kinyume na mambo mengi tuliyofundishwa katika historia ambayo yalipotoshwa sana.

Uzuri wa kile kitabu kiliandikwa Mwalimu Nyerere akiwa hai na taarifa zisizo na shaka kwamba alikisoma na wapo watu walimshawishi akijibu na kukanusha yaliyomo mule ili kitabu kile kipoteze kukubalika, Mwalimu Nyerere inasemekana aliahidi kukijibu kwa kuwatumia wasaidizi wake waliosaidia sana kufanya historia ya TANZANIA ionekane hivi ilikua akirudi Uingereza kwenye matibabu ndiyo kijibiwe lakini MwenyeziMungu akakipa ulinzi kitabu hicho mpaka leo hakuna aliyethubutu kukijibu.

Kwasababu hizo ndiyo maana nasema wale waislamu wanaompinga Sheikh Ponda na kuungana na maadui wasioipenda shura ya maimamu hawa hawajitambui abadani kwakukosa elimu sahihi na maarifa stahiki juu ya Uislamu na maisha ya Waislamu katika siasa uchumi na kijamiii kwani hata mimi nilikua sijielewi kama wao mbali ya kuwa na shahada mbili za chuo kikuu.

Hivo msiwalaumu bali waelimisheni na waombeeni dua.

Napenda kuwapomgeza familia ya Sheikh Ponda kwa ujasiri wa kutotetereka kila inapotokea dhahama ya kumsumbua, kumtesa, kumkamata hata kujaribu kumuua Sheikh Ponda.

Kwa hakika familia hii ni mfano wa familia za kiswahaba zilizohimili misukosuko iliyotoka kwa makafiri waliokaribu kuizima nuru ya Uislamu wakati wa Mtume (s.a.w)

Nawapongeza Waislamu wa Tanzania wapigania haki na kuupenda uislamu wao kwa kupinga ubaguzi na dhulma za aina yoyote dhidi ya waislamu Tanzania.

Kukamatwa Sheikh Ponda ni fursa adhwiimu ya Waislamu kuungana na kuwa na mshikamano na umoja uliopotea kwa Waislamu leo, juhudi za kupigania kuachiwa Sheikh Ponda mara zote zimeleta tija kubwa kwa kuwaunganisha Waislamu na kuwa kitu kimoja. Haijalishi mko wengi kiasi gani au mnapingwa na wangapi bali kumbukeni mnachokipigania kinatamaniwa sana hata na wale wanaowapinga ila kutokujitambua kwao wamedhania kubaguliwa huko ndiyo majaliwa yao.

Mfano mzuri nimeona kwenye waraka sakata la kuhamishwa wahadhiri waandamizi UDOM au kusambaratishwa viongozi na wafanyakazi wa NSSF hata ikibidi shirika life lakini Waislamu wale viongozi lazima waondolewe kwa njia yoyote ile.

Hakuna mwenye akili timamu ambae anaweza kukubaliana na kilichofanyika katika haya au akashindwa kubaini kama huu ni uthibitisho mwingine wa kuwepo udini nchini Tanzania.

Mambo haya ni mazito sana hata waliotendewa pamoja na usomi wao wameogopa kusema wanalakamikia chini ya kapeti kwasababu ya kuogopa kinachoweza kuwapata.

Lakini waraka wa shura ya maimamu imeweka wazi na Sheikh Ponda amesema kwa kinywa kipana juu ya dhulma hizi na ni wazi hapa ndiyo penye mtima nyongo wa kukamatwa Sheikh Ponda.

Pongezi tunazitoa kwasababu ni kazi imefanyika na ujumbe umefika umewauma sana ndiyo maana wamemkamata.

Faida ya hili ni serikali kuufanyia kazi kwakujua kwamba kumbe maamuzi fulani yanatakiwa kuzingatiwa ili yasilete malalamiko baadae.

Si ajabu ikatokea kulikua na watu wachache wenye udini au chuki binafsi na watendaji wenzao wakawatengenezea zengwe na kuwashawishi viongozi kufanya maamuzi na viongozi huenda wamefanya maamuzi kwa nia njema kwakupokea ushauri wa watu wa chini kumbe ushauri ule umebeba ajenda za udini ili hali viongozi wa juu hawakujua hilo lakini lawama zote wanazibeba wao. Hivyo malalamiko haya yanasaidia kuongeza umakini kwa viongozi katika kufanya maamuzi.

Hongereni sana shura ya maimamu na Sheikh Ponda kuisaidia serikali katika kuboresha misingi ya kufanya maamuzi.

Nawaomba msivunjike moyo wala msiumie sana kukamatwa Sheikh Ponda kwani katika harakati za kudai haki na usawa hakuna kinachofanya ujumbe usikike na mvumo uvume kishindo kisikike mtetemo utetemeshe ni kukamatwa wapiganaji au kuuawa wapiganaji.

Hatujasahau kifungo cha miaka 27 kwa Mh. Hayati Mandela kilivyorahisisha kupatikana Uhuru kwa ndugu zetu Afrika ya Kusini na kukomesha ubaguzi wa rangi uliodhaniwa ni majaliwa ya Waafrika.

Sheikh Ponda kakutana na madhila makubwa sana kabla hata Mambo sasa hajajua kama atakua Polisi au atakuja kuwa kamanda wa kanda maalumu.

Sheikh Ponda amesha pigwa risasi ili auawe hadharani na mwisho kumuweka mahabusu ili afe kwa maumivu makali ya majeraha ya kupigwa risasi kwa kumuweka jela miaka mitatu mwisho sheikh ponda akashinda kesi zote na kupona kabisa akiwa jela na mwisho wa sinema askari aliyetumwa kumpiga risa Sheikh Ponda akajiua mwenyewe kwa kujipiga risasi kutokana kuona maruweruwe kila siku maishani kwa kitendo alichokifanya.

Hivyo hakuna kubwa wala hakuna jipya watakalo fanya dhidi ya sheikh zaidi watamfungulia kesi ya uchochezi ndiyo maana wanatishia kumficha kumcheleweshea dhamana lakini atatoka tu.

Kukamatwa Sheikh Ponda ni fursa ya Waislamu kuwabaini viongozi Waislamu ambao ni wanafiki na wasaliti wa harakati za waislamu na umoja wao.

Ni kawaida sana kila mwaka wa uchaguzi kutokea Masheikh wanaokuja kuwabadilikia Waislamu waliokuwa wanawahamasisha kuwaonesha dhulma na hata kuwashawishi kuandamana kupinga dhulma hizi lakini kila inapofikia madhila kwa Waislamu au uchaguzi mkuu hujitokeza Masheikh bila aibu kuwageuka waislamu na kuyageuka maneno yao na kuwa upande ule ule uliokuwa unalaumiwa kuwadhulumu na kuanza kuupamba na kuwapamba.

Hatujawasahau masheikh kama Sheikh Magezi, Dr sule, na wengine wengi.

Nipende tu kuwashauri Masheikh hawa kutambua kwamba WAISLAMU sio wajinga na uchaguzi ni kipindi kifupi tu lakini aibu yake itadumu milele na waislamu wanakufuta na kukusahau mara moja kama ilivyotokea kwa Sheikh Mbukuzi.

Ni vema masheikh wenye vinyongo na kutoridhika wakabakia kimya kama alivyofanya Sheikh Mohamedi Issa na wengine waliokaa kimya kusubiri mawimbi makubwa yapite ili wabakie salama.

Masheikh wanaoogopa michubuko na majeraha ya kupigania haki za waislamu wasikubali kutumika wakati huu ni rahisi kuonekana wanafiki na wasaliti kama Waislamu wa Tanzania wanavyomuona Sheikh Kundecha sasa, visa vyake vyote na misemo ya kuvutia na kuchekesha Waislamu hawana haja navyo, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kubwa wakati huu.

Ni vema wakabakia kufundisha darsa misikitini kwa visa vya ndoa na vile vya udhun bin unuk lakin sio tena vile walivyokua wanafundisha vilivyojenga hamasa na ujasiri kwa waumini visa kama vya kina Amar bin Yasiri, Sumaya, vita vya badri n.k, hata sasa wawaachie wengine.

Nimalizie kwa kuuliza wasomi wenzangu walimu wangu wasomi Waislamu huko Tanzania mpo wapi siwaoni katika sakata hili la kuutetea waraka ambao wengi mmepata ajira na vyeo kwa kuhofia kuonekana kuwabagua Waislamu.

Tunasoma maandiko ya ndugu zetu wasio Waislamu ikiwemo Profesa Alex, Dr Saguti Kisyesye, Profesa Mujuni Rwechungura, Askofu Mwamakula Mwanakondoo, Baba Askofu Bagonza na wengine wengi.

Kulikoni wenzangu? siwaoni, kila nimuulizae mnamsaidiaje Sheikh Ponda na kuutetea waraka huo kwa hoja kila mmoja anambia waulize mawakili.

Basi niwapongeze mawakili kwa kazi nzuri ya kufa na kupona hamumtetei Sheikh Ponda bali mnawatetea Waislamu na Uislamu Sheikh Ponda ni alama ya Waislamu wa Tanzania wanaopinga ubaguzi na dhulma na kutetea haki za Waislamu,hivyo tunawaombea msichoke wala msirudi nyuma MwenyeziMungu atawalipa kwa kazi yenu.

Watu wausome waraka/ muongozo wenye hoja waujibu waraka na sio kuhangaika na Sheikh Ponda.

SHEIKH PONDA AACHIWE HURU
 
Umekaa na kutafuta namna ya kutoka kimaisha umeona umefeli huu ndio ushuzi unakuja kuandika hapa ili upate sapoti ya magaidi wenzako....?!

Kwa taarifa yako radicalism ni ugonjwa wa akili na wewe umeashaanza kukupata. Usidhani utaishia hapo. Leo unasema waislam wanadhurumiwa kesho hata ukaachiwa hii inchi yote hii na wapuuzi wenzako mnaofanania akili na maoni na mawazo utadhani hata mnajua nini maana ya uislam na dini imetokea wapi.............. Mtaendeleza roho chafu ya chuki dhidi ya wengine tena wakufanana nao dini kabisa..... Kesho utasema waislam wa kigoma sio watu wazuri bali wazuri ni waislam wa tanga sababu ya tabia ile ile ya chuki, choyo, ubinafsi na roho mbaya dhidi ya wengine.........

Kuna watanzania kibao wanaishi huko vijijini hawana dini wala hawajui nini maana ya dini yoyote, hao nao wadai wana waraka wa kutoa kusema hawana nafasi katika shughuli za serikali.....

Omba sana MUNGU roho chafu ya kuchukia binadamu wengine ikutoke. Hapo hautetei maagizo ya MUNGU wala uislam, wewe ni hasidi na mfitini uliyejificha nyuma ya dini na roho yako chafu ya ahera inakuita ndio maana unaongea upuuzi kama huu umeandika hapa.

MUNGU akusaidie akili yako chafu isafishike ukae ukijua kuwa huwezi kubagua ukamaliza utanendelea hadi mwisho wako maisha na kizazi chako utakiachia misala ya ubaguzi.

Kabla haujajitambua kwa dini,taifa, kabla haujajitambua kwa kabila au kanda unayotokea kaa ukijua wewe ni mwanadamu kwanza kabla ya yote na baada ya hapo wewe ni mwafrika, halafu ni wa jinsia fulani, hayo mengine ni ya ziada......

Roho mbaya tu shenzi wahedi wewe.....
 
Hiki ndicho ulichoenda kusomea huko? Acha udini utakufa mapema sababu ya roho mbaya lini elimu ya Tanzania ikabagua mtu? Unataka upewe ajira usio na elimu nayo kisa dini? Hao wanao kaa kimya wanajielewa, acha kuwachonganisha watanzania.
 
*KUKAMATWA SHEIKH PONDA NA FURSA YA KUWAUNGANISHA WAISLAMU NA KUWAPAMBANUA NA KUWATENGANISHA WANAFIKI WASALITI NA WAZANDIKI*

Dr Abdillah Sambalaa

Masomoni Uganda.

Niwape moyo ndugu zangu waislamu wa Tanzania wenzangu hasa wale wenye mrengo wa kuupenda uislamu wao katika nyanja zote katika siasa uchumi na kijamii na kuupenda uislamu kuwa na nguvu na wapendao kupinga dhulma unyanyasaji na ubaguzi na wenye kuupenda umoja na mshikamano wa WAISLAMU Tanzania na duniani kwa ujumla.

Najua sio waislamu wote wanaunga mkono katika hayo kwani wengi uislamu wao umeishia kuswali na kufunga na kwenda hija wao haiwashughulishi kuona waislamu kwanini wapo nyuma kiuchumi na kijamiii haiwashughulishi kuona kwanini waislamu wanabaguliwa katika elimu,ajira na utumishi uongozi na madaraka kwao sio jambo muhimu wapo waislamu wengi haiwashughulishi na kwa nini Mali za waislamu ikiwemo majumba ya waqfu ,viwanja hata mashamba ya waislamu yanauzwa kiholela na kuwafanya waislamu hawana cha kujivunia ni kama vile waislamu wamekuja Tanzania miaka ya 2000 wakakuta ardhi imejaa wakakosa kumiliki chochote.

Kwa kulijua hilo najua kuwa wapo waislamu wasioshughulishwa kabisa na kukamatwa sheikh PONDA na huenda wapo wanao ona ni sawa tu.Waislamu hawa sio wa kuwalaumu bali ni kuwaombea dua Allah awaoneshe haki kwani wengi wao hawana maarifa mazuri na hawajitambui lakini wengi wao pia wananufaika na mfumo huohuo unaolalamikiwa kumkamata Sheikh PONDA.

Hata Mimi mpaka nikiwa nasoma shahada ya pili chuo kikuu cha DSM nilikua bado sio mwelewa wa kuona na kuhoji kwanini nchi hii waislamu ni wengi sana kuliko jamii zingine lakini ni wachache sana kwenye kila fursa za serikali kuanzia kuchaguliwa kuendelea na masomo kuanzia sekondari hadi chuo kikuu pia kwenye ajira na uongozi katu sikuwahi kuwaza wala kujua ni kwanini.

Lakini pia nilikua nawaona wachochezi sana masheikh wanaopigia kelele ubaguzi na kutaka usawa baina ya watanzania katika fursa za serikali.

Nilikua karibu na baadhi ya masheikh wenye madaraka na waliokaribu sana na viongozi wa chama na serikali.

Masheikh wangu hawa walikua wanapenda kunikataza kuwasikiliza Sheikh Ilunga Kapunga, Sheikh Kundecha, Sheikh Ponda na wengine.

Hawakuwa wakiniambia sababu lakini walikua wakiniusia sana kuwa hawa watanipotosha.

Nikiwa nasoma UDOM Mara kadhaa sheikh Ilunga alipokuja kuongea na wanafunzi Mimi sikuhudhuria na nilikua napambana sana na wanafunzi wenzangu wanapoelezea mada walizosikiliza.

Wakati nakaribia kumaliza chuo UDOM yalianza malalamiko ya wasiokua waislamu kwamba UDOM Kuna udini sana waislamu watumishi na wanafunzi wamekua wengi sana kuliko kawaida. Lakini Mimi nilikua nawatafuta kwa tochi waislamu hao kwani walikua wachache mno lakini kwasababu nilikua sijitambui sikuona kama ile ilikua ni propaganda dhidi ya waislamu.

Nilipokua chuo kikuu UDSM nilipata bahati ya kukisoma kitabu maktaba ya chuo *MUSLIMS AND THE STATE IN TANZANIA* kilichoandikwa na Profesa Hamza Njozi, kitabu kile kilinianzishia safari mpya ya maisha yangu na kuipa thamani elimu yangu.

Niligundua kabla ya kusoma kitabu kile nikua MTU msomi mjinga na niliyepoteza muda mwingi kusoma bila kupata maarifa.

Niligundua kwamba wale masheikh wangu kwanini walikua wananikataza nisiwasikilize baadhi ya masheikh kumbe walikua wananikatia mawasiliano kunizuia kujifunza mambo ya uislamu kwa upana zaidi.

Kutoka katika kile kitabu nilikutana na masahibu mengi yaliyowakumba waislamu kutoka serikalini na ushahidi wake usio na shaka kwa madhira hayo.

Nilishangaa kuona mambo hayo hayasemwi japokua mengi yamekuwa ndiyo yakipiganiwa kwa muda mrefu na shura ya maimamu kwa kupazwa sauti na masheikh kama Sheikh Ponda, Sheikh Ilunga na wengine.

Kutoka katika kitabu kila *MUSLIMS AND THE STATE IN TANZANIA* nikapata hamasa na hamu ya kujifunza zaidi na kufanya utafiti zaidi ndipo nilipokuja kukutana na kitabu kingine Mimi nakiita ni *SAIKOLOJIA YA KUITAMBUA UHURU NA UKOMBOZI WA TANGANYIKA* Kitabu cha
*MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES (1924 - 1968)*
kilichoandikwa na Sheikh Mohamedi Saidi hapa sasa ndiyo nilijiona mjinga zaidi kwani mengi yaliyopo mule ni mambo ya kweli na halisi kinyume na mambo mengi tuliyofundishwa katika historia ambayo yalipotoshwa sana.

Uzuri wa kile kitabu kiliandikwa Mwalimu Nyerere akiwa hai na taarifa zisizo na shaka kwamba alikisoma na wapo watu walimshawishi akijibu na kukanusha yaliyomo mule ili kitabu kile kipoteze kukubalika, Mwalimu Nyerere inasemekana aliahidi kukijibu kwa kuwatumia wasaidizi wake waliosaidia sana kufanya historia ya TANZANIA ionekane hivi ilikua akirudi Uingereza kwenye matibabu ndiyo kijibiwe lakini MwenyeziMungu akakipa ulinzi kitabu hicho mpaka leo hakuna aliyethubutu kukijibu.

Kwasababu hizo ndiyo maana nasema wale waislamu wanaompinga Sheikh Ponda na kuungana na maadui wasioipenda shura ya maimamu hawa hawajitambui abadani kwakukosa elimu sahihi na maarifa stahiki juu ya Uislamu na maisha ya Waislamu katika siasa uchumi na kijamiii kwani hata mimi nilikua sijielewi kama wao mbali ya kuwa na shahada mbili za chuo kikuu.
Hivo msiwalaumu bali waelimisheni na waombeeni dua.

Napenda kuwapomgeza familia ya Sheikh Ponda kwa ujasiri wa kutotetereka kila inapotokea dhahama ya kumsumbua, kumtesa, kumkamata hata kujaribu kumuua Sheikh Ponda.

Kwa hakika familia hii ni mfano wa familia za kiswahaba zilizohimili misukosuko iliyotoka kwa makafiri waliokaribu kuizima nuru ya Uislamu wakati wa Mtume (s.a.w)

Nawapongeza Waislamu wa Tanzania wapigania haki na kuupenda uislamu wao kwa kupinga ubaguzi na dhulma za aina yoyote dhidi ya waislamu Tanzania.

Kukamatwa Sheikh Ponda ni fursa adhwiimu ya Waislamu kuungana na kuwa na mshikamano na umoja uliopotea kwa Waislamu leo, juhudi za kupigania kuachiwa Sheikh Ponda mara zote zimeleta tija kubwa kwa kuwaunganisha Waislamu na kuwa kitu kimoja. Haijalishi mko wengi kiasi gani au mnapingwa na wangapi bali kumbukeni mnachokipigania kinatamaniwa sana hata na wale wanaowapinga ila kutokujitambua kwao wamedhania kubaguliwa huko ndiyo majaliwa yao.

Mfano mzuri nimeona kwenye waraka sakata la kuhamishwa wahadhiri waandamizi UDOM au kusambaratishwa viongozi na wafanyakazi wa NSSF hata ikibidi shirika life lakini Waislamu wale viongozi lazima waondolewe kwa njia yoyote ile.

Hakuna mwenye akili timamu ambae anaweza kukubaliana na kilichofanyika katika haya au akashindwa kubaini kama huu ni uthibitisho mwingine wa kuwepo udini nchini Tanzania.

Mambo haya ni mazito sana hata waliotendewa pamoja na usomi wao wameogopa kusema wanalakamikia chini ya kapeti kwasababu ya kuogopa kinachoweza kuwapata.

Lakini waraka wa shura ya maimamu imeweka wazi na Sheikh Ponda amesema kwa kinywa kipana juu ya dhulma hizi na ni wazi hapa ndiyo penye mtima nyongo wa kukamatwa Sheikh Ponda.

Pongezi tunazitoa kwasababu ni kazi imefanyika na ujumbe umefika umewauma sana ndiyo maana wamemkamata.

Faida ya hili ni serikali kuufanyia kazi kwakujua kwamba kumbe maamuzi fulani yanatakiwa kuzingatiwa ili yasilete malalamiko baadae.

Si ajabu ikatokea kulikua na watu wachache wenye udini au chuki binafsi na watendaji wenzao wakawatengenezea zengwe na kuwashawishi viongozi kufanya maamuzi na viongozi huenda wamefanya maamuzi kwa nia njema kwakupokea ushauri wa watu wa chini kumbe ushauri ule umebeba ajenda za udini ili hali viongozi wa juu hawakujua hilo lakini lawama zote wanazibeba wao. Hivyo malalamiko haya yanasaidia kuongeza umakini kwa viongozi katika kufanya maamuzi.

Hongereni sana shura ya maimamu na Sheikh Ponda kuisaidia serikali katika kuboresha misingi ya kufanya maamuzi.

Nawaomba msivunjike moyo wala msiumie sana kukamatwa Sheikh Ponda kwani katika harakati za kudai haki na usawa hakuna kinachofanya ujumbe usikike na mvumo uvume kishindo kisikike mtetemo utetemeshe ni kukamatwa wapiganaji au kuuawa wapiganaji.

Hatujasahau kifungo cha miaka 27 kwa Mh. Hayati Mandela kilivyorahisisha kupatikana Uhuru kwa ndugu zetu Afrika ya Kusini na kukomesha ubaguzi wa rangi uliodhaniwa ni majaliwa ya Waafrika.

Sheikh Ponda kakutana na madhila makubwa sana kabla hata Mambo sasa hajajua kama atakua Polisi au atakuja kuwa kamanda wa kanda maalumu.

Sheikh Ponda amesha pigwa risasi ili auawe hadharani na mwisho kumuweka mahabusu ili afe kwa maumivu makali ya majeraha ya kupigwa risasi kwa kumuweka jela miaka mitatu mwisho sheikh ponda akashinda kesi zote na kupona kabisa akiwa jela na mwisho wa sinema askari aliyetumwa kumpiga risa Sheikh Ponda akajiua mwenyewe kwa kujipiga risasi kutokana kuona maruweruwe kila siku maishani kwa kitendo alichokifanya.

Hivyo hakuna kubwa wala hakuna jipya watakalo fanya dhidi ya sheikh zaidi watamfungulia kesi ya uchochezi ndiyo maana wanatishia kumficha kumcheleweshea dhamana lakini atatoka tu.

Kukamatwa Sheikh Ponda ni fursa ya Waislamu kuwabaini viongozi Waislamu ambao ni wanafiki na wasaliti wa harakati za waislamu na umoja wao.

Ni kawaida sana kila mwaka wa uchaguzi kutokea Masheikh wanaokuja kuwabadilikia Waislamu waliokuwa wanawahamasisha kuwaonesha dhulma na hata kuwashawishi kuandamana kupinga dhulma hizi lakini kila inapofikia madhila kwa Waislamu au uchaguzi mkuu hujitokeza Masheikh bila aibu kuwageuka waislamu na kuyageuka maneno yao na kuwa upande ule ule uliokuwa unalaumiwa kuwadhulumu na kuanza kuupamba na kuwapamba.

Hatujawasahau masheikh kama Sheikh Magezi, Dr sule, na wengine wengi.

Nipende tu kuwashauri Masheikh hawa kutambua kwamba WAISLAMU sio wajinga na uchaguzi ni kipindi kifupi tu lakini aibu yake itadumu milele na waislamu wanakufuta na kukusahau mara moja kama ilivyotokea kwa Sheikh Mbukuzi.

Ni vema masheikh wenye vinyongo na kutoridhika wakabakia kimya kama alivyofanya Sheikh Mohamedi Issa na wengine waliokaa kimya kusubiri mawimbi makubwa yapite ili wabakie salama.

Masheikh wanaoogopa michubuko na majeraha ya kupigania haki za waislamu wasikubali kutumika wakati huu ni rahisi kuonekana wanafiki na wasaliti kama Waislamu wa Tanzania wanavyomuona Sheikh Kundecha sasa, visa vyake vyote na misemo ya kuvutia na kuchekesha Waislamu hawana haja navyo, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kubwa wakati huu.

Ni vema wakabakia kufundisha darsa misikitini kwa visa vya ndoa na vile vya udhun bin unuk lakin sio tena vile walivyokua wanafundisha vilivyojenga hamasa na ujasiri kwa waumini visa kama vya kina Amar bin Yasiri, Sumaya, vita vya badri n.k, hata sasa wawaachie wengine.

Nimalizie kwa kuuliza wasomi wenzangu walimu wangu wasomi Waislamu huko Tanzania mpo wapi siwaoni katika sakata hili la kuutetea waraka ambao wengi mmepata ajira na vyeo kwa kuhofia kuonekana kuwabagua Waislamu.

Tunasoma maandiko ya ndugu zetu wasio Waislamu ikiwemo Profesa Alex, Dr Saguti Kisyesye, Profesa Mujuni Rwechungura, Askofu Mwamakula Mwanakondoo, Baba Askofu Bagonza na wengine wengi.

Kulikoni wenzangu? siwaoni, kila nimuulizae mnamsaidiaje Sheikh Ponda na kuutetea waraka huo kwa hoja kila mmoja anambia waulize mawakili.

Basi niwapongeze mawakili kwa kazi nzuri ya kufa na kupona hamumtetei Sheikh Ponda bali mnawatetea Waislamu na Uislamu Sheikh Ponda ni alama ya Waislamu wa Tanzania wanaopinga ubaguzi na dhulma na kutetea haki za Waislamu,hivyo tunawaombea msichoke wala msirudi nyuma MwenyeziMungu atawalipa kwa kazi yenu.

Watu wausome waraka/ muongozo wenye hoja waujibu waraka na sio kuhangaika na Sheikh Ponda.

*SHEIKH PONDA AACHIWE HURU*
We we waislam huwa hawaeleweki . China inatesa sana waislamu umewahi kusikia waislam wa huku wakipiga kelele za kulaani ?
 
Dini hizi zinatumika vibaya kwenye hizi shithole countries.
 
Hiki ndicho ulichoenda kusomea huko? Acha udini utakufa mapema sababu ya roho mbaya lini elimu ya Tanzania ikabagua mtu? Unataka upewe ajira usio na elimu nayo kisa dini? Hao wanao kaa kimya wanajielewa, acha kuwachonganisha watanzania.
Anataka kutuaminisha kuwa serikali inakataza watoto wanotoka familia za dini ya kiislamu kupata elimu na ajira...... Mimi mwenyewe sio mwislam halafu sipo kwenye ajira ya serikali napambana kivyangu, sikuwahi kupewa mkopo serikalini miaka yote nasoma, nimejilipia kila kitu mwenyewe na nimesoma enzi za kikwete ambaye ni mwislamu........ kwahiyo niseme waislamu walinibania kupata haki zangu za kiraia.......... Kuwa nina baguliwa sababu ya dini yangu..... Fala sana huyu mleta uzi......
 
Yaani kuna watu wengine hata wasome vipi huwaelimiki hata chembe anachokifanya ni kufunika vitabu na kutoka yeye mwenyewe huku elimu kaiacha darasani, badala ya kuhimiza watoto wasome kwa bidii kazi yao kuwalisha matango pori
 
Kabisa. Yeye anahisi dini ni kubishana na mashindano yasiyo na tija. Sasa hapo ukimkagua utakuta ana matatizo ya kisaikolojia sio mzima.
 
Hongera sana mleta mada, huu uzi wako ni ukweli mtupu
Waislamu Majority wanakubaliana na uliyoandika na wako na Sheikh Ponda

Achana na hawa ambao wanakukejeli, wanakutukana, hii ni kwa sababu wapo katika mfumo wa dhulma, wananufaika na mfumo huu kwa sababu unawapendelea na kuwakandamiza waislamu.

Kwa hiyo, matusi, Kejeli, na vijembe vyao ni mbinu tu ya kuwawakatisha tamaa msidai haki yenu.

Mfumo unawabeba na kuwanufaisha wao zaidi!

Waislamu wako kimya lakini wanafuatilia hali ya nchi yao very closely
 
Anataka kutuaminisha kuwa serikali inakataza watoto wanotoka familia za dini ya kiislamu kupata elimu na ajira...... Mimi mwenyewe sio mwislam halafu sipo kwenye ajira ya serikali napambana kivyangu, sikuwahi kupewa mkopo serikalini miaka yote nasoma, nimejilipia kila kitu mwenyewe na nimesoma enzi za kikwete ambaye ni mwislamu........ kwahiyo niseme waislamu walinibania kupata haki zangu za kiraia.......... Kuwa nina baguliwa sababu ya dini yangu..... Fala sana huyu mleta uzi......
Matusi ya nini jomba!Jibuni hoja zake!Mimi pia nimkristo lakini pia kuna mazingira serikali inapaswa kuyaepuka katika kuonesha kundi fulani limetengwa haswa kenye udini na ukabila.
 
Najua sio waislamu wote wanaunga mkono katika hayo kwani wengi uislamu wao umeishia kuswali na kufunga na kwenda hija wao haiwashughulishi kuona waislamu kwanini wapo nyuma kiuchumi na kijamiii haiwashughulishi kuona kwanini waislamu wanabaguliwa katika elimu,ajira na utumishi uongozi na madaraka kwao sio jambo muhimu wapo waislamu wengi haiwashughulishi na kwa nini Mali za waislamu ikiwemo majumba ya waqfu ,viwanja hata mashamba ya waislamu yanauzwa kiholela na kuwafanya waislamu hawana cha kujivunia ni kama vile waislamu wamekuja Tanzania miaka ya 2000 wakakuta ardhi imejaa wakakosa kumiliki chochote.
Mmeendekeza sana elimu ya dini kuliko elimu ya duniani, ukikuta mtoto wa muislam mfia dini lazima elimu ya dunia atakuwa anaperform vibaya.
Kuwa nyuma kiuchumi sijui kamaanisha nini wakati matajiri wakubwa ni almost wote waislam tanzania hii, ila hawa wa huku kitaa mfumo wa maisha yao unawafanya wawe maskini, wengi wao wanaoa wanawake halafu wanawafungia ndani, hawawahusishi na biashara kazi kupiga umbeya mitaani. (Nadhani pia ni matokeo ya elimu) sasa utata unakuja mume akifa mwanamke hajui aanzie wapi wakati alizoea kila kitu kinaletwa.
Kunabaadhi ya vitu inabidi mbadilike
 
Story ndeeefu!
Hoja imefifishwa na longolongo.

Bado una safari ndefu ya kufuta ujinga.
Possible umesoma ili uutumie usomi kijinga.
 
Back
Top Bottom