Ujue Mti chonganishi

Huu ni uongo mtupu, mjomba wangu ameipanda na sasa wanazeeka bila tatizo
Yale maingiliano ya dunia ya kiroho na dunia isiyoonekana huthibitishwa na matokeo yake na si mchakato unaoonekana Kwa wale ndugu zangu wanaotaka ithibati za kisayansi naomba watulie wasome kimyakimya tuu.

Kuna huu mti unaopendwa kupandwa kuzunguka nyumba zetu, ni mti mzuri wenye kivuli kizuri, hujulikana kama mti mwamvuli na matawi yake huota kwa mpangilio maalum
Ni mti wenye mizizi mirefu yenye nguvu ya ajabu kiroho katika ulimwengu uonekanoa Mizizi yake yenye nguvu huweza kupenya kwenye msingi wa nyumba na kusababisha ufa au nyufa na kuleta uharibifu mkubwa kwenye jengo lako.

Nyufa husika zisipodhibitiwa mapema huweza hata kusababisha nyumba kubomoka au hata kuanguka.. Nyufa hizi zina madhara ya moja kwa moja kiroho nyufa hizi huleta nyufa kwenye familia, mikosi na hata vifo wakati mizizi ikileta nyufa kwenye nyumba jengo, nguvu yake huleta nyufa katika familia.

Nyufa ndani ya familia husababisha mshikamano uliopo kukatika vipande vipande, watu kukosa ajira, biashara kuanguka, watoto kufeli masomo na vifo hasa vya wazazi
Sio mzi mzuri wa kupanda nyumbani na wengi sasa wanaukata Kama unao nyumbani kwako hebu linganisha na hiki nilichoandika hapa.
14b6c812d3da7967172acd3db2c429bf.jpg
 
Mkuu mshana Jr..VIP kuhusiana na huu kama una taarifa zake
 

Attachments

  • PHOTO_20190922_134458.jpg
    PHOTO_20190922_134458.jpg
    215.9 KB · Views: 27
  • PHOTO_20190922_134402.jpg
    PHOTO_20190922_134402.jpg
    247.4 KB · Views: 26
  • PHOTO_20190922_134449.jpg
    PHOTO_20190922_134449.jpg
    177.9 KB · Views: 27
Tanzania Forestry Research Institute, walithibitisha kuwa huo mti hauna madhara yoyote, bali ni imani tu za watu. Mti una faida nyingi sana huo.
 
Nina mwezi sasa korodani zinauma kweli. nafikiri itakuwa huu mti, naukata kesho. Shxzx type
 
Tanzania Forestry Research Institute, walithibitisha kuwa huo mti hauna madhara yoyote, bali ni imani tu za watu. Mti una faida nyingi sana huo.
Hao ni watu wa mazingira... Mambo ya kiroho watayajuaje?
 
Mkuu ulikata mti wako kimakosa. Sio huo unaozungumziwa. Kwanza huo mti matawi yake hayaoti kwa interval. Pili una matunda madogodogo yanayoliwa na binadamu. Hauitwi panga uzazi bali muharadali. Ingekuta leo hii una kivuli cha uhakika.

Jr
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom