Hizi shuhuda zimenitisha mno
Mtani yule aunt yangu alikuwa na huo mti kwake, mti umekuwa mkubwa sana sana,
Siku hiyo binti yake wa miaka 8 ametoka shule, gari imemleta hadi gatin, mama mzazi yupo, baba mzazi yupo, bibi mzaa mama yupo na mjakazi pia yupo.
Mtoto kaingia ndani kama ilivyo kwa watoto atatupa beg sebuleni sweta koridoni, soksi huko viatu huko.
Kidogo mama anaingia ndani anashauti wewe mtoto weka nguo vizuri.
Mama kaondoka kidogo kwenda town wengine walibaki.
Kidogo mjakazi anaingia ndani anaita baba baba njoo muone huyu anapenda michezo ya hatari.
Baba anaingia ndani kukuta mtoto kaingia chumba cha bafu yaani pana room ya kuanika vinguo vyao vya ndani palikuwa na kakamba ka manila, yaani ile manila wameigiwa mara 3 hivyo kamba imefungwa ili waanike vinguo vyao vya ndani.
Mtoto kasimama juu ya kapu la kuweka nguo chafu kajinyonga, na kafa.
Mtaa mzima pamoja na wafiwa walitoa ile miti.
Hata kuni zake hakuna aliyetumia.
Continue Rest in Paradise mjukuu.