Adui Mdogo Lakini Hatari: Utitiri wa Kuku (Poultry Mites)

Adui Mdogo Lakini Hatari: Utitiri wa Kuku (Poultry Mites)

Brayan_Jk

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2025
Posts
210
Reaction score
249
Hawa wadudu wadogo sana wansumbua na kuwananyonya damu ya kuku wako . Wanaficha kwenye nyufa za mbao na sehemu zisizo na mwanga , ila usiku ndio wanashambulia. Wanaongezeka haraka zaidi kwenye mazingira yenye joto na unyevunyevu, na huenea kupitia nyumba uchafu wa mda mrefu wa kutosafisha banda au vifaa vilivyotumika na wanyama au ndege wa porini wenye utitiri

Madhara yake ni makubwa:

Kuku hukosa utulivu, kujipiga, manyoya kuanguka na mayai kupungua

Mashambulizi makali husababisha upungufu wa damu (kucha na kilemba chake kuwa nyeupe), udhaifu na hata vifo

Na Si kuku pekee balinutitiri ukiingia nyumbani kwako utakuchosha kwa huleta muwasho, vipele na harara kwenye ngozi.


Jinsi ya kuzuia na kutibu:

Safisha na disinfect mara kwa mara nyumba za kuku

Wape kuku “dust bath” ya mchanga/majivu kujisafisha.

Safisha na Pulizia dawa za kuuwa utititiri kwa Kuku mmoja mmoja kisha nyunyizia mafuta asilia ( inapobidi)

Weka karantini kwa kuku wapya kabla ya kuwaunganisha na wengine.
 
Back
Top Bottom