Ujue Mti chonganishi

Ujue Mti chonganishi

Mshana Jr....ungefunguka kidogo kama unayo historia ya mti huu...!

Je....? Ni moja ya miti ya kupandikizwa maabara kisha ikatengenezwa Mbegu.

Ama ni moja ya miti ya kale yenye historia ya kujitosheleza...?
 
We mganga umenifanya nifikiri sana juu ya huu mti..mana nikiikumbuka family ya anko wangu kabla na baada ya kuupanda huu mti..sichelewi kusema huu mti una mabalaa..hebu tueleze na miti mingine yenye shida kama huu tuitambue mapema..
 
Yale maingiliano ya dunia ya kiroho na dunia isiyoonekana huthibitishwa na matokeo yake na si mchakato unaoonekana Kwa wale ndugu zangu wanaotaka ithibati za kisayansi naomba watulie wasome kimyakimya tuu.

Kuna huu mti unaopendwa kupandwa kuzunguka nyumba zetu, ni mti mzuri wenye kivuli kizuri, hujulikana kama mti mwamvuli na matawi yake huota kwa mpangilio maalum
Ni mti wenye mizizi mirefu yenye nguvu ya ajabu kiroho katika ulimwengu uonekanoa Mizizi yake yenye nguvu huweza kupenya kwenye msingi wa nyumba na kusababisha ufa au nyufa na kuleta uharibifu mkubwa kwenye jengo lako.

Nyufa husika zisipodhibitiwa mapema huweza hata kusababisha nyumba kubomoka au hata kuanguka.. Nyufa hizi zina madhara ya moja kwa moja kiroho nyufa hizi huleta nyufa kwenye familia, mikosi na hata vifo wakati mizizi ikileta nyufa kwenye nyumba jengo, nguvu yake huleta nyufa katika familia.

Nyufa ndani ya familia husababisha mshikamano uliopo kukatika vipande vipande, watu kukosa ajira, biashara kuanguka, watoto kufeli masomo na vifo hasa vya wazazi
Sio mzi mzuri wa kupanda nyumbani na wengi sasa wanaukata Kama unao nyumbani kwako hebu linganisha na hiki nilichoandika hapa.
14b6c812d3da7967172acd3db2c429bf.jpg
Ningependa kujua kuhusu muashoki
 
Mshana Jr....kuna aina nyingine ya Miti ni kweli inatoa Matunda ila sio ya kuliwa na Wanaadamu...!!

Vipi kwa Miti ya aina hii...?
The best panda ambayo matunda yake ni edible
 
Huu mti ninao nyumbani, niliupanda kama alama enzi nanunua kiwanja. Nina mwaka mmoja sasa kila nikifikiria kuukata, najikuta kubadili mawazo!
 
Yale maingiliano ya dunia ya kiroho na dunia isiyoonekana huthibitishwa na matokeo yake na si mchakato unaoonekana Kwa wale ndugu zangu wanaotaka ithibati za kisayansi naomba watulie wasome kimyakimya tuu.

Kuna huu mti unaopendwa kupandwa kuzunguka nyumba zetu, ni mti mzuri wenye kivuli kizuri, hujulikana kama mti mwamvuli na matawi yake huota kwa mpangilio maalum
Ni mti wenye mizizi mirefu yenye nguvu ya ajabu kiroho katika ulimwengu uonekanoa Mizizi yake yenye nguvu huweza kupenya kwenye msingi wa nyumba na kusababisha ufa au nyufa na kuleta uharibifu mkubwa kwenye jengo lako.

Nyufa husika zisipodhibitiwa mapema huweza hata kusababisha nyumba kubomoka au hata kuanguka.. Nyufa hizi zina madhara ya moja kwa moja kiroho nyufa hizi huleta nyufa kwenye familia, mikosi na hata vifo wakati mizizi ikileta nyufa kwenye nyumba jengo, nguvu yake huleta nyufa katika familia.

Nyufa ndani ya familia husababisha mshikamano uliopo kukatika vipande vipande, watu kukosa ajira, biashara kuanguka, watoto kufeli masomo na vifo hasa vya wazazi
Sio mzi mzuri wa kupanda nyumbani na wengi sasa wanaukata Kama unao nyumbani kwako hebu linganisha na hiki nilichoandika hapa.
14b6c812d3da7967172acd3db2c429bf.jpg
Hizi stori Zipo Africa tu
 
Back
Top Bottom