FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,212
Hakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mpaka kutusi.

Haya yanayoendelea si maoni tena bali ni uvunjifu wa amani uliokusudiwa. Uhuru wa maoni ni lazima uwe na mipaka.

Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi. Na cha kushangaza sana waziri wa habari amekaa kimya. Waziri wa sheria amekaa kimya. Waziri wa mambo ya ndani amekaa kimya, waziri wa ulinzi amekaa kimya.

Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.

Siioni tofauti yao na msiba wa taifa wa wakati wa mwenda zake.

Mpaka sisi tuliozowea mitandao ya kijamii tunawashangaa moderators wapo kimya, watu wanaporusha matusi na kejeli mpaka kwa Rais na mawaziri wake. Hivi hatuyaoni? Au tunapenda huu uchokozi uendelee mpaka uzae madhara?

Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.

Mimi nadhani wale wote wanaodai nchi imeuzwa waende mahakamani au kwa wao kupeleka madai au serikali iwaite mahakamani waje kuonesha nchi imeuzwa wapi na kwa lipi zaidi?

Nahisi kuna watu wapo nyuma ya pazia amabao wanadhani labda yataishia kiwepesi wepesi yakiachiwa yaendelee. Sasa hivi tayari chuki za wazi zinajionesha kati ya Wasio EWaisslam na Waislam, wasio Waarabu na Waarabu, Wabara na Wazanzibari. watu wa pwani na wasio wa pwani.

Hivi hayo yote kweli yamesababishwa na makubaliano ya Dubai na Tanzania yaliyopitishwa bungeni au kuna yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo hatuyaelewi?

Tunaionmba serikali ichukuwe hatua za dhati, kila anaerusha au kuongea chuki akajieleze kwa ushahi wa hayo ayasemayo, kama hana ushahidi aseme ukweli ni na nani yupo nyuma yake anaemlipa au kumchochea kufanya hivyo.

Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.

Naamini katika uwazi na ukweli na naamini katika uhuru wa maoni na habari, lakini kila uhuru ni lazima uwe na mipaka yake. Naona au Tanzania hatuna mipaka ya kujielezza maoni yetu aukama tunayo ama hatuijuwi au tunaiwachiie makusudi mipaka inavukwa?

Serikali, hususa Waziri wa habari, Nape Nnauye tueleze tupo bado ndani ya mipaka ya sheria au tumekiuka? Kama bado upo ndani ya mipaka ya sheria za uhuru wa maoni, tunaomba shertia zikafanyiwe ukarabati. Ili tuwe nchi yenhe kuheshimu utowaji mapni yetu uwe wa kuheshimiana.

Wewe kama hupendi nilichosema au kufanya mimi nifahamisheni usinitukane.

Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.
 
Kila mtu ana jambo lake ki maslahi, likiguswa atalalamika...
Jambo la DP World lina maslahi pande tofauti. Kila upande usikilizwe.
Hakuna kuona hawa ni hawa, wale ni wale...
Hilo ni sawa kabisa, lakini si linatakiwa lijadiliwe kiamani, kila mwenye hoja aiseme hoja yake bila jazba wala uchochezi au kuomesha chuki kwa wengine?

Au wewe unaridhika na lugha za uchokozi (provoking) zinazowachiwa kutumika hivi sasa?
 
Toka uanze mjadala wa DP world, umekuwa na makosa mengi ya kiuandishi.

Mfano Uzi huu una makosa zaidi ya 10, na wewe ilikuwa kinara wa kuwarekebisha watu wanaokosea.

Kuhusu DP world sina cha kuongeza wala kuongeza, mtavyokubaliana ndio hivyo hivyo
 
Mtoto anapo lilia wembe sawa acha umkate je atakae kosa usingizi ni nani? na kupoteza muda na gharama za matibabu . Ignorance and laziness to handle uncertainty the end result will be uncertainty inherent which is a disaster
 
Sipati picha kama ungekuwa mod jf ingekuwaje maana hayo unayoita 'maafa' mods wenyewe hawajayaona na ndio maana hawafuti nyuzi hizo.

Nijuavyo mie mods hufuta nyuzi zote zenye kuleta maafa muda mfupi tu baada ya kusambazwa
Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.
 
Ukishakuwa mtumwa... Lazime utumikie mabosi wako wanaokufanya ule... Wanasiasa wengi hapa Africa ni watumwa, hawapo kufanya siasa kwa manufaa ya wafrika
Sawa kabisa, kila mmoja wetu ana maoni yake, na ni vizuri kwenye maoni tusijumuishe, uweke huyo mwana siasa na alichokifanya ambacho wewe hukioni sawa, ndiyo nguvu ya hoja.

lakini kutukana na kuchochea kwa lugha za maudhi kunajenga au kunabomoa?
 
Back
Top Bottom