Sio upuuzi mkuu... *SURIYA* Anauliza hayo maswali kwa lengo la kufahamu chanzo kilicho pelekea huyo ndugu kupata HAEMORRHOIDSAcha upuuzi bwana we msaidie namna ya kupona,umri amekutajia kazi yake we ya nini?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni dawa gani alitumia mkuu?Bawasiri sio lazima ufanyie operation kuna ndugu yangu ilimsumbua sana lakini alipopata tiba ya asili hadi sasa ana mwaka wa nne haijamrudia tena zipo dawa za asili bila operation.
Mkuu je kwa bawasiri ya ndani inayotoka wakati wa kujisaidia na kurudi yenyewe baadaye (daraja la pili), mafuta hayo yaweza saidia pia?Mkuu! Achana na hao wanaotaka pesa zako ili upone... mimi nakupa tiba ya bure kabisa sitaki hata mia yako kwa sababu mimi pia nilipatwa na ugonjwa huu na nikapata tiba humu mitandaoni sijalipia hata mia zaidi ya bando tuuu... Nenda duka la madawa ya asili popote unapopataka mimi sina duka... ukanunue mafuta ya Nyonyo(Castrol oil) uwe unapakaza hapo kwenye shida kila siku wakati unataka kulala mpaka iondoke yenyewe... mimi nimepona kabisa kwa tiba hiyo na haijachukua hata wiki...
Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nami nitest hii kitu. Shukran mkuu kwa somoNilipona na nikamponesha mtu wangu wa karibu.
Nilitwanga alovera nilichanganya katika maji sikumbuki yalikuwa kiasi gani kwani nilikuwa najifanyia majaribio mwenyewe kabla sijaenda hospital nilikunywa ndani
ya week moja asubuhi grass moja kisha najipaka ute wa alovera katika bawasiri na jioni hivyo hivyo.Bawasiri ilitoweka nikampa mtu wangu wa karibu ajitibu kwa njia hiyo akapona.
Ila mchana nilikuwa nakunywa grass moja ya mwarobaini
Grass ndogo ya maji ya kunywa.
Jaribu nawe Wenda ukapona.
hii kitu ni kweli inatesa sana, Dawa nilizoshuhudia watu wa karibu wametumia na kupona ni mbili, lakini naamini kuna dawa nyingi za kuponesha huo ugonjwa.dawa yake ni ipi, je mtu akifanyiwa upasuaji inachukua siku ngapi kupona?
Mkuu ulikuwa unafanya mazoezi gani hasa?Mimi iliwahi nitokea kwa wiki 2 hivi kiasi kwamba nikaanza kuogopa maana kuna jamaa yangu ilimsumbua sana .
Nikawa nakunywa maji sana na kufanya mazoezi ikayeyuka
Sent using Jamii Forums mobile app
tumia utomvu wa ndizi kupakaza eneo lenye tatizo siku 5-7 utakua umemaliza tatizoHabari wakuu,
Nimekuwa nikinywa sana maji, kula mboga za majani na matunda. Naomba kama mtu ambaye alishawahi kuumwa bawasiri/hemorrhoids na akapona kabisa, anijuze alifanya nini akapona.
Ahsanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani, je kwa bawasiri ya ndani, dawa yake ni ipi mkuu?hii kitu ni kweli inatesa sana, Dawa nilizoshuhudia watu wa karibu wametumia na kupona ni mbili, lakini naamini kuna dawa nyingi za kuponesha huo ugonjwa.
Dawa hizo ni :
* Mafuta ya nazi kama ni kinyama kilichoota kwa nje na huwa kinauma sana. (paka kila siku asubuhi na jioni)
* Mafuta ya Nyonyo (castor oil) haya nayo paka asubuhi na jioni. utapona kabisa.
Note: mimi sio daktari nimeshauri tu kwa kuona watu wa karibu yangu wakipona.
Ahsante.
Habari, naomba na mimi namba ya huyo mtu na mimi nimtafute ni mhanga piaUkihitaji nitakupa mawasiliano yatakazokuwezesha kumpata.
Dasi desi naomba namba ya huyo mtu kama ulifanikiwa kuipata maana na mimi mhanga inanikosesha amani sana hiyo kitunipe tafadhali
Habari naomba uni PM namba za huyo mtu mwenye dawa pleaseMkuu tatizo lako linatibika kwa uhakika kabisa.
Kuna babu mmoja yuko anatibu tatizo hilo kwa miti shamba na amewatibu wengi sana ila yuko kanda ya ziwa (Simiyu). Na hivi hata mwezi haujaisha amemtibu mtu na amepona, yeye sio mganga wa kienyeji ila sema tu anajua dawa mbali mbali za magonjwa na hasa tatizo la bawasiri (mang'ondi) ndio limemfanya akawa kama mganga maana wengi wamekuwa wakipona kwake na huwa anasema kwa tatizo hilo hakuna haja ya kuhangaika kumeza au kupaka kemikali za hospitali maana kwake ni tatizo dogo sana.
Kikwao ugonjwa huo wanaita Mang'ondi.
Kuna bawasiri ile inayotokea kwenye njia ya haja kubwa na ile inayotokea kwa sehemu za siri kwa wanawake.
Kama utakuwa na uwezo wa kufika kwake nina uhakika tatizo hilo litakuwa historia kwako kama Mungu ikimpendeza.