Ugomvi mkubwa wa Mirathi. Familia ya Mandela yaanza kuuza mali za marehemu. Kweli Africa tunafanana Tabia

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau.

Ugomvi mkubwa wa mirathi ya marehemu Nelson Mandela umefikia pabaya. Baada ya baadhi ya wanafamilia kuanza kuuza mali za Marehemu.

Watoto na Wajukuu wa mandela wameingia kwenye ugomvi mkubwa wa kugombania mali za babu yao marehemu Mandela.

Africa tunafanana tabia. Kwenye swala la mirathi ugomvi lazima utokee

1705945510460.png

1705945098440.png
 
Attachments

  • Screenshot_20240122-182313_Firefox.jpg
    Screenshot_20240122-182313_Firefox.jpg
    199 KB · Views: 5
  • 1705945468105.png
    1705945468105.png
    95.2 KB · Views: 4
Habari wadau.

Ugomvi mkubwa wa mirathi ya marehemu Nelson Mandela umefikia pabaya. Baada ya baadhi ya wanafamilia kuanza kuuza mali za Marehemu.

Watoto na Wajukuu wa mandela wameingia kwenye ugomvi mkubwa wa kugombania mali za babu yao marehemu Mandela.

Africa tunafanana tabia. Kwenye swala la mirathi ugomvi lazima utokee
Ni kweli tunafanana maana hasili yetu ni moja.
Ila swala la kuwa na ugomvi kwenye mirathi ktk familia nyingi za kiafrica ni sababu ya athari za miingiliano ya tamaduni za mashariki ya kati (kwenye jamii zilizotawaliwa na waisilam) na tamaduni za magharibi(jamii zilizotaliwa na wazungu)

Uwepo wa mchanganyiko wa tamaduni unaleta shida sana kwenye swala la mirathi baina ya wale wanaoshikilia msimamonwa mila na tamaduni na wale wanaoshikilia ukisasa..
Tulifanya makosa sana kuacha asili zetu na kupokea asili za watu wengine tukiamini ndio usasa kumbe tulikuwa tunajiangamiza..
 
Habari wadau.

Ugomvi mkubwa wa mirathi ya marehemu Nelson Mandela umefikia pabaya. Baada ya baadhi ya wanafamilia kuanza kuuza mali za Marehemu.

mke wa zamani Winnie Mndela ,Watoto na Wajukuu wa mandela wameingia kwenye ugomvi mkubwa wa kugombania mali za babu yao marehemu Mandela.

Africa tunafanana tabia. Kwenye swala la mirathi ugomvi lazima utokee

View attachment 2879805

View attachment 2879793
nadhani hapo kwenye winnie mandela urekebishe maana alifariki 2018 kama sijakosea.
 
Habari wadau.

Ugomvi mkubwa wa mirathi ya marehemu Nelson Mandela umefikia pabaya. Baada ya baadhi ya wanafamilia kuanza kuuza mali za Marehemu.

mke wa zamani Winnie Mndela ,Watoto na Wajukuu wa mandela wameingia kwenye ugomvi mkubwa wa kugombania mali za babu yao marehemu Mandela.

Africa tunafanana tabia. Kwenye swala la mirathi ugomvi lazima utokee

View attachment 2879805

View attachment 2879793
Ndugu, mke wa zamani uliyemtaja naye ni marehemu, anagombea vipi hizo mali?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mke ni mmoja na watoto ni wale walio ndani ya ndoa. (2) andaa mtoto atafute vyake na sio kurithi vyako. (3) unda board ya kuendesha shughuli zako baada yako. Na mjumbe wa kila board atoke taasisi tofauti zinazoaminika huku dunian. Mfano capuchin brothers nk. Hii ni kama ipo hela mingi. Watoto wako wawe sehem ya wajumbe japo maamuz yaamuliwe na kikao. Watoto watatibiwa wakiumwa na kila mwaka watakuwa wanapewa gar jipya na mwisho wa mwez kuna hela flan wataingiziwa. Watasoma chochote wanachotaka na wajukuu.Warithi halisi wa mali zako ni kizazi cha nne blood line. Kila asilimia 10 ya mapato yako ni mali ya Mungu. Watasomesha na kusaidia masikin na ukitoa huo msaada uwajulishe kwa barua kuwa Mungu wa mbingun na Bwana wetu Yesu Kristo amekutuma kuwasaidia. Kwenye barua usiandike jina lako wala anuani zako ila wape risiti ya malipo uliyofanya. Wasikujue. Watoto wangu wasipewe mali zaid ya matumiz yao kwa anasa. Wakitaka zaid watafute zao. Mtoto wangu daima namfundisha ni lazima wafanye kaz kwa bidii na kwa malengo ili kutimiza wajibu na sio kwenda kula bata. Ole wake atakaemdhulumu mtu au ndugu. Na ole wake atakaekuwa mchawi. Na wanangu lazima wawe wakristo. Na ole wake atakaepigania mali kuwazid wenzie. Mwisho kama nikijaliwa na andaa eneo kubwa. Na kujenga hapo kituo kikubwa ambacho kitakuwa ni eneo vijana na watoto watakuwa wanakutana kumuimbia na kumuomba Mungu na kufundishwa desturi na utamaduni wetu kila wiki end jion. Na Kristo anataka nini kutoka kwetu. Eneo litaitwa hema ya kukutania. Nitalikabidhi kwa taasisi za kikristo ninazoziamin na nitaandika siku wakija kwenda kinyume na kuoanisha ukiukaji wa misingi ya ukristo walikabidhi kwa familia yangu itakayokuwepo nyakati hizo nayo ukikuta ilishakiuka pageuzwe makao ya watoto yatima na masikin katika Kristo. . Haya ni mawazo yangu nikijaaliwa. Eneo nishanunua la kutosha namuomba Mungu anisaidie nitimize haya nami niweke alama kabla cku zangu hazijakamilika. Kauli mbiu yangu siku zote "MPE MUNGU HAKI YAKE".
 
Ngozi nyeusi hatari.
sio ngozi nyeusi tu!! ata wazungu!!!,unafikiri kwa nini wazungu walimuua gadafi?{mafuta],sadam[mafuta],kwa nini congo haipati amani{madini},kwa nini walitawala afrika{mali ghafi],kwa nini wanapiga vita bomba la mafuta kutoka uganda kuja tz{wivu},kwa nini wanatengeneza virusi{ili wauze kinga}.....so acheni akili mgando!!
 
Mali zinatafutwa ili kujenga utajiri sio kutumika kutatua shida na njaa zisizo na mashiko.

Kimsingi wazazi wanapofanikiwa kupata mali wanatakiwa kuwa na successional plan ambayo itaelekeza mtoto gani ambaye anaonekana ana uwezo wa kusimamia mali vema zikasimama.

Wazazi wanapofanikiwa kupata mali then wageuze familia kuwa kampuni na zile mali kuwa assets za hiyo kampuni. Kuanzia hapo ni mwendo wa kuzingatia utendaji na sio kubembelezana au kusema huyu sijui mtoto wa kwanza sijui wa mwisho, hiyo hapana.

Cha kuzingatia ni weledi na uwezo mzuri wa watoto katika kumultiply mali na kuongeza utajiri wa familia. Unaweka mtoto miaka 3 ya usimamizi unampa mamlaka yote yeye atajua direction. Then unamtazama sasa anajiongeza vipi katika kupambana na haya maisha.

Bidii ikiwa vema then matunda yanaonekana na atatanua utajiri nakuwapa wenzake pia nafasi ya umiliki na usimamizi.

Kuna mzee watoto wake ni wa nne kila mtoto alimuuliza anataka kampuni gani, kila mtoto akasema aina ya biashara anataka kufanya, mzee wake akamfungulia kila mtoto biashara yake ili aanze jifunza ukuzaji wa mtaji. Watoto wake kwa sasa kila m'moja anajitegemea na wapo vema kwakweli maisha yamewakalia vema, mzee alifariki 2012 ila watoto wake hadi leo hawajayumba na wametengamaa wanashirikiana vema sana.
 
Hlii iwe ni funzo kwetu wapambanaji wote,,

Utajibana maisha na kutafuta pesa kwa jasho na damu ili uwatengenezee watoto maisha ya baadae.

Lakini watoto watauza mali zote ulizoziacha bila kujali.

Nadhani sasa mi wakati wa kujitafakari na kula mali zako mwenyewe ukiwa hai..
 
Habari wadau.

Ugomvi mkubwa wa mirathi ya marehemu Nelson Mandela umefikia pabaya. Baada ya baadhi ya wanafamilia kuanza kuuza mali za Marehemu.

Watoto na Wajukuu wa mandela wameingia kwenye ugomvi mkubwa wa kugombania mali za babu yao marehemu Mandela.

Africa tunafanana tabia. Kwenye swala la mirathi ugomvi lazima utokee

View attachment 2879805

View attachment 2879793
Mboni watoto wa Ruge wamepewa mabillion yao wametulia zao tu, ukiona hivyo familia imejaa masikini wengi masikini ndio wanaogombea Mali hukuti matajiri wakigombea Mali
 
Back
Top Bottom