Baadhi ya ndugu wauza nyumba ya familia Kariakoo iliyokuwa na waqfu. Mapanga yatembea nje nje

MELEKAHE

JF-Expert Member
Nov 19, 2023
665
2,829
Nimeona video inatrend ya ugomvi mkubwa wa nyumba ya urithi Kariakoo mtaa wa Manyema.

Nyumba hiyo ya ghorofa 5 ilijengwa na mzee anaeitwa Mohammed Alidina ambae alifariki miaka kazaa iliyopita.

Mzee huyo wakati akiwa hai alitoa sehemu ya nyumba hiyo. Floor ya juu itumike kama madrassa na kufanya taratibu za kukabidhi kwa msikiti ambazo waislamu wanaziita waqfu. Ghorofa zilizobaki aliendelea kuzitumia kuishi na zingine kupangisha appartments na fremu kwa wafanyabiashara Kariakoo.

Baada ya huyo mzee kufariki aliacha watoto 11, ambao watoto wao waligawana hizo appartments na fremu na kuendelea na maisha.

Mbeleni watoto wachache wa kiume wa marehemu mzee huyo wakapendekeza wazo la kutaka nyumba hiyo iuzwe kila mtu akajenge kwake. watoto wengine wakapinga kwamba hawataki nyumba iuzwe maana baba yao enzi za uhai alisema nyumba isiuzwe na akatoa sehemu ya nyumba iwe madrassa inayomilikiwa na waislamu wote. sasa watauzaje nyumba yenye wakfu ambayo ni mali ya waislamu wote.

Watoto wenye wazo la kuuza wakaona hapa kuuza ngumu. wakaamua kwenda kumshirikisha imamu wa msikiti ambao ulipewa wakfu sehemu ya nyumba hiyo. maana msikiti ulikuwa na documents za wakfu walizopewa na marehemu baba yao.

Kimya kimya wakashirikiana na imamu wa msikiti uliopewa hizo documents. wakatafuta mteja Mkinga mmoja wakamuuzia nyumba bila watoto wengine kujua.

Mbeleni mkinga huyo ambae ni mnunuzi aliyonunua hiyo nyumba akaenda kuchukua mali yake. Ndipo watoto wengine wakagundua nyumba imeuzwa. Ndipo ugomvi mkubwa ukaibuka na mapanga juu. 
Halafu mbona wameachiwa mali tu, frem unapokea kodi na bado nyumba nzuri hiyo kila mmoja ana sehemu yake tamaa za nini?

Huyo Sheikh ndio kaniacha hoi, unashiriki kuuza nyumba ya ibada?
Nipo Kariakoo, anaesimamia hiyo nyumba ni dd yao. Ishu ni kua anawapiga ndugu zake. Mfano frem ni 1,000,000 anawaambia wenzake kodi ni 600,000. Hiyo ndo shida
 
Billie Holiday alituasa tutafute kila mtu chake.
One for Billie Holiday.


View: https://youtu.be/mp349H8G0XQ?si=ivrD0_0Z8k7__zA8

God Bless the Child

Billie Holiday


Mama may have, papa may have
But God bless the child that's got his own

Them that's got shall get
Them that's not shall lose
So the bible said and it still is news
Mama may have, papa may have (mama may have, papa may have)
But God bless the child that's got his own, that's got his own (ooh-ooh)


Yes, the strong get smart
While the weak ones fade
Empty pockets don't ever make the grade (ooh)
Mama may have, papa may have (ooh, ooh)
But God bless the child that's got his own, that's got his own (ooh, ooh)


Money, you've got lots of friends
They're crowding around the door
When you're gone and spending ends
They don't come no more
Rich relations give crusts of bread and such
You can help yourself, but don't take too much
Mama may have, papa may have (mama may have, papa may have)
But God bless the child that's got his own, that's got his own
God bless the child, the child that's got his own

Source: Musixmatch
Songwriters: Billie Holiday / Alexis Latrobe / Arthur Jr. Herzog
God Bless the Child lyrics © Edward B Marks Music Company, Marks Edward B. Music Corp.
 
Guys hebu tutofautishe dini na mambo mengine.
Kwanini bado baadhi ya watu bado wanahodhi maisha ya watu kwa kigezo cha kua ni dini fulani.

Na hii sasa inapelekea baadhi ya watu wakiona jina la kiislam/kigalatia wanatuhumu waislam/wagalatia wote.
 
Back
Top Bottom