Kubota ndani ya miez6 ulikuwa na jumla ya kuku630ulikuwa unauza100kila mwezi? Eneo lako linatoshaje idadi hiyo?
 
Pole miguu kukosa nguvu kama sio wagonjwa ni kukosa calcium uwawekee mifupa kwenye chakula chao ila kama serious vitamoin inawasaidia nguvu.
Naombeni msaada wenu, nina vifaranga vya kuku chotara ambavyo vina umri wa wiki 7.
Tatizo ni kwamba miguu yao inakosa nguvu, wanashndwa kutembea.
Nilimpeleka mmoja kwenye duka la dawa za mifugu, wakamchunguza na kunipatia dawa ya vitamin kwa kuwa walinieleza kuwa miili yao imeshndwa kutengeneza vitamin B plus.
Tatizo bado linaendelea japokuwa nilianza kuwapatiwa vitamin hao vifaranga wote. Nasubiri ushauri wenu wanajamvi.
 
Kubota ndani ya miez6 ulikuwa na jumla ya kuku630ulikuwa unauza100kila mwezi? Eneo lako linatoshaje idadi hiyo?
Mkuu Ibra6 unaporejea maneno yangu ni vema u-quote post yangu maana sikumbuki kama nimewahi simulia kitu hiki ulichoandika, kuku 630? Miezi sita? Nashindwa kukujibu maana naona hainihusu.
 
Mimi nimekushauri mifupa, lakini pia angalia chakula chako ubora wake ukoje, angalia signs zingine je hawana ugonjwa wowote? wiki ya saba hawahitaji vitamin unless wanaumwa ninavyojua ni chakula kiwe kamili
Mama joe asante kwa ushauri wako, mifupa uwa nawawekea, nitaenda kuwanunulia vitamin uliyonishauri
 
naona kafanya mental calculation kupitia maelezo yako au ya GAZETI... kwa kweli ni ngumu kujua idadi kamili ila tu afuate maelezo ili kuweza kufikisha malengo yake.
Mkuu Ibra6 unaporejea maneno yangu ni vema u-quote post yangu maana sikumbuki kama nimewahi simulia kitu hiki ulichoandika, kuku 630? Miezi sita? Nashindwa kukujibu maana naona hainihusu.
 
Namshukuru Mungu na ushauri wenu ni kweli tukikazana tutaweza tu, changamoto kubwa ni magonjwa ya ghafla kutokea ila nashukuru yaani kila likija hili unakuta mwingine hapa kesha leta na ufumbuzi umejadiliiwa yaani imenisaidia sana sikuwa na Dr yoyote wa mifugo zaidi ya kupata ushauri hapa, kwa RETI na kwenye phamarcy. Sikutaka kuchukua mkopo nilitaka niende taratibu kwa kujibana tu na kupunguza matumizi yasiyo lazima. Naomba nikutie moyo mama Timmy kuku chotara hawana tofauti na hawa kienyeji kwa kulisha na dawa, mimi nimefuga wale wa kisasa ndio nimehamia kwa hawa, ukuaji wa hawa chotara ni wa haraka wakati hawahitaji gharama kubwa kihivyo maana hawali chakula kingi kama wakisasa wala hawahitaji vitamin isipokuwa wiki chache 2 za mwanzo. Kwavile wanakua haraka tayari wakifika kiezi 5 tu unauza kwa 10000 lakini ukiwaacha hadi miezi 8 jogoo ni wakubwa sana na wanauzwa 15000 -20000. Unakuwa huna pressure ya kukubali bei ndogo maana hawali chakula kingi. Faida ya pili wanataga mapema kuliko wa kienyeji hivyo wanaanza kujilisha wenyewe wakiwa na miezi 6 kuendelea na vilevile waweza kuwatumia mayai yao kutotoa vifaranga aidha kwa kuwatumia tetea wa kienyeji pure au incubator na hivyo kutokuwa na haja ya kununua tena vifaranga wengine. Nitajaribu kuweka mchanganuo wa gharama na faida ingawa nikiangalia sio tofauti na iliyowekwa na RETI hapahapa. Lengo langu ni kuongeza aina nyingine ya kuku chotara ili kuwa na aina tofautitofauti, kuanza kutengeneza chakula changu mwenyewe kupitia formula nilipewa na ex SUA lecture na Dr mifugo sasaivi yuko wizarani yeye na mkewe wameitumia na waliniambia inafaa sana ingawa itabidi nipate ushauri wa mwenye mashine kiwango cha usagaji na uchanganyaji wa chakula nitaleta feedback hapa. Nawashukuru wote kwa michango yenu Mungu azidi kuwafanikisha zaidi ktk malengo yenu.

Ubarikiwe sana..

Binafsi sio shabiki wa kuku chotara na hasa kutokana na uoga wa matunzo na gharama zake, Lakini kwa hili unanitia hamasa nianze japo kufuga kwa majaribilo angalau wawili watatu.

Vipi kwenye soko lake kwa hapa Dar es salaam watu wanawanunua kwa bei ile ile sawa na wa kienyeji au wanataka uwauze kwa bei ya broilers??
 
Naombeni msaada wenu, nina vifaranga vya kuku chotara ambavyo vina umri wa wiki 7.
Tatizo ni kwamba miguu yao inakosa nguvu, wanashndwa kutembea.
Nilimpeleka mmoja kwenye duka la dawa za mifugu, wakamchunguza na kunipatia dawa ya vitamin kwa kuwa walinieleza kuwa miili yao imeshndwa kutengeneza vitamin B plus.
Tatizo bado linaendelea japokuwa nilianza kuwapatiwa vitamin hao vifaranga wote. Nasubiri ushauri wenu wanajamvi.

Kama unawalisha kwa kutumia chakula cha kutengeneza mwenyewe usisahau kuweka CHOKAA YA MIFUGO kwenye mchanganyiko wao, hii sio chokaa ile ya kujengea au ya kupaka kwenye urembo wa nyumba, ni chokaa maalumu huuzwa kwenye maduka ya mifugo..

Lakini pia yawezekana likawa ni tatizo la ukosefu wa protini katika ukuaji wao kwani protini hujenga mwili kama itakosekana kwenye chakula vifaranga vitadhoofu sana na wewe utaona kama vinakosa nguvu hususani za miguu lakini kimsingi ni udhaifu wa mwili mzima, ni bora ukawapa wadudu kama mchwa na funza(kuna utaalamu wa kuwtengeneza funza na mchwa humu) bila kusahau majani mabichi yanayochipua kwa ajili ya vitamins nyingi sana kwa kuku hasa wanaokua..

Hope utawaona wakichangamka soon...
 
Asante kwa kweli hat mie mwanzo nilisita kuwachukua kwasababu niko kibiashara zaidi, nilichukua kam 18 nikawa nawalaza stoo ya nje asubuhi wanashinda chini ya miti na bustani chochote nilichonacho nawapa ila chanjo muhimu na chakula chao nawapa ingawa sio walaji kama broiler. Nilikuja baadae kuokota mayai daily na kuuza majogoo 15000 hii ikanitia moyo. Hawa Dar huwezi uza kama broier labda wawe wa miezi miwili au 3 mtu anaenda kuwafuga vinginevyo ni 10000-25000. Na soko ni kubwa wanaoenda kuwafuga, wakula familia, baa na hoteli, wachuuzi sokoni. Endapo mtu unataka kuwauza jumla basi unaweza mwenyewe kupunguza bei kama unataka hela nyingi kwa pamoja lakini si chini ya 10000. Tatizo wengi tunafanya ufugaji ni hobby au vitoweo na sio source of income. Ukimsoma Kubota ni kuwa ali dedicate muda wake kuwaangalia kuwalisha kuwatibu ili kuweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku wa kienyeji pure. Sasa sie wengine waajiriwa, familia, safari kweli niajiri mtu atakuwa makini na mbunifu kufikia malengo yangu au utaishia kumlipa mtu mshahara na kulaumu hana faida. Hawa kukisia tu nimetumia wastani sio zaidi ya laki moja unusu kwa mwezi kwa umri huu nikiamua kuuza wote bila kusubiri niokote mayai pia bado faida ipo.... kwa hivyo pamoja na kitoweo, hobby ni source of income pia na ninaweza tengeneza vifaranga wangu pia.
Ubarikiwe sana..
a
Binafsi sio shabiki wa kuku chotara na hasa kutokana na uoga wa matunzo na gharama zake, Lakini kwa hili unanitia hamasa nianze japo kufuga kwa majaribilo angalau wawili watatu.

Vipi kwenye soko lake kwa hapa Dar es salaam watu wanawanunua kwa bei ile ile sawa na wa kienyeji au wanataka uwauze kwa bei ya broilers??
 
Hongereni kwa ujasiriamali wakuu.
Nina swali kidogo naomba kufahamishwa.
Ile homa ya kuku (kideri) huwa ni kipindi gani katika mwaka.
Let say kuanzia mwezi gani mpaka mwenzi gani?
Kiangazi, masika, kipupwe, au??
 
Wakuu wote, (Kubota et al). Mungu mwenyezi katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth, awabariki sana.

Mkuu Chasha, naomba kujua jinsi ya kuandaa mbegu za mpapai kama dawa ya kideri. Ubarikiwe.

Umesali kwa hisia sana mkuu, tumia maarifa uliyopewa na wakuu wote wa humu, neno umaskini utalisikia magazetini tu.
 
naona kafanya mental calculation kupitia maelezo yako au ya GAZETI... kwa kweli ni ngumu kujua idadi kamili ila tu afuate maelezo ili kuweza kufikisha malengo yake.

Ni kweli Mkuu Mama Joe, ninakukubali sana. Nilipoanza kuku walikuwa wanatotolewa sana na vifaranga walikufa sana hadi nilipokuja kugundua siri ndiyo kundi likaanza kupanuka.
 
Hongereni kwa ujasiriamali wakuu.
Nina swali kidogo naomba kufahamishwa.
Ile homa ya kuku (kideri) huwa ni kipindi gani katika mwaka.
Let say kuanzia mwezi gani mpaka mwenzi gani?
Kiangazi, masika, kipupwe, au??

Nililona uhakika nalo masika ni nadra kutokea.
 
Mkuu Ibra6 unaporejea maneno yangu ni vema u-quote post yangu maana sikumbuki kama nimewahi simulia kitu hiki ulichoandika, kuku 630? Miezi sita? Nashindwa kukujibu maana naona hainihusu.
Kubota, hebu nitie moyo ndugu yako, maana ndiyo nataka kwenda kuanza hii biashara, lakini mimi nataka kuanza na kuku kama 50 hivi. Hebu niambie ni kwa kiasi gani umeona inalipa?
 
Kubota, hebu nitie moyo ndugu yako, maana ndiyo nataka kwenda kuanza hii biashara, lakini mimi nataka kuanza na kuku kama 50 hivi. Hebu niambie ni kwa kiasi gani umeona inalipa?
Mkuu sina shaka umejiandaa vya kutosha kwa kujenga mabanda, vifaa vya chakula, vyakula, ulinzi na madawa. Ninaimani pia kuwa kama umesoma uzi huu wote na nyuzi zingine za ufugaji kuku humu utapata maarifa ya kutosha ambayo ukichanganya na akili zako utachukua maamuzi muafaka kuepuka hasara zinazosababishwa na kutokuwa na uelewa. Mimi binafsi ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa kuku wanasoko la uhakika. Huku niliko soko ni kubwa. Hasa kama unalenga kuuza kipindi cha mahitaji makubwa ya kitoweo yaani sikukuu. Bei za kuku wa kienyeji ziko juu kama ambavyo wachangiaji wengi wanavyotoa ushuhuda humu! Nadhani umeshasoma! Changamoto kubwa ni kwa wewe mfugaji kuweza kuzalisha kuku kwa wingi kadri uwezavyo hapa ndiyo uwe tayari kupambana siku za mwanzo za ufugaji wako kuweza kuwakuza vifaranga kwa wingi. Ni imani yangu kwa kuwa tayari utakuwa umesoma michango mingi utakuwa na tahadhari huenda usipitie magumu tuliyoanzia wengine, isipokuwa anza taratibu kisha baadae upanue uzalishaji wako kadri utakavyojiamini kuwa unaweza! Ukishamudu ufugaji huu hakuna shaka inalipa sana sana. Jitahidi usome uzi wote huu kama hujafanya hivyo.
 
Salaam nd. Kubota na wachangiaji wote wa uzi huu. Inabidi nikiri kujiunga JF kuufuata Uzi huu. Nikiwa kwenye utafiti wa kukabiliana na tatizo la magonjwa na chakula cha kuku wa kienyeji, nimejikuta nikidondokea kwenye uzi huu mara kadhaa, natanguliza shukrani kwa fadhila za maelezo/tafiti/changamoto na fulsa mlizopitia kufika mlipo, amini hamtupi hela ila njia ya kuipata kwa wingi.
Mbarikiwe sana, na Mungu atugawie penye manono ya nchi na umande wa mbingu wingi wa nafaka, mvinyo na kuku pawe makao yetu.
 
Mkuu kubota tunajua we mfugaji practical.sio mfugaji wa thiory.wafugaji wengi ni wa hobby na thiory! Vumilia maswali
 
Umetushirikisha kuanzia vifaranga hadi wanafikia kuuzwa,ukaishia hapo! Tueleze ulivyouza. idadi, bei awam,wateja,ugumu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom