Asigwa ndugu yangu vp umeshapima upepo?naomba mrejesho
Bado Mama timmy kuna kundi la kuku hapa ninalo nasubiri likifikisha umri fulani wa kuweza kuhimili mikiki ya kujitafutia chakula ndio nilitumie kupimia upepo maana afya yao naona hainiridhishi na mbegu yao ni ile haramu...

Ila baada ya wiki kama nne hivi nafikiri watakua wametosha kupewa hizo dawa nafikiri itakua wakati mzuri wa kuleta mrejesho hapa....
 
Nashukurukuru ndugu yangu kwa taarifa.ninasubiri kusikia kutoka kwako baada ya hizo wiki nne.
 
Wakuu nina document fulani fulani hapa za vituo tofauti tofauti vya ufugaji wa kuku wa kienyeji na mbinu zao kama mtataka ntazia-attach hapa na nitamuomba mkuu Kubota aziunganishe mwanzo mwa uzi ili kila mtu atakae utembelea huu uzi aweze kuzi-download na kuzitumia binafsi

Nafikiri kesho nikipata nafasi nitazituma kwa sasa natumia simu, kama wazo hili litafaa basi niruhusuni niziweke

Natanguliza shukrani sana kwenu.....
 
Last edited by a moderator:
Kubota asante kwa somo, naona pattern inajieleza vizuri kabisa, kiasi fulani nitaweza kuifanya ingawa eneo ni dogo. Naomba kuuliza je inawezekana kuchanganya mifugo mfano mbuzi wakachunga na kuku au inabidi hawa wawekwe tofauti? ninamaana ktk kitalu kimoja na kwa wakati huohuo nikawaachia kuku na mbuzi kuchunga pamoja? Nimesoma kuwa bata sio vizuri kuwachanganya maana wanavidudu vingi vinavyoathiri kuku. Naomba kujua hii habari ya mifugo mingine. Asanteni sana.

Ufugaji kuku huria wenye faida
Wadau wa ujasiliamali JF huu ni mwendelezo wa maelezo ya mchoro na ufugaji huria kwa ujumla. Si kuku wa kienyeji tu bali kuku wa mayai na broiler wanaweza kufugwa kwa faida kubwa kwa kuwafuga huria wakichunga kwenye majani. Hii hupunguza gharama za ufugaji. Kuku hula majani kwa kiasi kikubwa sana. Hata hivyo jambo la muhimu sana ni upya wa majani anayokula kuku. Ndiyo maana lazima kuwalisha kwa mzunguko ili kila wakati wachunge kwenye eneo ambalo majani yamechipua na hayana uchafuzi. Uchungaji huu hupunguza gharama ya chakula cha kuku kwa kiasi zaidi ya 60%. Ni vema malisho yakaboreshwa kwa kupanda ndani yake majani ya jamii ya mikunde ambayo kuku hupendelea zaidi.

Kuhusu swali lako Mkuu Mama Joe yawezekana kuchanganya kuku na mbuzi. Ufugaji huria wa kuku umekuwa ukifanyika kwa mafanikio kwa kuchanganya ng’ombe na pia kuku na kondoo. Hii inasaidia kwa vile kuku hubakisha kiasi kikubwa cha majani marefu hivyo ngombe au kondoo hufyeka kabisa na kuacha majani yako level.

Kwa mfano kwenye mchoro wa ufugaji huria nilioambatanisha kwenye post yangu iliyotangulia, ng'ombe (1 kwa ekari) anaweza kuchungwa kwenye plot kabla kuku hawajaingizwa ili kuyaweka majani kwenye kimo ambacho kuku wanaweza kula majani vema.Kuku huvutiwa sana na majani chipukizi yanayochipua baada ya ng'ombe kuchunga. Kuku huruhusiwa kuingia kuchunga baada ya siku nne baada ya ngombe kuchunga. Kuku huchakura chakura samadi ya ng'ombe na kula wadudu na funza kadharika na viini ambavyo ni lishe kwa kuku. Kuku husafisha malisho kwa kula wadudu maadui wa ng'ombe.

Kuhusu mbuzi na kuku wanaweza kuchanganyika bila shaka maana hawaambukizani magonjwa kirahisi. Hata hivyo kondoo ndiyo husaidia sana kufyeka majani baada ya kuchunga kuku! Mara nyingi kuku wanaweza kuchunga kwa kuchagua majani na kuacha mengine marefu, wakishatolewa kondoo huingia ili kupiga levo kabisa au ikibidi kuku na kondoo wanaweza kuchungwa pamoja. Kondoo au mbuzi 5 hadi kumi huweza kutoshelezwa na ekari moja kulingana na aina yao.
 
Wakuu nina document fulani fulani hapa za vituo tofauti tofauti vya ufugaji wa kuku wa kienyeji na mbinu zao kama mtataka ntazia-attach hapa na nitamuomba mkuu Kubota aziunganishe mwanzo mwa uzi ili kila mtu atakae utembelea huu uzi aweze kuzi-download na kuzitumia binafsi

Nafikiri kesho nikipata nafasi nitazituma kwa sasa natumia simu, kama wazo hili litafaa basi niruhusuni niziweke

Natanguliza shukrani sana kwenu.....

Mkuu Asigwa nami natanguliza shukrani kwa ukarimu wako, nasubiri kwa hamu hizo documents za ukombozi.
 
wakuu kwenye kufahamu aina ya majani ambayo kuku hupendelea naoma atulistie hapa. Mkuu Kubota ameshauri kuwa ni vema malisho yakaboreshwa kwa kupanda ndani yake majani ya jamii ya mikunde ambayo kuku hupendelea zaidi. Anayejua hizo jamii ya kunde na mengine atuorodheshee, asanteni
 
Ufugaji kuku huria wenye faida
Wadau wa ujasiliamali JF huu ni mwendelezo wa maelezo ya mchoro na ufugaji huria kwa ujumla. Si kuku wa kienyeji tu bali kuku wa mayai na broiler wanaweza kufugwa kwa faida kubwa kwa kuwafuga huria wakichunga kwenye majani. Hii hupunguza gharama za ufugaji. Kuku hula majani kwa kiasi kikubwa sana. Hata hivyo jambo la muhimu sana ni upya wa majani anayokula kuku. Ndiyo maana lazima kuwalisha kwa mzunguko ili kila wakati wachunge kwenye eneo ambalo majani yamechipua na hayana uchafuzi. Uchungaji huu hupunguza gharama ya chakula cha kuku kwa kiasi zaidi ya 60%. Ni vema malisho yakaboreshwa kwa kupanda ndani yake majani ya jamii ya mikunde ambayo kuku hupendelea zaidi.

Kuhusu swali lako Mkuu Mama Joe yawezekana kuchanganya kuku na mbuzi. Ufugaji huria wa kuku umekuwa ukifanyika kwa mafanikio kwa kuchanganya ng'ombe na pia kuku na kondoo. Hii inasaidia kwa vile kuku hubakisha kiasi kikubwa cha majani marefu hivyo ngombe au kondoo hufyeka kabisa na kuacha majani yako level.

Kwa mfano kwenye mchoro wa ufugaji huria nilioambatanisha kwenye post yangu iliyotangulia, ng'ombe (1 kwa ekari) anaweza kuchungwa kwenye plot kabla kuku hawajaingizwa ili kuyaweka majani kwenye kimo ambacho kuku wanaweza kula majani vema.Kuku huvutiwa sana na majani chipukizi yanayochipua baada ya ng'ombe kuchunga. Kuku huruhusiwa kuingia kuchunga baada ya siku nne baada ya ngombe kuchunga. Kuku huchakura chakura samadi ya ng'ombe na kula wadudu na funza kadharika na viini ambavyo ni lishe kwa kuku. Kuku husafisha malisho kwa kula wadudu maadui wa ng'ombe.

Kuhusu mbuzi na kuku wanaweza kuchanganyika bila shaka maana hawaambukizani magonjwa kirahisi. Hata hivyo kondoo ndiyo husaidia sana kufyeka majani baada ya kuchunga kuku! Mara nyingi kuku wanaweza kuchunga kwa kuchagua majani na kuacha mengine marefu, wakishatolewa kondoo huingia ili kupiga levo kabisa au ikibidi kuku na kondoo wanaweza kuchungwa pamoja. Kondoo au mbuzi 5 hadi kumi huweza kutoshelezwa na ekari moja kulingana na aina yao.

Mkuu kubota kabla hujahama kwenye hii mada naomba ufafanuzi kidogo katika mambo matatu hapa
  • Mimea jamii ya mikunde unayoizungumzia hapa ni hii ya maharage, kunde na aina zake??
  • Umeongelea suala la uwezekano wa kupungua kwa kiasi cha chakula kwa takribani 60% ya chakula, hii ni ifromation nyeti sana kwa wajasiriamali. Swali hapa ni je kama nitapanda say majani ya aina moja kwa kuku na wakawa wanakula kwa mwaka mzima aina hiyo hiyo ni vizuri au inafaa kuchanganya changanya majani ya aina tofauti ili kubadili aina ya virutubisho wanavyopata kuku??
  • Vipi hawa mbuzi wa maziwa na nyama naowaona wanafugwa mitaani siku hizi hapa Dar es salaam wanaoachiwa wanachunga hovyo tu je wanafaa?? Nauliza maana najua mbuzi hupenda sana majani ya kwenye vijimiti na vimiba miba sasa kama nitawa-limit wawe wanakula majani hayo ayo kila siku haina athari kwao kiafya??

Shukrani sana mkuu
 
Wakuu nina document fulani fulani hapa za vituo tofauti tofauti vya ufugaji wa kuku wa kienyeji na mbinu zao kama mtataka ntazia-attach hapa na nitamuomba mkuu Kubota aziunganishe mwanzo mwa uzi ili kila mtu atakae utembelea huu uzi aweze kuzi-download na kuzitumia binafsi

Nafikiri kesho nikipata nafasi nitazituma kwa sasa natumia simu, kama wazo hili litafaa basi niruhusuni niziweke

Natanguliza shukrani sana kwenu.....

Tutashukuru kuzipata, asante kwa wema wako.
 
Last edited by a moderator:
Hakika nilipotea kidogo ..............ila kuku wangu wanaendelea vizuri kupitia somo la humu darsani
 
please nami waweza kunitumia huo mchanganuo mkuu,sijawahi kufuga but my aim ni kuanza na 1000 layers
 
Mkuu kubota kabla hujahama kwenye hii mada naomba ufafanuzi kidogo katika mambo matatu hapa
  • Mimea jamii ya mikunde unayoizungumzia hapa ni hii ya maharage, kunde na aina zake??
  • Umeongelea suala la uwezekano wa kupungua kwa kiasi cha chakula kwa takribani 60% ya chakula, hii ni ifromation nyeti sana kwa wajasiriamali. Swali hapa ni je kama nitapanda say majani ya aina moja kwa kuku na wakawa wanakula kwa mwaka mzima aina hiyo hiyo ni vizuri au inafaa kuchanganya changanya majani ya aina tofauti ili kubadili aina ya virutubisho wanavyopata kuku??
  • Vipi hawa mbuzi wa maziwa na nyama naowaona wanafugwa mitaani siku hizi hapa Dar es salaam wanaoachiwa wanachunga hovyo tu je wanafaa?? Nauliza maana najua mbuzi hupenda sana majani ya kwenye vijimiti na vimiba miba sasa kama nitawa-limit wawe wanakula majani hayo ayo kila siku haina athari kwao kiafya??

Shukrani sana mkuu

Aina nzuri ya mikunde kwa malisho ya kuku ni Red clover, white clover na Alfalfa, kama unaweza mtaalamu wa mifugo anaweza kukuonyesha mimea hii maana sijui majina yake kwa kiswahili.

Majani hata kama ni ya aina moja haina tatizo kikubwa yawe ni yale yanayochipua maana hata hivyo atajazia virutubisho vingine kutoka kwenye chakula cha ziada (concentrate) ambacho ni lazima pia uwawekee!

Viumbe wala majani huwa wanabacteria tumboni ambao hubadili wanga ulioko kwenye majani kwa hiyo ingawa ni vema wakita majani mchanganyiko yakiwemo ya mikunde lakini wanaweza kuishi kwa kula aina moja ya majani tu. Tabia ya mbuzi kula majani yaliyoko juu ni survival mechanism lakini haimaanishi hawawezi kuishi pasipo majani ya juu. Mbuzi hufugwa kwa kukatiwa na kulishwa majani kama ng'ombe! Ila Mkuu Asigwa huko kwenye mbuzi umenipeleka sina uzoefu nako sana. Kama wajuzi wa mifugo watapita hapa watasaidia kujazia.
 
ndugu Kubota na jamii ya wafugaji kuku kwa jumla, ninajiandaa kufuga kuku kuanzia august, krismas nataka kula kuku live kutoka bandan.
mwez ujao najenga banda la miti lililokandikwa na udongo, na kuezekwa na makuti, milango ya bati, itakuwa na chemba tatu 1 kulala na kuatamia, wakitotoa wanamishiawa geto namba 2 na vifaranga vyao, geto la 3 ni Jela.
sasa mchwa ndio shida eneo hili nahis watadondosha banda ndan ya siku 180, je kuna dawa ya kupaka mchwa wasile iyo miti ya banda?
 
Mkuu Ankojei nakupongeza sana kwa mikakati yako natumaini utafanikiwa. Nami nasubiri mchango wa wadau jinsi ya kudhibiti mchwa. Tuko pamoja!
 
WANA JF UJASIRIAMALI - BIG UP SANA. Kwa kufuatilia kwa makini shauri hizi, infact nimeweza atleast kujikongoja na nina imani lengo langu la kufiksha kuku wa kienyeji 2000 kwa kutumia huu azlishaji wa kiasili nitaweza. nilianza na kuku 31 wale wa Malawi, na hivi sasa ninao 604. Ni weusi tiii, wanafurahisha ukiwatazama. Mimi niko wilaya ya Ileje, Mbeya jirani na Malawi.Bahati nzuri pumba, mashudu , na mtama vinapatikana kwa wingi. Kijijini nako kuna faida. Nategemea NANE NANE niuze baadhi ili kujikimu kwa mahitaji mengine. NAKUKUBALI SANA NDUGU YANGU SENIOR EXPERT MEMBER. Ila naomba simu no. yako kuna kitu nataka unipe ushauri nikiwa bandani.
 
POLITICS NA MAPENZI FORUMS hakuna kitu kule zaidi ya upuuzi tu. Nimefurahi sana hadi mke wangu na watoto wanapenda hii forum yetu, na kabla hawajaingia bandani lazima wakamue nn wana JF wameshauri. Na tunapokuwa sitting room tukisubili mlo wa jioni , tuna discuss yaliyojili kwa siku nzima, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kuku kwa ujumla. Nawashukuru sana mtandao wa AIRTEL kuwa na kasi kubwa ya ku download mambo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom