Ufugaji Nguruwe Kibiashara sio rahisi ila unawezekana🙂

Kiongozi..Unalima bamia pekee au mboga gani nyingine zinalipa .?
Unalima bondeni au unatumia maji ya kisima..?
Bamia, hoho, nyanya na mchicha. Maji ya kisima unaweka pump na simtank. Ukiweza unaweka mabomba ya chini, mimi ninatumia mpira na bomba la kuzunguka.

Miti ya matunda nimepanda kwenye mipaka ya shamba mfano maembe na maoera.
 
wafugaji wengi si walimaji ndio maana unakuta wanshindwa kumudu mifugo yao.
ukitaka kuwa mfugaji mzuri usiye teteleka hakikisha kuwa shamba kubwa la kulima kama mazao yanao weza kulisha mifugo na kufanyia biashara kidogo.
unaweza kuanzisha shamba la nyasi kubwa ili kama una ng'ombe na mbuzi.
hata miti aina fulani kwa ajili ya kulishia.
nguruwe shamba lake kwa ajili yake ni kulima mboga mboga,matunda,maindi,nyanya na hata kama watu wakishindwa kununua basi ni chakula.

stoo ya kuifazia nafaka kwa ajili ya mifugo na nyasi zisikauke.

uwa viongozi wenu wakienda ulaya wanaenda kufanyaga nini huko kuja kuwaeleza hili.
nilijifunza nchi za watu
 
Umeongea POINT sn mkuu!
 
Bamia, hoho, nyanya na mchicha. Maji ya kisima unaweka pump na simtank. Ukiweza unaweka mabomba ya chini, mimi ninatumia mpira na bomba la kuzunguka.

Miti ya matunda nimepanda kwenye mipaka ya shamba mfano maembe na maoera.
Nashkuru sana mkuu kwa maarifa haya. Nina access ya kiasi kikubwa Cha ardhi ila sijamaster kilimo Cha mbogamboga

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Naombeni msaada kwa wataaramu wanao jua namna nzuri ya kufuga nguruwe wa biashara na wanachukua mda gani mpaka wanakua tayari kwa kufanyiwa biashara
Karibuni sana kwa maoni
 
Vidonge vya ARV's huchanganywa kwenye chakula chake.Mnifunge tu ila hata kuku hufanyiwa ivo.
Aisee very interesting...! kwahiyo kinachanganywa vipi, kidonge kimoja Kwa kilo ngapi ya chakula/Kwa nguruwe mwenye uzito gani/wanakila Kwa siku ngapi maana binadamu si wanatumia kwa kila siku...!

Hivi ushawahi kuona hao wafugaji wa kuku na nguruwe wanatumia hivo vidonge au nawewe unaskia Tu kama wengine tunavoskia?
 
Njoo uyole mbeya mitaan humu ujionee mkuu...vidonge viwili hulowekwa kwenye maji Lita moja then unachanganya kwenye chakula cha nguruwe...kuku huwekewa kwenye maji ya kunywa
 
Njoo uyole mbeya mitaan humu ujionee mkuu...vidonge viwili hulowekwa kwenye maji Lita moja then unachanganya kwenye chakula cha nguruwe...kuku huwekewa kwenye maji ya kunywa
Shukrani Kwa ushuuda mkuu, Ila hiyo issue nahisi imekaa kiimani Sana, inawezekana wanafanya Tu kwa mkumbo ila matokeo wanayopata hayatokani na hivo vidonge au inawezekana ni kweli

Me nipo Dar na nafuga pia, lakini najuana na wafugaji wenzangu wengi tu ila hakuna ata mmoja ambae anafanya hizo Mambo, tuliishia kuziskia tu, na kuna uwezekano mkubwa kuna wafugaji wanatumia kwa mkumbo tu bila kuwa uhakika na wanachokitafuta

Mikoa kama Mbeya wafugaji wengi wanafuga nguruwe wa kienyeji, nguruwe ambae akizaliwa Hadi kufikisha kilo 50 inabidi ukae nae zaidi ya miezi 6 kwahiyo ni rahisi wao kutumia kila Aina ya mavitu wanayoskia wakati mchawi wao ni Aina ya mbegu za wanyama wao

Watu hudhani kazi ya ARV ni kufanya waathirika wa ukimwi wanenepe na hiyo ndio nadharia wanayotumia wafugaji kama hao wa Mbeya, ilhali uhalisia ni kwamba vile vidonge huzuia/hupunguza multiplication ya virus hivo kufanya muathirika kuwa load ndogo ya HIV virus katika damu

Baada ya virus kupungua damuni hapo CD4 zinapanda juu, mtu anakuwa mgumu kushambuliwa na magonjwa nyemelezi na mwisho wa siku ata chakula anachokula kinaenda kufanya kazi yake mwilini, kwahiyo hizo nadharia za kutumia ARV wanatumia wafugaji wachache Sana na wengi wao ni Wajinga
 
Naombeni msaada kwa wataaramu wanao jua namna nzuri ya kufuga nguruwe wa biashara na wanachukua mda gani mpaka wanakua tayari kwa kufanyiwa biashara
Karibuni sana kwa maoni
Jaribu university of google and youtube utapata kila kitu, ila kitu muhimu ukitaka kufuga ni lazima utumie wataalam wakushauri na kukuelekeza maana kuna magonjwa mengi na changamoto nyingi ambazo wataalam watakusaidia kirahisi sana ukiwatumia, niliwahi kuona jamaa kapoteza banda zima kwa ajiri hakuwapa chanjo wanyama wake
 
Tatizo pumba zimepanda bei sanaa!!
Ndio maana muanzisha mada akasema kufuga kisasa. Hapa inamaana ht suala la pumba ni lakulitazama ni kipindi Gani pumba bei rahisi. Pandisha nguruwe wako huku ukitazamia watazaa kipindi Gani ili ukawalishe watoto kwa pumba za bei nafuu. Kwa mfano una majike 10 unataka kuyapandisha ni vyema ukayategea ukayapandisha kuanzia mwezi wa kumi na mbili na January ili wakazae mwezi wa nne na watano ambapo mahindi, alizeti na mpunga unavunwa hapo Sasa inawezekana kuwalisha kwa bei nafuu huku unaweka stock itakatokusaidia kuanzia mwezi wa nane mpk wa 11. Lazima tujue ufugaji unahitaji pesa isiyo na mawazo,
 
Asante
 
Bofya kwenye kitufe cha 'Search' hapo juu ya browser kulia, ingiza key word 'Nguruwe'...utapata list ya thread zote humu zinazohusu ufugaji wa Nguruwe, pamoja na majibu ya maswali yako mengi!!:(:(
 
Habarini za mwaka mpya wana Jf!

Baada ya muda mrefu kuto post makala humu (nimekuwa busy kwenye media zingine kama instagram, utube,whatsap,telegram..),acha leo nichangie kidogo maana nimeona post nyingi kuhusu ufugaji nguruwe zenye mapungufu. Wakongwe wa Jf watanikumbuka maana nime post sana makala za ufugaji humu miaka hadi kumi iliyopita.

Ufugaji nguruwe kibiashara sio rahisi ila unawezekana.Ugumu unakuja kwa sababu ni biashara na biashara zote zina kanuni ili kujipa uwezekano wa kufanikiwa. Ili uweze kufanikiwa katika ufugaji nguruwe kuna maeneo makubwa mawili:

A.Uzalishaji
Uzalishaji wenye tija unategemea mbegu na matunzo. Matunzo ni mambo yanayohusisha mazingira ya kuishi wanyama, lishe sahihi, chanjo/tiba na utarartibu wa kuzuia magonjwa kuingia kwenye mradi.

B. Masoko
Hakuna namna mradi wako utadumu bila kuuza bidhaa zako. Biashara yoyote haiwezi kudumu kama hakuna mauzo. Wafugaji wengi huanza ufugaji bila kufanya utafiti wa soko na miradi yao hukwama

Hivyo kama unataka kufanya biashara kwenye ufugaji nguruwe chukua hatua hizi
1. Tafiti kuhusu ufugaji nguruwe kupitia machapisho mbalimbali kam vitabu,makala mitandanoni kama google,instagram na utube.

Hii itakusaidia kuuelewa ufugaji na changamoto/fursa zilizopo.

2. Pata ushauri toka kwa wafugaji wazoefu. Kuna faida kukutana ana kwa ana au kwa namna nyingine na mtu mwenye uzoefu kwenye ufugaji ukaweza kujadili nae na kujifunza mambo muhimu. Hata kama utahitajika kulipia huduma hiyo fanya.Ni muhimu sana kwako

3. Tafiti kuhusu soko la bidhaa za nguruwe. Hapa fanya utafiti wewe binafsi ndugu,usitegemee maneno ya kuambiwa. Soko la bidhaa za nguruwe lipo ila haina maana soko la bidhaa zako wewe lipo linakungoja!!

4. Amua bidhaa utakazozalisha na weka malengo kulingana na soko la bidhaa zako

5.Anza mradi kwa kuongozwa na mshauri mzoefu. Kila kitu kinategemea malengo yako:aina ya mbegu,ukubwa wa mradi,soko......

Ni waandishi pia wa kitabu cha ufugaji nguruwe cha kiswahili rahisi kwa kila mtanzania 'Kanuni za Ufugaji Nguruwe wenye tija'

Waweza wasiliana nasi kwa 0789412904/0754393838 kwa simu au whatsap. Tusipopokea andika ujumbe tutakupigia.

Nakubali mkuu Malafyale piga kazi
 
Nina ekari 5 za shamba Morogoro manispaa, mtaa wa ngerengere...

Nimekuwa na ndoto ya kufanya kilimo cha kisasa cha mbogamboga kama vitunguu, nyanya, hoho, bamia, kabichi, n.k, lakini pia kujenga mabanda mazuri ya ufugaji wa nguruwe, kuku na mbuzi!

Pamoja na kuwa na nia hiyo, sijaweza kuanzia kwani ili yote yaweze kufanyika napaswa kuchimba kisima kirefu hiki kinataka kati ya Mil.8-12 kikiwa na miundombinu yake madhubuti!(hiyo pesa sina)

Niliwahi kuwafuata wachimbaji wa visima ili tufanye makubaliano, wanichimbie then mimi niwalipe kwa instalments hata kama itakuwa zaidi kidogo ya bei ya kawaida, hawakunielewa!

Lakini nina hakika kwamba, nikifanikiwa kutengeneza miundombinu niliyoitaja hapo juu, ndani ya mwaka nitakuwa na uhakika wa kutengeneza sio chini ya Milioni 40, (well analysed) kwa hili shamba la ekari 5!

Lakini bahati mbaya sana banks zetu haziamini sana uwekezaji wa shambani, hivyo kutoa mikopo pia ni changamoto kubwa, lakini kama ningepata mtu anayekubali kufanya partnership kwenye hili, tungepata faida nzuri tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom