Ufugaji samaki kibiashara

Oct 2, 2019
5
2
Mbinu muhimu wakati wa uanzishaji ufugaji wa samaki

i. Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji. Ni wazi kuwa dhamira ya kweli ni kitu muhimu sana unapotaka kufanya jambo lolote kwani bila kudhamiria basi huwezi kufanikiwa, matokeo ya kutokuwa na dhamira ni kukata tamaa pindi utakapokutana na changamoto ya aina yoyote lakini ukiwa umedhamiria utakuwa na uwezo wa kuzikabili changamoto na hivyo kujikuta ukifika mwisho wa safari yako huku ukiwa na mafanikio

ii. Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa samaki. Tathmini hii inahusisha nguvukazi, rasilimali pesa, pamoja na umiliki wa eneo. Mkulima akiweza kujitambua na kutambua uwezo wa nguvukazi aliyonayo itakuwa ni rahisi kwake kuyamudu majukumu mbalimbali yaliyopo katika ufugaji, pia katika suala la kutambua ukubwa wa ardhi aliyonayo litamsaidia kujua idadi ya samaki anaoweza kufuga pamoja na kiasi cha fedha kinachohitajika.

iii. Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi au bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuufadhili mradi.

iv. Hulka ya uvumilivu na kuthubutu.

v. Tathmini ya soko la bidhaa za samaki.

vi. Kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samaki.

vii. Kuwa na mtaalamu au mshauri katika kipindi chote cha Ufugaji.
 
Asante kwa somo zuri mjumbe.
Hivi ukiachana na vyakula vya samaki vya madukani.

Samaki anakula chakula gani cha kulima shambani ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom