Ufisadi wa Johnson Lukaza

......hali ya johnson kipesa sasa hivi ni mbaya sana..kwani akauti zake zote zimeminywa yakiwemo yale magari..najuta kwa nini sikununua moja ya apartment zake ..kwani nisingemlipa[ningejilipa pesa zetu alizokunywa]..hata hivyo kwa walionunua apartment zake huko sigara nashauri wasimlipe!!

jammaa siku hizi anatembelea RAV four old model....mafuta yenyewe ishu!!....akauti zote freezed...msichangae mkasikia ame balalli!
 
...wakuu suala la johnson kuwa kwenye ile safari ya kwanza ya kutembelea dunia [takribani mwezi mmoja na nusu]..ilikuwa safari ya jk ya kwanza nje..ni kweli...ni mkifuatilia list ya walioambatana nae ile safari waliokaribia 100 ..asilimia kubwa wapo kwenye list ya mafisadi wa EPA......wanamtandawo!
 
......hali ya johnson kipesa sasa hivi ni mbaya sana..kwani akauti zake zote zimeminywa yakiwemo yale magari..najuta kwa nini sikununua moja ya apartment zake ..kwani nisingemlipa[ningejilipa pesa zetu alizokunywa]..hata hivyo kwa walionunua apartment zake huko sigara nashauri wasimlipe!!

jammaa siku hizi anatembelea RAV four old model....mafuta yenyewe ishu!!....akauti zote freezed...msichangae mkasikia ame balalli!

Duu?? ila hili somo kubwa sana kwa wapendao ufisadi!, na ama kweli malipo ni hapa hapa duniani, angalieni fisadi Mkapa anavo ishi utadhani Panya ndani ya shimo, anaogopa kivuli chake mwenyewe, Fisadi Lowasa last week nasikia Arusha aliokolewa na wauza supermarket moja kumficha chumba cha ndani baada ya kelele za fisadi kuanza sikika nje ya duka hilo,

Hii ya Lukaza, alivo kuwa akimwaga pesa kama njugu.. inatisha kama sasa hivi kibao kimemgeukia kiasi hiki!

Kumbe bora kushindia ugali matembele kwa raha zako kuliko kuwa fisadi ambao mwisho wake ndo huu!
 
JAMAA NI BALAA SANA ONA NYUMBA ANAVYOUZA........
Thank you for your enquiry, please be advised that the Flats are two bedroom flats with akitchen and a bathroom. The Flats' price is at Tshs. 35,000,000 Million for cash purchases and Tshs. 40,000,000 Million for twelve Months credit with 20% down payment. The flats have plenty of open areas in the estate. The estate will be proffessionally managed by PROIN TZ Ltd. for the peace of mind of al the clients. I hope i have addressed both of your concerns, if not please do not hesitate to contactus. Thanking you for your interest and look forward to hear from you soon. Kind Regards Abu Faraji

Mhhhhh

and who is this?
 
A man may rise to high success in the world, even to lofty attitudes in the spritual realm, and again descend into weakness and wretchedness by allowing arrongant, selfish and corrupt thoughts to take possession of him- James Allen 1834

No one can mantain victory (richness) attained by wrong thoughts and acts!
 
ES

by the way habari ya lile RANGE ROVER VOGUE ni kweli kabisa alisafirisha na BA cargo...lakini kuna kipande ambacho naona hukuweka

aliingia show room na brifcase imejaa £60,000 wazungu walikuwa hawajui cha kufanya naye mwishowe wakamuuzia hivyo vivyo kwa cash...

by the way £1=$2
hivyo hiyo ilikuwa ni $120,000

kwa pesa za madafu sijui ni kiasi gani lakini kama portfolio yake ni nyumba kama hizi...
chimati1.jpg
ea1200556605.jpg
nadhani £60,000 itakua ni lose change kwake
 
Jamni tukumbushane huyu Johnson Lukaza alikuwa katika kitengo gani??na ni nani huyu katika taifa hili la wadanganyika??

Johnson Lukaza kwa tunaomjua hapa Dar alikuwa dalali wa magari kutoka Dubai kabla ya kupigiwa pande la mipesa ya EPSA! Alikuwa akipatikana sana pale Falcon Restaurant Mnazi Mmoja mkabala na Mahakama ya Wilaya ya Ilala. Wala hayumo ktk duru la watawala
 
Sasa weew kama dalali kapewa dili mnamlaumu nini.. kapewa pande kakamua kweli... Angekataa angepewa mwengine so as they say same shit different toilet.... Bora kajitoa alivyokuja kuchukua hiyo Range Sport london alikua na nyodo yakufam2. Watu kama hawa nikuwafilisi to for their part and then go after the big dogs.
 
Hii ni mwendelezo wa toleo letu la wiki iliyopita katika mfululizo wa kuangalia CCM na Urafiki wenye Mashaka:

toleo14_phixr.jpg

Jisomee..
 
Attachments

  • TOLEOJIPYA14.pdf
    330.3 KB · Views: 384
Thanks man for this post, ukiangalia ile picha ya muungwana akimshika mkono Lukaza na pia ukaangalia yale yanayoendelea sasa.....picha hii inafanaa na ile ya Urafiki wa Kima na Mamba....kwa mnao kumbuka similar picture kwenye kitabu cha darasa la pili au tatu hivi!
 
Lakini msingi wa urafiki huu hasa ni nini? Kwanini CCM inapokea misaada kutoka kwatu watu of questionable character? Yawezekana kuwa CCM haijali misaada inatoka kwanini alimradi watu hao hawajakutwa na hatia mahakamani?

Ilipogundulika kuwa shangazi yake Obama kule MA (ambaye ni illegal) amechangia karibu dola 230 hivi kwenye kampeni ya mpwae Kamati ya Kampeni ya Obama ilirudisha fedha hizo mara moja. Imetokea pia kwenye wanasiasa wengi inapogundulika kuwa michango waliyopokea imetoka kwa watu ambao haifai kuwa nao karibu.. kwanini CCM haiwezi kufuata mfano huu kuonesha kuwa hata ile kuonekana wanakula sahani moja na mwizi ni no no!?
 
Lakini msingi wa urafiki huu hasa ni nini? Kwanini CCM inapokea misaada kutoka kwatu watu of questionable character? Yawezekana kuwa CCM haijali misaada inatoka kwanini alimradi watu hao hawajakutwa na hatia mahakamani?

Ilipogundulika kuwa shangazi yake Obama kule MA (ambaye ni illegal) amechangia karibu dola 230 hivi kwenye kampeni ya mpwae Kamati ya Kampeni ya Obama ilirudisha fedha hizo mara
. Imetokea pia kwenye wanasiasa wengi inapogundulika kuwa michango waliyopokea imetoka kwa watu ambao haifai kuwa nao karibu.. kwanini CCM haiwezi kufuata mfano huu kuonesha kuwa hata ile kuonekana wanakula sahani moja na mwizi ni no no!?
Mkjj hayo hayawezekani abadani katika CCM hii ya JK,Msekwa na Makamba. Tumeona vikao vikuu vya chama vikitumia nguvu kubwa kusafisha wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi huku viongozi hao wakuu wakifumba midomo kama vile jambo hilo ni jema.
 
Mwanakijiji,
Niliwahi kuongea na mwana CCM mmoja kuhusu michango inayotolewa na matajiri. Yeye alikiri kuwa Jeetu Patel ni tapeli na amechangia sana CCM na anafahamiana na wakubwa wengi katika chama. (Siku hizo neno ufisadi lilikuwa bado halitumiki) Patel ninamfahamu kwa sababu alianzia biashara zake Musoma. Nikamwuliza mheshimiwa hivi hamuoni shida kupokea fedha za Jeetu huku mnajua kuwa biashara zake ni za kitapelitapeli? Jamaa aliniangalia kana kwamba the issue had never crossed his mind.
 
lakini chama kama cha Mapinduzi kitaweza vipi kuendesha pasipo kuungwa mkono na wanachama wake? Lakini swali la muhimu nadhani pia ni kuona kwanini kuna ulazima wa CCM kuchangiwa wakati kinapokea ruzuku ya karibu bilioni 2 kila mwezi?
 
Labda hawajiamini. Si unaona jinsi Mc Cain alivyomshangaa Obama kuwashinda Republicans katika fund raising? Wenyewe (Republicans) walizoea kupewa hela na big Corporations wakati Obama alianzisha grass roots movement ya wachangiaji wadogo wadogo.
 
Jamani hivi operation sangara imeishia wapi? Si walisema watarejea baada ya wiki moja?

Katika vitu ambavyo vinawapa kichwa ngumu CCM ni kuwa na wapinzani wababaishaji. Kwanza OPARESHENI SANGARA kauli mbiu inayotoa hamasa yoyote ile.....!!!

Kwanini wasiita Tanzania Tunayoitaka..Ikawa kama vile kuwaambia wananchi watarajie nini kutoka kwao, na pia kupata maoni ya wananchi kuhus Tanzania Wanayoitaka!

Credibility ya viongozi wetu wa vyama vingi vya upinzani inatia mashaka sana!!
 
Mwanakijiji,

..ndiyo maana nikaanzisha posting kuhusu ripoti ya Philip Mangula kuhusu rushwa wakati wa kampeni za uraisi 2005.

..mnakumbuka jinsi Mkapa alivyokuwa akijigamba kushughulikia rushwa kwa kumtolea mfano Nalaila Kiula?

..wa-Tanzania tulimuamini Mkapa kweli kweli. tena tulikwenda mbali, kwa kushawishiwa na wanamtandao, na kudai Sumaye anamchafua Mkapa.

..sijui kama wananchi wamegundua ulaghai aliokuwa akiufanya Mkapa.

..cha msingi hapa ni kuifuatilia rushwa hii mpaka kwenye kilele chake. haitoshi kuwashughulikia hawa kina Jeetu Patel, tunapaswa kujua mahusiano ya mapesa haya na kampeni za uchaguzi za CCM.
 
Back
Top Bottom