Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Hahahahaha.... Ila nchi hii nyumbu wengi sana! Hapa umegusa upande wao wanakanyagana kama ng'ombe.
 
watanzania wengi vyeti magumashi ndio maana unasikia sijui kubadili majina mengine waliapa mahakamani kwa nini wawe wao tuu huko mahamani..
 
Hivi wale repeaters wa shule za msingi wanakuwa kwenye category gani kisheria?Hawajafoji vyeti, walifaulu kwa akili zao ila kwa majina yasiyo yao.Hawa tunawaweka kundi gani?Nawakumbuka sana nilikuwa nashika namba 1 darasani ilipofika la darasa la 6 wakaletwa watatu nikaanza kushika namba 4.

hao wapo katika kundi la akina mwigulu nchemba.. alichukua jina la mtu akalitendea haki.. kafaulu kila kitu.
 
Huyu cheti chake hakina athari sana kwa Wananchi maana wananchi wenyewe wanamkubali.Tatizo lipo kwa Daudi Bashite ambaye amekuwa mstari wa mbele kuita wenzake Vilaza.
Huyu hata akijiita Kalubandika Kakufi yeye bado ni chaguo la watu wa jimbo lake kwa sasa hana impact yoyote ila atakapokua mtumishi wa serikali lazima tumjadili
 
Hawa jamaa inaoneka wanapenda surname ya HECHE. Hata mimi kuna mdg wke nilisoma nae Primary alkua anaitwa SUGUTA CHARLES ila tulipofika Sec alibadili akajiita DAVID HECHE. Nadhani hata yeye alibadili tu.
 
MBONA MNACHEZEWA AKILI NA MPUMBAVU MMOJA ......HANA MATOKEO YA MUSOMA TECH YA WEGESA....HANA DETAILS ZA JOHN HECHE...ILA KAAMUA KUTUFANYA WOTE NI WAPUMBAFU KAMA YEYE......ACHANENI NA HUYU MPUMBAFU
 
Hii muvi inafika patamu sasa naona kuna mmoja humu anataka kuchezea remote atatoka nje. Hebu tuache tushuhudie hii muvi hadi mwisho bashite ataibuka shujaa au ndio itakuwa jina la makondakta litakuwa limefika mwisho wake kusisika kwenye tasnia hii
 
Kiukweli hapa ndio penye maajabu

- Kwanini aitwe JOHN HECHE wakati tumesoma wote Musoma Tech. ukiitwa WEGESA CHARLES ?

---------------
---------
Nasubiri kama atakuja kukanusha na kubisha nimwage hapa hapa data kamili - Wegesa Charles is my Homeboy, School & ClassMate
Hon. John Wegesa Heche


Member Type : Constituent Member

Constituent : Tarime Vijijini

Political Party : CHADEMA

Phone : +255786261668

P.O Box : -

Email Address : j.heche@bunge.go.tz

Date of Birth : 1981-07-14



Education History :


School Name/Location Course/Degree/Award From To Level
St. Augustine University Degree 2006 2009 Bachelor
Bunda -TTC Diploma 2004 2006 Diploma
Musoma Alliance ACSEE 2001 2003 Secondary School
Bulima CSEE 1997 2000 Secondary School
Nyamaharaga CPEE 1989 1996 Primary School


Employment History :


Company/Institution Position From To
Ministry of Education Secondary Teacher 2006 2009


Political Experience :


Political Party Position From To
The Parliament of Tanzania Member of the Parliament 2015 2020
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Chairman- Youth Wing (BAVICHA) 2011 2014
Tarime District Councilor 2008 2010
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Secretary- SAUT -Branch 2006 2009
 
LETE HIVYO ULIVYO NAVYO TUMUONGEZE HECHE HAPA PIA KAMA HUNA OMBA RADHI FASTA
 
Ndugu wanaJF,

Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

Nawatakia jioni njema.
 
Umekosea Wegesa ni jina la kike so acha utoto na Umbea
Heche ndio jina lake kwa watu tunaomjua toka anazaliwa
 
Back
Top Bottom