Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Jan 15, 2013.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2013
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 145
  Ndugu wanaJF,

  Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

  Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

  Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

  Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

  Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

  Sasa nije kwa John Heche Suguta:
  Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

  Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

  Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

  John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

  Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

  Nawatakia jioni njema.

   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2013
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,002
  Likes Received: 6,110
  Trophy Points: 280
  mhuuuuuuuuuuuuum
   
 3. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2013
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,107
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Good safi sana kwa kutolea ufafanuzi
   
 4. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2013
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  asante kurekebisha upepo
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2013
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,027
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Juliana bwana.
   
 6. Tangopori

  Tangopori JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2013
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Eka deny mbee!
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2013
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,000
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu kwa huu ufafanuzi wako uliosimama kama ule wa Dr Slaa kuhusu MOU
   
 8. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2013
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 480
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Safi HOJA INAJIBIWA KWA HOJA
   
 9. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2013
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Juliana Shoza sijui Shonza ni SISIMIZI kama KAFULILA NA ZITTO KABWE!Wana BAVICHA NA CHADEMA ngalawa mwendo wake huwa ni wa kuyumba yumba tu,lakini safari itamalizika salama tu!
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2013
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,231
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna ubaya mie kuuliza iko swali nataka kujua kama kuna majina ya kikristo.
   
 11. Rapherl

  Rapherl JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2013
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 3,300
  Likes Received: 1,406
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa umewaacha uchi lazima wachutame
   
 12. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2013
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Pongezi kamanda Maranya kwa ufafanuzi murua.
  Nina hakika aliyepata kushikilia nafasi ya Makamu Mwenyekiti BAVICHA sasa ameinamisha kichwa kwa ukurupukaji wake.
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2013
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,647
  Likes Received: 21,507
  Trophy Points: 280
  Huyu bundi wa CHADEMA si mchezo....
   
 14. Dr. Ndimu

  Dr. Ndimu JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2013
  Joined: Oct 30, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani we mwita ni nan ake wegesa, kwanin yy aloiba majina asije hapa kufafanua? Mwaka wenu huu kwakweli.
   
 15. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio maana unamuona RITZ anaanza kutoka kwenye mada nakuingiza udini mara majina ya kikristo,hoja hujibiwa kwa hoja.
   
 16. N

  Ndikwega JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2013
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 4,392
  Likes Received: 1,748
  Trophy Points: 280
  yani kweli huu mwaka wetu tumekamata vibaya masaliz yani hayafurukutinkila yakitaka kuchomoza ngumi ya jicho,mara pua, mara mdomo aa pole sn pm7, ee leteni uwongo mwingine wajina umefeli
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2013
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Tunashukuru Mkuu Mwita Maranya kwa ufafanuzi makini na wa hekima kubwa.

  Masalia na Shetani wao,Chadema na Mungu wetu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2013
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 17,549
  Likes Received: 8,295
  Trophy Points: 280
  wewe ndio kichwa nazi kabisa, wamekutajia na ndugu zake ili kukuridhisha lakini bado huelewi..kama unaweza tuambie huyo mwenye jina yuko wapi hadi akubali kuporwa jina ngazi ya chuo.!
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 42,867
  Likes Received: 11,273
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka maneno ya shonza ya baki hila ya mwita yaondoke!

   
 20. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Miafrika ndivyo tulivyo by NYANI NGABU/
   
Loading...