Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Kiukweli hapa ndio penye maajabu

- Kwanini aitwe JOHN HECHE wakati tumesoma wote Musoma Tech. ukiitwa WEGESA CHARLES ?

---------------
---------
Nasubiri kama atakuja kukanusha na kubisha nimwage hapa hapa data kamili - Wegesa Charles is my Homeboy, School & ClassMate


mkuu, unaweza onesha kama aliwahi kufeli katika masomo yake?

Maana wizi wa vyeti na kubadili majina mara nyingi sana hujitokeza kwa watu //vijana waliofeli.

Asante.
 
Hivi wale repeaters wa shule za msingi wanakuwa kwenye category gani kisheria?Hawajafoji vyeti, walifaulu kwa akili zao ila kwa majina yasiyo yao.Hawa tunawaweka kundi gani?Nawakumbuka sana nilikuwa nashika namba 1 darasani ilipofika la darasa la 6 wakaletwa watatu nikaanza kushika namba 4.


Kwa kifupi wewe haukuwa na akili kama ulivyokuwa unajiona.
Wewe Ulikuwa ni chongo uliyekuwa unaongoza kwenye nchi ya vipofu.
 
Kwa kifupi wewe haukuwa na akili kama ulivyokuwa unajiona.
Wewe Ulikuwa ni chongo uliyekuwa unaongoza kwenye nchi ya vipofu.
Inawezekana unachokisemani kweli lakini sikuwa kilaza kiasi hicho.unajua kilichokea nini kwenye makeo ya darasa la saba?Mungu alikuwa na mimi.Nilifaulu mimi na binti mmoja ambaye tulianza naye la kwanza(shule nzima wawili tu enzi hizo),wale repeaters marks hazikutosha nikapenya hadi O-level,A level comb inayoanza na P, nikapiga nikatoboa mlimani UDSM kozi ya wanaume.Weekend njema
 
Hawa jamaa inaoneka wanapenda surname ya HECHE. Hata mimi kuna mdg wke nilisoma nae Primary alkua anaitwa SUGUTA CHARLES ila tulipofika Sec alibadili akajiita DAVID HECHE. Nadhani hata yeye alibadili tu.

Umesema vyema.

Hasa, jambo hili kwa wakurya ni kwamba wao mara nyingi hawawapi watoto majina ya kikristo (wanapokuwa wadogo) basi hao watoto wakianza kwenda au kujiunga na Kanisa Fulani hapo ndiyo watabadili Yale majina yao ya utotoni na mwisho inaonekana wana majina tofauti.
Ila ukuryani najua hiyo ni kawaida kuwa na majina mawili au zaidi tofauti mfano: majina ya nyumbani, kitaani hadi shuleni.
 
Inawezekana unachokisemani kweli lakini sikuwa kilaza kiasi hicho.unajua kilichokea nini kwenye makeo ya darasa la saba?Mungu alikuwa na mimi.Nilifaulu mimi na binti mmoja ambaye tulianza naye la kwanza(shule nzima wawili tu enzi hizo),wale repeaters marks hazikutosha nikapenya hadi O-level,A level comb inayoanza na P, nikapiga nikatoboa mlimani UDSM kozi ya wanaume.Weekend njema

Umejibu vyema.

Haya, rekebisha usemi wako hakuna kozi ya wanaume maana katika kozi zote naona wapo wanawake pia wana taaluma za hiyo kozi inayoanzia na "P" tena wengi tu.
Mfano, wahandisi, madaktari, marubani, maprofesa n.k.kwa hiyo ukisema kozi ya wanaume unakuwa unakosea.

Usioneshe tabia ya kutokuwathamini wanawake ukinzingatia mzazi wako mmoja ni mwanamke na mwezi huu wa 3 ni wa kuadhimisha siku hiyo ya wanawake duniani itakuwa tarehe 8 March.

Weekend njema.
 
Ndugu wanaJF,

Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

Nawatakia jioni njema.

Sawa!
 
Hawa majamaa wapo tayari kufanya kila aina ya maigizo ili upepo wa kukomalia vyeti vya BASHITE upite lakini wapi. All in all Kamanda is back......hapa issue ya Bahizoooo ikiendelezwa tunaweza shangaa Saa 8 akaonekana.
 
Nime bahatika kuwa na mke wa kikurya kunakitu ameniambia cha kwanza wakurya wanaongoza kwa kugushi miaka pili wanatumia vyeti vya ndugu zao vya form two ndio maana mtu moja anakua na majina mawili family moja inawatu wawili wenye majina sawa either mmoja ataenda jeshini or mwengine ataenda kwenye taasi nyingine


Mke wako alikupima / anakupima akili aone wewe unazo akili ama ni akili za kushikiwa!
Be careful, wakurya wako makini sana.
 
Matumizi ya majina mawili tofauti kwa John Heche na Wegesa Charles bado ni ukakasi.
Hoja ya Bashite haiwezi kuzimwa kizembe namna hii au kumpa ubunge mwalimu Salma Kikwete ili mtuhamishe kwenye mjadala, hii mbinu imeshindwa hata kabla haijaanza.
 
Matumizi ya majina mawili tofauti kwa John Heche na Wegesa Charles bado ni ukakasi.
63dd58477264bdda3a31415cb6ed5233.jpg
 
Safi sana kwa ufafanuzi murua kabisa hapa, discussion closed, bado yule Bashite aje amwage kwa ufupi sana tutamuelewa tu wala asiogope kabisaa
 
Nime bahatika kuwa na mke wa kikurya kunakitu ameniambia cha kwanza wakurya wanaongoza kwa kugushi miaka pili wanatumia vyeti vya ndugu zao vya form two ndio maana mtu moja anakua na majina mawili family moja inawatu wawili wenye majina sawa either mmoja ataenda jeshini or mwengine ataenda kwenye taasi nyingine
Umekubali kudanganywa na mke wako...daah angalia kaka.,isije ikawa hata watoto umepew tu uwalee...ni angalizo tu
 
Back
Top Bottom