Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Kiukweli hapa ndio penye maajabu

- Kwanini aitwe JOHN HECHE wakati tumesoma wote Musoma Tech. ukiitwa WEGESA CHARLES ?

---------------
---------
Nasubiri kama atakuja kukanusha na kubisha nimwage hapa hapa data kamili - Wegesa Charles is my Homeboy, School & ClassMate
Anayekueleza ya wengine atawaeleza wengine ya kwako
 
Kiukweli hapa ndio penye maajabu

- Kwanini aitwe JOHN HECHE wakati tumesoma wote Musoma Tech. ukiitwa WEGESA CHARLES ?

---------------
---------
Nasubiri kama atakuja kukanusha na kubisha nimwage hapa hapa data kamili - Wegesa Charles is my Homeboy, School & ClassMate
Ndugu wanaJF,

Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

Nawatakia jioni njema.
 
Kiukweli hapa ndio penye maajabu

- Kwanini aitwe JOHN HECHE wakati tumesoma wote Musoma Tech. ukiitwa WEGESA CHARLES ?

---------------
---------
Nasubiri kama atakuja kukanusha na kubisha nimwage hapa hapa data kamili - Wegesa Charles is my Homeboy, School & ClassMate
Mmoja mmoja ndo mpango, sahizi tuna mhudumia Bashite kwanza tukimaliza tuta ruhusi mwingine aingie.
 
Timu zimejiandaa kubadili upepo wa bashite.... Ila katika hili haina jinsi... Mkulu akitaka arudishe imani ya watu njia pekee ni kuachana Na bashite la sivyo akizidi Kung'ang'ania atatengeneza makovu makubwa Sana kwenye mioyo ya watu
 
Safi Sana Na bashite aje sasa zamu yake atutolee ufafanuzi

Karibu bwana bashite
 
Hahaha mh. Shonza pole sana. Mshauri Bashite naye atoe ufafanuzi mujarab kama huu.
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Mama bashite alitaga kwenye maswali mwambie daudi alete vyeti vyake bado tunahakiki vyeti aache maneno alete vyeti
 
duuh. kumbe kutoa ufafanuzi wa majina na shule alizosoma mtu ni rahisi hivi. safi sana akina suguta.
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Sasa daudi si atoke naye au haoni wenzie wanavofanya
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Hapa waanze kutoa vyeti vya DAUD A BASHITE kwanza sio kutafuta namna ya kulifutika hili jambo kwenye uvungu wa kashfa na stori za hapa na pale hata kama ni heche naye tutamfuatilia ila kwa sasa DAUD BASHITE ndiye anayehitajika
 
Back
Top Bottom