UDSM mwaka huu kuna nini?

UDSM mwaka huu kuna nini?

Tangu kupata uhuru sidhani Kama Kuna changes za maana zimefanyika kwenye mfumo wa elimu.

Anyways sio kesi kwa mwaka huu ufaulu ni mkubwa na hio sio UDSM tu hata MZUMBE kwa upande wa LAW wamechukua 3-5, wengine wote wamebehuliwa nje

Ajaribu kuapply na mburahati😂 ,(jokes)
😂😂😂😂
 
Habarini wana jukwaa.

Nimeona nije hapa jukwaani nitoe hili jambo, huenda nitapata ufafanuzi.

Nimekuwa nikikutana na malalamiko ya wanafunzi waliomaliza form 6 mwaka huu, wanaotarajia kujiunga na vyuo hivi karibuni. Wengi wao wanalalamika kuwa kila waombapo nafasi UDSM wanakataliwa, na wengine wanadiriki kusema kuwa vigezo sahihi wamekidhi kulingana takwa husika.

Sio mtaani wala mtandaoni ni malalamiko juu ya vijana na mabinti wanaotarajia kujiunga na Elimu ya Juu. Kuhusu Kukataliwa kuwa admitted hapo UDSM.

kuna huyu jirani yangu, yeye alisoma Ilboru Sec mchepuo wa PCM, kapata 1 ya 5, kachagua Udsm Course ya Civil Engineering, kakosa, bas analalama kila muda, hapa hata mie nimeshanga, huyu vigezo amekidhi kabisa, au labda huu mwaka 1 ya 3 na 4 ziko nyingi, hivyo inafanya wenye 5 na kuendelea wakose nafasi hapo COET?

Na Malalamiko ni kwa kila kada wanalalama mno, huku wakiwa na 1 zao nzuri, shida nn? Au utaratibu umebadilika hapo siku hizi? Kulikoniii?

Najua hapa kuna wafanyakazi, wana taaluma, wahadhiri, kutoka hapo UDSM, hebu mje mtoe ufafanuzi kutuondolea sintofahamu hii, maana huku uraiani hali ni mbaya watoto wanavurugwa vibaya, wakati ndoto zao ni kuwa hapo Mlimani main campus.

Tujuzweee kulikoniiiii?
Kwani ana kadi ya CCM?🤣
 
University of Dar es salaam home of intellectuals
Ilikuwa ni zamani. BTW kuna kitu watanzania tunashindwa kuunganisha kwa sababu hata elimu yetu ni ya kukariri. Ni hivi: huwezi kuendesha nchi kama wanavyofanya CCM halafu utegemee mambo yajiendee vizuri. Haya malalamiko yote ni matokeo ya uongozi mbovu, usio na vision, unaotegemea njia za kitapeli na mabavu kubaki kwenye madaraka japo umeshindwa. Na mbaya zaidi ni kuwa hata hao vijana wanaolalamika wengi hawaioni hii shida, wanadhani tatizo ni uongozi wa chuo kikuu. Bila kuiondoa CCM hakuna kitakachobalika ila mambo yatazidi kuharibika.
 
Cocastic kumbe ukipigwa mboko vizuri unamwaga pwenti point pwenti.
Hapa nakupa misumari yako, maua badae😁
Babuu

Afu mbona sijawahi kuwa kilaza, toka O level shule ya bweni (single sex), Advance Special School, Chuo UDSM hapo COET.

Sema nn sometimes najichetua ili maisha ya flow vile yanataka kuwa.
😂😂😂😂😂😂
 
Kwani UDSM si huwa wanatoa sababu ya kwanini haujawa selected?
Najua hivyo pia, nilimuuliza huyu jirani anasema eti haoni sababu, Nikamuambia au hiyo course tayari idadi imekamilika, anasema hajaarifiwa hivyo.

Nikasema khee labda kuna mambo siyafamu siku hizi. Niwaachie wenyewe.
 
Competition ni kubwa but form six leavers wengi wanaotaka engineering dit ni bora zaidi kuliko udsm .

Kwa sababu udsm wanatao bachelor of science in engineering , alafu dit wanatoa bachelor of engineering kwa hiyo wangetakiwa kuelewa hicho

Pia Udsm kwa tanzania hii siyo chuo bora kwa engineering labda ni chuo bora kwa mazingira mazuri.

Ni chuo kikuu kikongwe hapa bongo lakn siyo chuo bora kwa engineering .

Kama kuna kuna mwenye hoja alete hapa hoja zake kutetea udsm
Mkuu hayo mambo ya kubishana kuhusu chuo inanesha wewe bado uko unasoma chuo (dit) au ndio umemaliza form6. Maliza udsm maliza dit alafu Njoo huku mtaani tukupe site usimamie au mradi u design, hapo ndio utajua kubishania chuo ni utoto wa hali ya juu.
 
Dunia imebadilika sasa. Pengine qualification pekee sio kigezo. Labda aongee watu vizuri.
 
Back
Top Bottom