UDSM mwaka huu kuna nini?

UDSM mwaka huu kuna nini?

Kuna Dgo O level ana One ya 8 Advance ana ONE ya 6 PCB Hadi sasa hajapata chuo chochote!!
PCB one ya 5 mpaka 9 aliyeweka first choice doctor of medicine chuo cha MUHAS,kakosa chuo.Kwa sababu MUHAS wanaangalia first choice tu,other choices wanakuambia kabisa the selection wasn't runned.Wengi wameliwa kichwa hadi UDOM.
 
Nani kakudanganya? Vipanga wengi, hukimbilia Civil, Electrical, na Mechanical, Telecommunications, petroleum kuna kipindi zilikua na soko, kwa sasa wengi wao wanalia,
Labda hiyo Biomedical.
Civil, vipanga wachache huikimbilia,vipanga wengi wa PCM hukimbilia hizo zingine ulizozitaja, pia kati ya kozi ulizozitaja hapo, civil ndo ina admission capacity kubwa pale udsm.
 
Civil, vipanga wachache huikimbilia,vipanga wengi wa PCM hukimbilia hizo zingine ulizozitaja, pia kati ya kozi ulizozitaja hapo, civil ndo ina admission capacity kubwa pale udsm.
Najua kuhusu hili, ndo maana nikashangaa jirani angu kukosa CE, wakati pale UD, COET hii course ndo inachukua wanafunzi wengi
 
PCB one ya 5 mpaka 9 aliyeweka first choice doctor of medicine chuo cha MUHAS,kakosa chuo.Kwa sababu MUHAS wanaangalia first choice tu,other choices wanakuambia kabisa the selection wasn't runned.Wengi wameliwa kichwa hadi UDOM.
Kwanza km mtu una 1 kuanzia ya 5 had 9 kwa PCB, kwann utake MUHAS? tena km MD, ndo kabisa usiguse, labda DDS na Pharm, na nyingine.

Tatizo la wanafunzi wanataka vyuo vikubwa huku vigezo extra hawana.
Polee yao.
 
Si wanajifanya vichwangumu,wanadhani MUHAS chuo cha baba zao.Na pia wanaona hizo nyingine sio course nzuri.Wacha wakose.
 
Kuna chuo kikuu halafu kuna Chuo kikuu kikuu cha Tz. Watu wanabisha ila kuna raha fulani kuchaguliwa UDSM.
NI chuo cha ndoto za wanafunzi wengi tukiwa sendokari.
Ni chuo maarufu.

Watu hawajui vyuo vingine.

Mtu mpaka anafika kidato cha sita hajui kuna vyuo kibao, hilo ndio tatizo.

Akiulizwa unataka kwenda kusomea nini yeye anachagua chuo badala ya kozi ya kusoma.
 
Ni chuo maarufu.

Watu hawajui vyuo vingine.

Mtu mpaka anafika kidato cha sita hajui kuna vyuo kibao, hilo ndio tatizo.

Akiulizwa unataka kwenda kusomea nini yeye anachagua chuo badala ya kozi ya kusoma.
Kwa zamani ni kweli kilikuwa chuo maarufu kiasi vingine vizifahamike kwa urahisi. Lakini siku hizi vyuo vingi vimekuwa famous kwa watu wengi.
Still UDSM inajibeba na umaarufu wake wa kitambo kwamba ni chuo prestigeous nchini, inabaki kuwa dream ya kila mtu kusoma hapo.
 
Sio kweli kwamba UDSM ni dream ya kila mtu. UDSM kwa washamba washamba wa elimu ndio dream
 
Kwanza km mtu una 1 kuanzia ya 5 had 9 kwa PCB, kwann utake MUHAS? tena km MD, ndo kabisa usiguse, labda DDS na Pharm, na nyingine.

Tatizo la wanafunzi wanataka vyuo vikubwa huku vigezo extra hawana.
Polee yao.
Dah kweli competition ni kubwa 1 ya 5 mpaka 9 anapitia hayo
 
Kwa zamani ni kweli kilikuwa chuo maarufu kiasi vingine vizifahamike kwa urahisi. Lakini siku hizi vyuo vingi vimekuwa famous kwa watu wengi.
Still UDSM inajibeba na umaarufu wake wa kitambo kwamba ni chuo prestigeous nchini, inabaki kuwa dream ya kila mtu kusoma hapo.
Mkuu UDSm bado ni chuo maarufu na kinatoa watu wengi mno.

Walio makazini miaka hii wengi ni zao la hicho chuo, umaarufu wake haufutiki kirahisi.
Pia bado ni chuo bora nchini.
 
Chuo cha taifa bhana
Mimi nilivyoona na Division II ya 10 yangu hata sikuapply licha ya wazazi kunilazimisha. Nilijua tu pale wanaenda vipanga tu 😂😂😂
Nikaomba zangu Mechanical Engineering DIT, ATC, MUST na NIT. Hapo DIT wamenitema vingine vimenikubali. Finally nimechagua zangu tu MUST nimetulia.

Hapo niliosoma nao kila mtu analalamikia UDSM, na niliwaonya sana kuwa elfu 10 zenu zinaenda bure. Watu wana Div 1 ya 6 huko wametemwa. Usicheze na chuo cha taifa wewe 😂😂😂
 
Habarini wana jukwaa.

Nimeona nije hapa jukwaani nitoe hili jambo, huenda nitapata ufafanuzi.

Nimekuwa nikikutana na malalamiko ya wanafunzi waliomaliza form 6 mwaka huu, wanaotarajia kujiunga na vyuo hivi karibuni. Wengi wao wanalalamika kuwa kila waombapo nafasi UDSM wanakataliwa, na wengine wanadiriki kusema kuwa vigezo sahihi wamekidhi kulingana takwa husika.

Sio mtaani wala mtandaoni ni malalamiko juu ya vijana na mabinti wanaotarajia kujiunga na Elimu ya Juu. Kuhusu Kukataliwa kuwa admitted hapo UDSM.

kuna huyu jirani yangu, yeye alisoma Ilboru Sec mchepuo wa PCM, kapata 1 ya 5, kachagua Udsm Course ya Civil Engineering, kakosa, bas analalama kila muda, hapa hata mie nimeshanga, huyu vigezo amekidhi kabisa, au labda huu mwaka 1 ya 3 na 4 ziko nyingi, hivyo inafanya wenye 5 na kuendelea wakose nafasi hapo COET?

Na Malalamiko ni kwa kila kada wanalalama mno, huku wakiwa na 1 zao nzuri, shida nn? Au utaratibu umebadilika hapo siku hizi? Kulikoniii?

Najua hapa kuna wafanyakazi, wana taaluma, wahadhiri, kutoka hapo UDSM, hebu mje mtoe ufafanuzi kutuondolea sintofahamu hii, maana huku uraiani hali ni mbaya watoto wanavurugwa vibaya, wakati ndoto zao ni kuwa hapo Mlimani main campus.

Tujuzweee kulikoniiiii?
Performance ya wahitimu wa siku hizi ni unrealistically rosy. Chuo hata kikiamua kuwa na darasa la watu wenye 1 ya pt 3 tu, darasa litajaa. Kiuhalisia, wengi wa wale wanaopata division one leo ni equivalent ya wale waliokuwa wanapata division II na III kabla ya kizazi cha millennials.
 
Back
Top Bottom