UDSM mwaka huu kuna nini?

UDSM mwaka huu kuna nini?

Habarini wana jukwaa.

Nimeona nije hapa jukwaani nitoe hili jambo, huenda nitapata ufafanuzi.

Nimekuwa nikikutana na malalamiko ya wanafunzi waliomaliza form 6 mwaka huu, wanaotarajia kujiunga na vyuo hivi karibuni. Wengi wao wanalalamika kuwa kila waombapo nafasi UDSM wanakataliwa, na wengine wanadiriki kusema kuwa vigezo sahihi wamekidhi kulingana takwa husika.

Sio mtaani wala mtandaoni ni malalamiko juu ya vijana na mabinti wanaotarajia kujiunga na Elimu ya Juu. Kuhusu Kukataliwa kuwa admitted hapo UDSM.

kuna huyu jirani yangu, yeye alisoma Ilboru Sec mchepuo wa PCM, kapata 1 ya 5, kachagua Udsm Course ya Civil Engineering, kakosa, bas analalama kila muda, hapa hata mie nimeshanga, huyu vigezo amekidhi kabisa, au labda huu mwaka 1 ya 3 na 4 ziko nyingi, hivyo inafanya wenye 5 na kuendelea wakose nafasi hapo COET?

Na Malalamiko ni kwa kila kada wanalalama mno, huku wakiwa na 1 zao nzuri, shida nn? Au utaratibu umebadilika hapo siku hizi? Kulikoniii?

Najua hapa kuna wafanyakazi, wana taaluma, wahadhiri, kutoka hapo UDSM, hebu mje mtoe ufafanuzi kutuondolea sintofahamu hii, maana huku uraiani hali ni mbaya watoto wanavurugwa vibaya, wakati ndoto zao ni kuwa hapo Mlimani main campus.

Tujuzweee kulikoniiiii?
Competition kaka. 1 point 5 kwa PCM ni division 2 ya point kadhaa miaka ya 90.
 
H
PCB one ya 5 mpaka 9 aliyeweka first choice doctor of medicine chuo cha MUHAS,kakosa chuo.Kwa sababu MUHAS wanaangalia first choice tu,other choices wanakuambia kabisa the selection wasn't runned.Wengi wameliwa kichwa hadi UDOM.
HUjAeleweka hapa Mkuu rudia tena!!

Nyie sio Wanafunzi wa Mchonde kweli!?
 
H

HUjAeleweka hapa Mkuu rudia tena!!

Nyie sio Wanafunzi wa Mchonde kweli!?
hapana mkuu,me nimemaliza form six 1939.

ANYWAYS,Ni kwamba kwenye choices za kozi kwa vyuo vya MUHAS na UDOM,kwa mwaka huu wameangalia first choice peke yake,mfano mwanafunzi aliyepata one ya 6 akaweka first choice yake doctor of medicine then second choice akaweka nursing,huyu kwa mwaka huu amekosa chuo kwa sababu MD wameshajaa tayari 235 students pale muhas.
 
H

HUjAeleweka hapa Mkuu rudia tena!!
in short kwa mwanafunzi wa PCB aliyepata chuo mwaka huu wapo wa aina tatu
1.wanafunzi vipanga waliopata 3,4 na 5 baadhi

2.wanafunzi waliopata 7 mpaka 9,ila hawakung'ang'ania courses zenye competition kama doctor of medicine,DDS,pharmacy kwenye vyuo vikubwa kama MUHAS .

3.wanafunzi wa PCB waliokimbia course za afya na kuchagua computer sciences,accountancy.
 
Tuachane na hayo, nimemuona Anko T kavaa dera aisee😭

Hivi Anko T na noel nani ana afadhali kidogo?😭😅
 
in short kwa mwanafunzi wa PCB aliyepata chuo mwaka huu wapo wa aina tatu
1.wanafunzi vipanga waliopata 3,4 na 5 baadhi

2.wanafunzi waliopata 7 mpaka 9,ila hawakung'ang'ania courses zenye competition kama doctor of medicine,DDS,pharmacy kwenye vyuo vikubwa kama MUHAS .

3.wanafunzi wa PCB waliokimbia course za afya na kuchagua computer sciences,accountancy.
Nimekusomz mkuu
 
Back
Top Bottom