Uchumi wako unaweza kununua kitu gani unachojisikia?

Screenshot_20231210_104609_WhatsApp.jpg
 
Nilikuwa napita pita zangu huko mtandaoni,nikakutana na tangazo la wauza viwanja (madalali).

Nilisikitika sana baada ya kusoma like tangazo. Nikasema Bongo Kuna watu Wana uchumi ambao wanaweza kununua kiwanja chochote na mahali popote. Na Hawa siyo kina Mo na Bahresa,ni watu tu ambao wapo low key ila ni wanene(mafogo/matajiri).

Nikijiangalia, najiona Sina uwezo wa kununua kiwanja mahali popote pale ninapotaka,Wala kujenga nyumba yeyote ninayoitaka kwa sababu uchumi wangu upo limited.

Siku nimeenda Kidimbwi nikagundua kumbe Mimi Bado sana. Yani hata kinywaji (pombe) Sina uwezo wa kununua pombe yoyote ninayojisikia kununua. Kwa sababu nilikutana na pombe za hadi milioni mbili,alafu chupa Moja tu jamani!! Mbaya zaidi Kuna watu wananunua bila kumuuliza uliza bei Wala kujikuna kichwa.

Kuna watu Wana uchumi wa kwenda mahali popote pale duniani kula Bata.

Mwingine ana uwezo/uchumi wa kula chochote anachojisikia na muda waowote akitaka.

Mwingine ana uwezo wa kununua gari lolote linalouzwa hapa duniani,wakati Kuna kina sisi hata Toyota Passo inakuwa kipengere.

Anyways,turudi kwenye swali;

Uchumi wako una nguvu ya kufanya nini unachojisikia?
mtu kusema huwezi kununua kiwanja mahali popote hiyo ni lame excuse ambayo haina mashiko kuna mahali huko mbwinde hata elfu ishirini unapata kiwanja, labda kama unataka vya mjini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom