Nizingatie nini msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka?

Jugado

JF-Expert Member
Oct 28, 2021
1,449
3,135
Utangulizi

Msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka huwa na heka heka nyingi na watu hupendelea kufurahia kula na kusherekea walichopanda Kwa mwaka mzima. Hata hivyo Kwa kua ni msimu wenye matukio sio kidogo Kwa sababu ya asili ya shunguli nyingi ni vyema kuzingatia mambo kadhaa.

Mambo ya jumla na usalama

1. Epuka kulewa sana (kupitiliza). Kama ni lazima ulewe sana fanya hivyo nyumbani kwako sio kwenye mtoko. Huko kwenye mtoko kuna matukio sana.

2. Kama una familia hakikisha unasherekea na familia yako, ikiwezekana nyumbani.

3. Epuka sehemu za mikusanyiko mikubwa.

4. Watoto wasitoke wenyewe. Wawe kwenye uangalizi Kila dakika.

5. Kama unatoka usitoke mwenyewe. Pia epuka kuonekana na cash nyingi. Watu wabaya hupenda kuwadhuru watu wenye cash.

6. Kama uchumi sio mbaya kumbuka kutuma chochote nyumbani Kwa wazazi wako na ndugu ambao hawamudu kununua mahitaji muhimu ya sikukuu. Inaweza kua hata laki moja tu.

Kujizuia Kwa ajili ya 'Njanuari'

1. Kama uchumi wako sio stable sana yaani wasubiri mshahara, au kipato cha kuunga hakikisha unajiandaa Kwa January.

Mimi hununua gas ya ziada, mkaa gunia, maharage, mchele wa kutosha, unga wa kutosha na mafuta na hata elf 50 iweke mahali itakufaa sana. Maana Kwa kawaida January hakuna wa kumkimbilia.

2. Kama una Kodi think about it.

3. Kurudisha watoto shule. Kama una maokoto lipa ada December hii.

5. Kwa ujumla tusile bata as if tunakufa December. Kila kitu kiwe na kiasi.

6. Kama uchumi haupo poa sana jizuie kusafiri kwenda nyumbani.

Hitimisho

Tunachukua tahadhari za muhimu ili kinachoweza kuzuilika kizuilike. Cha kutokea kisiwe Kwa ajili ya uzembe.

ONGEZEA MENGINE
 
Shukrani mkuu, atakayezingatia hii thread yako basi manufaa yake atayaona baada ya January 2024 panapo majaaliwa , niwatakie maandalizi mema ya sikukuu za mwisho wa mwaka WanaJF wenzangu na maandalizi na mema ya kuupokea mwaka mpya wa 2024 panapo majaaliwa ya mwenyenzi Mungu.
 
Shukrani mkuu, atakayezingatia hii thread yako basi manufaa yake atayaona baada ya January 2024 panapo majaaliwa , niwatakie maandalizi mema ya sikukuu za mwisho wa mwaka WanaJF wenzangu na maandalizi na mema ya kuupokea mwaka mpya wa 2024 panapo majaaliwa ya mwenyenzi Mungu.
Asante sana mdau
 
Back
Top Bottom