Muda gani ni sahihi kumshambulia adui?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hakuna asiye na adui. Na hakuna ambaye sio adui kwa mwingine. Yaani wewe unavyojiona hapo kuna mtu anakuona ni adui yake. Halikadhalika wapo unaowaona ni maadui.

Unaweza kuwa na maadui kwa Wema wako. Kama vile unavyoweza kuwa na maadui kwa ubaya wako. Adui ni adui bila kujali sababu za uadui. Unaweza kuwa na uadui unaosababishwa na tofauti za kifikra na kimtazamo. Pia wapo unaowaona màadui kwa sababu ya mitazamo yao dhidi yako haipatani.

Wapo maadui wanaotokana na maslahi ya kiuchumi. Yaani unapoingiliana laini ya uchumi ya mtu mwingine tayari mnakuwa màadui. Au mtu anapoingilia laini yako ya uchumi automatically mnaingia katika ligi ya uadui. Elewa, ilimradi unaishi basi uadui hauepukiki.

Sasa kuna ukweli uadui ambao mpo katika vita ya moja kwa moja. Vita ya wazi na wala sio ile vita baridi au vita ya ndani kwa ndani. Yaani mnachukiana au unamchukia fulani lakini fulani hajui kama wewe ni adui yake. Au kuna mtu anakuchukia na ni adui yako mkubwa lakini hujui kabisa.

Adui anaweza kuwa yeyote, lakini adui mbaya ni yule anayekutawala;
i) Anayekutawala kihisia, huyu anaweza kuwa mkeo, mumeo, ndugu, wazazi, Wakwe au rafiki.
Ii. Anayekutawala kiuchumi, huyu anaweza kuwa Boss au mwijiri wako.
iii) Anayekutawala kisiasa. Hapa tunazungumzia serikali. Inaweza kuwa adui yako kwa kukusababishia maisha magumu.
iv) Anayekutawala Kiroho. Hawa ni wachungaji, masheeikhe, maimamu, Askofu, waganga wa kienyeji. N.k

Mbinu za kujua adui zako

Taikon Master kama Mastermind, Multiplayer, Game changer na Mtibeli halisi ninakupa mbinu chache za kujua maadui zako ili uweze kuishi kwa Amani;

1. Yeyote anayetaka umuamini na umuone mwema.
Mtu yeyote anayelazimisha umuamini, anajifanya mwema kwako lakini kwa wengine sio mwaminifu na sio Mwema huyo ni adui yako. Adui wengi wenye akili huhakikisha anaiteka imani yako. Usimshuku. Imani ni silaha na vazi la adui kumpumbaza anayemuwinda. Uaminifu bandia ni vazi la kondoo. Mtu mwaminifu ni mwaminifu kwa watu wote na sio wewe pekeako. Ukiona mtu anasaliti wengine lakini kwako anajifanya ni mwema. Huyo ni adui yako.

2. Anapenda kukuchimba, kujua mipango na mambo yako. Adui kikawaida hutaka taarifa kutoka kwako ambazo zitamsaidia yeye kwa wakati ujao. Mtu anayekuuliza mambo yako ambayo yeye hahusiani nayo. Huyo uwe mwangalifu naye. Watu kama hawa kuna namna ya kudili nao na kuweza kuwadhibiti. Mtu anauliza mipango yako wakati hajawahi kukusaidia kwa chochote huko nyuma huyo ni adui.

3. Anapenda akifanya mazuri wewe ndio uwe shahidi. Watu wabaya hupendelea ushahidi wakifanya mazuri. Hupenda kujionyesha pale wafanyapo mazuri. Hizo ni sifa za adui. Hufanya hivi kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni kuteka na kupumbaza Watu. Na kujiwekea defence mechanism hapo baadaye.

4. Anapenda kukushauri mara kwa mara hata haujamuomba. Na mara nyingi ukifanikiwa huchomekea kuwa yeye ndiye aliyekushauri ilhali wazo hilo huenda ulikuwa nalo au ulikuwa unafanya kabla hata hajazungumzia jambo hilo kwako. Ukiona upo na mtu hasa rafiki, ndugu au jamaa ambaye anapenda kutoaga ushauri mara kwa mara yaani haiwezi kupita siku au Wiki anakushauri hiki mara kile. Hiyo kwako iwe red alert ya kuwa Mtu huyo ni mbaya. Watu wabaya waliokaribu yako ndio huwa na tabia hizo.

Kikawaida Watu wema, hutoa ushauri kwa nadra hasa pale unapohitajika. Na sio mara kwa mara.

5. Anapenda kuwasema Wengine mambo yao na hawezi kum-face mtu kumwambia Ukweli.
Huyo ni mtu mbaya. Moja ya dalili ya Watu wasaliti ni kukusema nyuma ya mgongo wako au migongo ya Watu wengine. Kikawaida Watu wabaya hawana uwezo wa kum-face mtu moja kwa moja. Ukienda mbugani au vitani sio rahisi adui kuja uso kwa uso. Lazima wajifiche kwenye vichaka wakikuvizia.

Kama anashindwa kuwaambia ukweli watu anaowasema. Hii inamaanisha hata wewe kuna mambo hawezi kukwambia anawaambia wengine. Na mengi ya mambo hayo ni mabaya tu. Watu hawa ndio wazuri wa kukusagia kunguni.

Ni muda gani wa kumshambulia adui?

Watu wengi humshambulia adui na kujikuta wakipoteza pambano au wakishindwa kunufaika na pambano.

1. Jua uwezo wako
Hakikisha unajua uwezo wako kabla ya kumshambulia adui yako. Uwezo namba moja ni uwezo wa Akili. Hakikisha unajua uwezo wako wa akili katika mapambano upo kwa kiwango kipi. Uchumi wako na connection ya walioupande wako.

2. Wajue adui zako
Kabla ya kushambulia hakikisha umewajua maadui wako halisi. Hili litawezekana baada ya kutumia akili kuliko Hisia zako. Hakikisha unajua adui anaakili na upeo kiasi gani. Uchumi wake. Connection zake (watu walioupande wake) Silaha anazozitegemea.

Ni vizuri unapopambana na adui yako ukishajua washirika wake. Ni muhimu kuanza na wale washirika ambao unawaona wananguvu na watakaokupa changamoto. Ukishawa-keep busy au kuwaangamiza washirika tegemeo wa adui yako unaweza kuratibu shambulio kwa adui yako. Hakikisha uhusika wako katika kushambulia washirika wako uwe fiche au bandia. Yaani wewe usihusishwe wala kuonekana.

Ni vizuri kushambulia yale mambo yanayompa furaha adui au mshirika wake. Mfano kile anachojivunia kama uchumi au familia yake yenye furaha na amani basi unaweza anzia hapo. Shambulio la kile anachokipenda, anachojivunia au kinachompa mtu furaha ndio shambulio bora zaidi litakalomtoa adui mchezoni na hata kuwa na nafasi nzuri ya kurejesha mapigo kwa kiwango chenye tija kwake.

3. Angalia kama unaweza Kunufaika na adui yako katika vita yenu
Sio kila adui lazima ummalize papo hapo. Vita unapoianza hakikisha umefanya hesabu ya kila hatua na mashambulio na faida na hasara zake. Mfano, adui yako umemchukulia mke wake kama sehemu ya kisasi chako. Huna sababu ya kumuangamiza wakati unaweza kutumia pesa na kumkomba bila ya yeye kujua. Kuliko umuue alafu uanze kupata shida ya kumlea huyo Mkewe na watoto wake.

Au adui yako akipiga kelele na mitafaruku yenu inasababisha unapata pesa mitandaoni kama unaakaunti YouTube au blog au Facebook au Instagram. Adui wa hivi huwezi kummaliza ilhali vita yenu inakunufaisha wewe kiuchumi.

Hata Mungu na shetani kwa wale wenye kuamini huulizaga mbona Mungu hamuui shetani. Jibu ni kuwa huwezi muua adui ambaye unanufaika kutoka kwake.

Adui huangamizwa moja kwa moja kama analeta madhara makubwa kwako na ikiwa hakipo faida yoyote.

4. Adui unaweza kumtumia kupambana na maadui wako wengine
Adui yako mdogo unaweza kumseti akajikuta katika ugomvi usiomhusu. Yaani akawa katikati yako na adui yako Mkubwa. Kwa hiyo inakuwa vita ya maadui zako. Wanapigana wewe kazi yako ni kuchochea kuni tuu. Ukiona huyu kazidiwa na inakaribia kumalizwa unambusti ili waendelee na vita huku wewe ukitumia nguvu ndogo wao wakizidi kuhenyeka.

5. "Neutralise Karma"
Shambulia ukishakuwa umeuseti wakati. Yaani wakati haupo upande wa adui. Ili kuleta ile kauli ya Dua la kuku halimpati mwewe. Yaani hapo karma isifanye Kazi. Watu wenye akili ni wale wanaojua kui - neutralise Karma. Yaana amekupiga na kukuonea lakini hatalipwa baya lolote. Ndio maana Watu wengi humlalamikia Mungu kwa nini adui zao hawapatwi na mabaya. Taikon ninakuambia kuna kitu kinaitwa "Neutralise Karma" Hii ni nadharia ambayo nimeiandikia kitabu kidogo ambacho hakizidi kurasa mia moja.
Hiki ni kitabu kwa wale walioamua kuwa Watu wabaya.

Taikon Master nimemaliza. Acha nipumzike.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
 
Mtibeli, wanasema kisasi kitamu ni kile unalipiza wakati adui yako kajisahaulisha. Yaani akiwa ktk kilele cha furaha ndipo una piga hapo hapo. Mpaka aje ku recover atakuwa amedhohofika vilivyo.
 
Hapa Tsu nzu "Art of War" na Robert Green "48 Laws of Power" anahusika sana.
Ukikurupuka inaweza kula kwako.
 
Kuna kipndi nilipoteza kila nilicho kichuma , niligundua adui zangu wengi walikua wamama wa umri mkubwa wenye vijana rika langu huko kijijini kwetu sitimbi.
 
Warumi 12:17,19-21
[17]Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
[19]Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
[20]Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
[21]Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
 
Haina haja ya kumshambulia matendo yake yatamashambulia yeye mwenyewe,atajilaani yeye mwenyewe kwa hila zake,wakati huo wewe Mungu atakuwa amekubariki na watashangaa imewezekanaje.Kisasi ni kazi ya Mungu!
 
Mkuu hiyo energy na time unayoitumia kwa maadui ungeweza ku-direct kwenye ku-build prosperity yako.

Na ili ufikie hiyo prosperity NI lazima njiani ukutane na màadui na uwashinde. Ndio hapo umuhimu wa kukabiliana na adui ulipo.

Huwezi fikia mafanikio pasipo njiani kukutana na maadui wanaotaka kukukwamisha.
 
Haina haja ya kumshambulia matendo yake yatamashambulia yeye mwenyewe,atajilaani yeye mwenyewe kwa hila zake,wakati huo wewe Mungu atakuwa amekubariki na watashangaa imewezekanaje.Kisasi ni kazi ya Mungu!

Mungu amekupa mandatory ya kuitawala dunia na yaliyomo ikiwemo hao maadui
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hakuna asiye na adui. Na hakuna ambaye sio adui kwa mwingine. Yaani wewe unavyojiona hapo kuna mtu anakuona ni adui yake. Halikadhalika wapo unaowaona ni maadui.

Unaweza kuwa na maadui kwa Wema wako. Kama vile unavyoweza kuwa na maadui kwa ubaya wako. Adui ni adui bila kujali sababu za uadui. Unaweza kuwa na uadui unaosababishwa na tofauti za kifikra na kimtazamo. Pia wapo unaowaona màadui kwa sababu ya mitazamo yao dhidi yako haipatani.

Wapo maadui wanaotokana na maslahi ya kiuchumi. Yaani unapoingiliana laini ya uchumi ya mtu mwingine tayari mnakuwa màadui. Au mtu anapoingilia laini yako ya uchumi automatically mnaingia katika ligi ya uadui. Elewa, ilimradi unaishi basi uadui hauepukiki.

Sasa kuna ukweli uadui ambao mpo katika vita ya moja kwa moja. Vita ya wazi na wala sio ile vita baridi au vita ya ndani kwa ndani. Yaani mnachukiana au unamchukia fulani lakini fulani hajui kama wewe ni adui yake. Au kuna mtu anakuchukia na ni adui yako mkubwa lakini hujui kabisa.

Adui anaweza kuwa yeyote, lakini adui mbaya ni yule anayekutawala;
i) Anayekutawala kihisia, huyu anaweza kuwa mkeo, mumeo, ndugu, wazazi, Wakwe au rafiki.
Ii. Anayekutawala kiuchumi, huyu anaweza kuwa Boss au mwijiri wako.
iii) Anayekutawala kisiasa. Hapa tunazungumzia serikali. Inaweza kuwa adui yako kwa kukusababishia maisha magumu.
iv) Anayekutawala Kiroho. Hawa ni wachungaji, masheeikhe, maimamu, Askofu, waganga wa kienyeji. N.k

Mbinu za kujua adui zako

Taikon Master kama Mastermind, Multiplayer, Game changer na Mtibeli halisi ninakupa mbinu chache za kujua maadui zako ili uweze kuishi kwa Amani;

1. Yeyote anayetaka umuamini na umuone mwema.
Mtu yeyote anayelazimisha umuamini, anajifanya mwema kwako lakini kwa wengine sio mwaminifu na sio Mwema huyo ni adui yako. Adui wengi wenye akili huhakikisha anaiteka imani yako. Usimshuku. Imani ni silaha na vazi la adui kumpumbaza anayemuwinda. Uaminifu bandia ni vazi la kondoo. Mtu mwaminifu ni mwaminifu kwa watu wote na sio wewe pekeako. Ukiona mtu anasaliti wengine lakini kwako anajifanya ni mwema. Huyo ni adui yako.

2. Anapenda kukuchimba, kujua mipango na mambo yako. Adui kikawaida hutaka taarifa kutoka kwako ambazo zitamsaidia yeye kwa wakati ujao. Mtu anayekuuliza mambo yako ambayo yeye hahusiani nayo. Huyo uwe mwangalifu naye. Watu kama hawa kuna namna ya kudili nao na kuweza kuwadhibiti. Mtu anauliza mipango yako wakati hajawahi kukusaidia kwa chochote huko nyuma huyo ni adui.

3. Anapenda akifanya mazuri wewe ndio uwe shahidi. Watu wabaya hupendelea ushahidi wakifanya mazuri. Hupenda kujionyesha pale wafanyapo mazuri. Hizo ni sifa za adui. Hufanya hivi kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni kuteka na kupumbaza Watu. Na kujiwekea defence mechanism hapo baadaye.

4. Anapenda kukushauri mara kwa mara hata haujamuomba. Na mara nyingi ukifanikiwa huchomekea kuwa yeye ndiye aliyekushauri ilhali wazo hilo huenda ulikuwa nalo au ulikuwa unafanya kabla hata hajazungumzia jambo hilo kwako. Ukiona upo na mtu hasa rafiki, ndugu au jamaa ambaye anapenda kutoaga ushauri mara kwa mara yaani haiwezi kupita siku au Wiki anakushauri hiki mara kile. Hiyo kwako iwe red alert ya kuwa Mtu huyo ni mbaya. Watu wabaya waliokaribu yako ndio huwa na tabia hizo.

Kikawaida Watu wema, hutoa ushauri kwa nadra hasa pale unapohitajika. Na sio mara kwa mara.

5. Anapenda kuwasema Wengine mambo yao na hawezi kum-face mtu kumwambia Ukweli.
Huyo ni mtu mbaya. Moja ya dalili ya Watu wasaliti ni kukusema nyuma ya mgongo wako au migongo ya Watu wengine. Kikawaida Watu wabaya hawana uwezo wa kum-face mtu moja kwa moja. Ukienda mbugani au vitani sio rahisi adui kuja uso kwa uso. Lazima wajifiche kwenye vichaka wakikuvizia.

Kama anashindwa kuwaambia ukweli watu anaowasema. Hii inamaanisha hata wewe kuna mambo hawezi kukwambia anawaambia wengine. Na mengi ya mambo hayo ni mabaya tu. Watu hawa ndio wazuri wa kukusagia kunguni.

Ni muda gani wa kumshambulia adui?

Watu wengi humshambulia adui na kujikuta wakipoteza pambano au wakishindwa kunufaika na pambano.

1. Jua uwezo wako
Hakikisha unajua uwezo wako kabla ya kumshambulia adui yako. Uwezo namba moja ni uwezo wa Akili. Hakikisha unajua uwezo wako wa akili katika mapambano upo kwa kiwango kipi. Uchumi wako na connection ya walioupande wako.

2. Wajue adui zako
Kabla ya kushambulia hakikisha umewajua maadui wako halisi. Hili litawezekana baada ya kutumia akili kuliko Hisia zako. Hakikisha unajua adui anaakili na upeo kiasi gani. Uchumi wake. Connection zake (watu walioupande wake) Silaha anazozitegemea.

Ni vizuri unapopambana na adui yako ukishajua washirika wake. Ni muhimu kuanza na wale washirika ambao unawaona wananguvu na watakaokupa changamoto. Ukishawa-keep busy au kuwaangamiza washirika tegemeo wa adui yako unaweza kuratibu shambulio kwa adui yako. Hakikisha uhusika wako katika kushambulia washirika wako uwe fiche au bandia. Yaani wewe usihusishwe wala kuonekana.

Ni vizuri kushambulia yale mambo yanayompa furaha adui au mshirika wake. Mfano kile anachojivunia kama uchumi au familia yake yenye furaha na amani basi unaweza anzia hapo. Shambulio la kile anachokipenda, anachojivunia au kinachompa mtu furaha ndio shambulio bora zaidi litakalomtoa adui mchezoni na hata kuwa na nafasi nzuri ya kurejesha mapigo kwa kiwango chenye tija kwake.

3. Angalia kama unaweza Kunufaika na adui yako katika vita yenu
Sio kila adui lazima ummalize papo hapo. Vita unapoianza hakikisha umefanya hesabu ya kila hatua na mashambulio na faida na hasara zake. Mfano, adui yako umemchukulia mke wake kama sehemu ya kisasi chako. Huna sababu ya kumuangamiza wakati unaweza kutumia pesa na kumkomba bila ya yeye kujua. Kuliko umuue alafu uanze kupata shida ya kumlea huyo Mkewe na watoto wake.

Au adui yako akipiga kelele na mitafaruku yenu inasababisha unapata pesa mitandaoni kama unaakaunti YouTube au blog au Facebook au Instagram. Adui wa hivi huwezi kummaliza ilhali vita yenu inakunufaisha wewe kiuchumi.

Hata Mungu na shetani kwa wale wenye kuamini huulizaga mbona Mungu hamuui shetani. Jibu ni kuwa huwezi muua adui ambaye unanufaika kutoka kwake.

Adui huangamizwa moja kwa moja kama analeta madhara makubwa kwako na ikiwa hakipo faida yoyote.

4. Adui unaweza kumtumia kupambana na maadui wako wengine
Adui yako mdogo unaweza kumseti akajikuta katika ugomvi usiomhusu. Yaani akawa katikati yako na adui yako Mkubwa. Kwa hiyo inakuwa vita ya maadui zako. Wanapigana wewe kazi yako ni kuchochea kuni tuu. Ukiona huyu kazidiwa na inakaribia kumalizwa unambusti ili waendelee na vita huku wewe ukitumia nguvu ndogo wao wakizidi kuhenyeka.

5. "Neutralise Karma"
Shambulia ukishakuwa umeuseti wakati. Yaani wakati haupo upande wa adui. Ili kuleta ile kauli ya Dua la kuku halimpati mwewe. Yaani hapo karma isifanye Kazi. Watu wenye akili ni wale wanaojua kui - neutralise Karma. Yaana amekupiga na kukuonea lakini hatalipwa baya lolote. Ndio maana Watu wengi humlalamikia Mungu kwa nini adui zao hawapatwi na mabaya. Taikon ninakuambia kuna kitu kinaitwa "Neutralise Karma" Hii ni nadharia ambayo nimeiandikia kitabu kidogo ambacho hakizidi kurasa mia moja.
Hiki ni kitabu kwa wale walioamua kuwa Watu wabaya.

Taikon Master nimemaliza. Acha nipumzike.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
akiingia kwenye 18zako tu unatembea nae mbele bila mbambamba 🐒

R I P Laigwanan comrade ENL
 
Haina haja ya kumshambulia matendo yake yatamashambulia yeye mwenyewe,atajilaani yeye mwenyewe kwa hila zake,wakati huo wewe Mungu atakuwa amekubariki na watashangaa imewezekanaje.Kisasi ni kazi ya Mungu!
Uko sahihi lakini hi hoja hai apply kwenye ulimwengu wa mafia au ujasusi
 
Back
Top Bottom