Dodoma moja
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 307
- 177
Habari ya majukumu wakuu
Bila kuwachosha sana niende moja kwa moja kwenye mada, nilinunua kiwanja kwa ajili ya makazi pemebezoni mwa mji kipindi hicho bado palikuwa hapajachanganya sana kama sasa lakini kadri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda paliendelea kubadilika na palichanganya sana kutokana na uwepo wa tawi la chuo kimoja maarufu na kufanya watu waongezeke kwa kasi na hata bei ya nyumba za kupanga kupanda maradufu.
Kipindi nanunua palikuwa hapajapimwa lakini tulipimiwa upimaji shirikishi na Halmashauri na ilipofika mwaka 2020 nikaanza kujenga taratibu hadi mwaka huu ambapo katika plan zangu ilikuwa ifikapo mwezi Mei nihamie lakini kipindi naanza ujenzi kulikuwa na eneo kubwa kidogo pembeni yangu nikawa nasikia linauzwa lakini kwa kuwa sikuwa na uwezo wa kulinunua na pia halikuwa akilini mwangu wala sikuhangaika nalo, siku moja nikasema ngoja niende site kukagua duh cha ajabu nikakutana na jengo linanyanyuka kwa kasi kwenye hilo eneo kuuliza majirani wakaniambia eneo limeuzwa na aliyenunua anajenga gesti yenye vyumba karibu 20 nikaishiwa pozi kuwa nitaishije na gesti pembeni yangu vip kuhusu ustawi wa familia yangu?
Sasa nimepata wazo na mim nimeamua kuibadilisha nyumba yangu kuwa lodge pia na fundi ameshanichorea ramani nitapata vyumba kama vitano ambavyo nitaanza navyo
Acha niendelee kubaki kwenye upangaji potelea pote although najua ninachokifanya lodge ikianza nitatumia ninachokipata kule nalipa kodi huku najenga taratibu sehemu nyingine uzuri nimeshanunua kiwanja kingine vilikuwa vinauzwa kwenye mradi wa Halmashsuri ambako hakuna ujinga wa mtu kujenga chochote anachojisikia tu baada ya kupata funzo kwa kilichotokea nikasema kwa sasa sitanunua squtter tena bora nigharamike kwa kununua bei kubwa lakin ni kiwanja ambacho nitajenga kwa amani na kuishi kwa amani pia
Naamini hata humu JF kuna wadau watakuwa walishakutana na changamoto kama yangu