Uchumi wa Tanzania Waporomoka kutoka 6.9% hadi 4.7% kutokana na Corona

Hayo yamefichuka leo baada ya hotuba ya Mh Rais Samia Suluhu alipokuwa anawahutubia Wafanyakazi wa Tanzania kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani

Ameitaja Corona kama sababu kubwa ya kuanguka kwa uchumi wa Nchi yetu , ambapo amewaomba wafanyakazi kuvumilia hadi mwakani ili kuongezwa mshahara baada ya Uchumi wa nchi kuporomoka kutoka 6.9% hadi 4.7%

Ikumbukwe kwamba kwa miaka mingi viongozi wa Tanzania wakiwemo Rais wa zamani pamoja na Mawaziri kadhaa mmojawapo akiwa Mwigulu Nchemba hawakuamini uwepo wa corona wala athari zake .
Aisee 🤔🤔
 
Mama naye kaanza kuchapia! Uchumi unapimwa kwa GDP. Anaposema umeshuka kutoka 6.9% kwenda 4.7% ana maanisha nini hasa? Au alikusudia kasi ya "ukuaji wa uchumi" wetu imepungua? Contraction (kushuka) kwa uchumi ingalikuwa negative rate. Ama?
Na bado mtajificha humu ngoja mama atulie, awambie ukweli ,mungu wenu wa Chato alikua Hitler na stetani
 
Uchumi wa nchi umeporomoka au makadirio ya kiwango cha ukuwaji wa uchumi ndicho kimeshuka? Ni vyema ikaeleweka, kushuka kwa kasi ya ukuwaji wa uchumi hakumaanishi uchumi umeporomoka bali uchumi utakuwa ila si kwa kiwango kilichokadiriwa awali.
 
Tatizo siyo kushuka kwa uchumi, hapa tatizo ni kwanini walikuwa hawataki kukili kuwa uchumi unadorora kisa korona ?
Mbona huwa inasemwa itakuwa mlikuwa tu hamfatilii na kuchambua hotuba naona hata mleta mada ndo leo anaskia wakati hata samia alipokuwa anahutubia bunge alisema
 
Na bado mtajificha humu ngoja mama atulie, awambie ukweli ,mungu wenu wa Chato alikua Hitler na stetani
Nafikiri hujaelewa tu ninachosema. Ukisema uchumi umepungua kutoa 6.9% kwenda 4.9%, haina maana yoyote (kiuchumi). Maana nitakuuliza uchumi wa 6.9% ipoje? Uchumi unapimwa kwa GDP (say, TZS 150 trillion). Hiyo anayosema mama naamini ni "ukuaji" wa hiyo GDP ....kwa maana kwamba uchumi ulikuwa unakua kwa 6.9% lakini "kasi" hiyo sasa imepungua mpaka 4.7%. Hii maana yake ni kuwa uchumi bado unakua lakini kwa kasi ndogo kuliko mwanzo. Ukisema uchumi umepungua au kushuka ni dhana tofauti ....hapo unazungumzia contraction.....(labda useme kutoka TZS 150tr mpaka TZS 140tr).

NB: Huyo ,'mungu wa chattle' ana mitume wake waaminifu sana. Mimi sio mmoja wao!
 
Hayo yamefichuka leo baada ya hotuba ya Mh Rais Samia Suluhu alipokuwa anawahutubia Wafanyakazi wa Tanzania kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani

Ameitaja Corona kama sababu kubwa ya kuanguka kwa uchumi wa Nchi yetu , ambapo amewaomba wafanyakazi kuvumilia hadi mwakani ili kuongezwa mshahara baada ya Uchumi wa nchi kuporomoka kutoka 6.9% hadi 4.7%

Ikumbukwe kwamba kwa miaka mingi viongozi wa Tanzania wakiwemo Rais wa zamani pamoja na Mawaziri kadhaa mmojawapo akiwa Mwigulu Nchemba hawakuamini uwepo wa corona wala athari zake .
Nimerudi rafiki yangu wa kitambo kutafakari Tanzania ya kesho inaendaje
 
Mama aliita kudemka... korona kumchukua ni habari za mitandaoni.
Mungu wenu Jiwe aliwapotosha watu . Ohh uchumi wa kati, oohh sijui vita vya uchumi, oohhh Tanzania tumeishinda Corona !!! Yako wapi ?! Zaidi ya kuishia kumzoa na yeye .

Mungu ni fundi, tena fundi mkuu
 
Hayo yamefichuka leo baada ya hotuba ya Mh Rais Samia Suluhu alipokuwa anawahutubia Wafanyakazi wa Tanzania kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani

Ameitaja Corona kama sababu kubwa ya kuanguka kwa uchumi wa Nchi yetu , ambapo amewaomba wafanyakazi kuvumilia hadi mwakani ili kuongezwa mshahara baada ya Uchumi wa nchi kuporomoka kutoka 6.9% hadi 4.7%

Ikumbukwe kwamba kwa miaka mingi viongozi wa Tanzania wakiwemo Rais wa zamani pamoja na Mawaziri kadhaa mmojawapo akiwa Mwigulu Nchemba hawakuamini uwepo wa corona wala athari zake .
Hongera kamanda
 
Back
Top Bottom