Mtu wa kwanza
New Member
- Sep 14, 2018
- 3
- 0
Kibesa S/msingi wilaya ya Ubungo, jijini Dar Es Salaam, wanafunzi wa darasa la nne waamuliwa kufanya mtihani mfululizo kwa gharama ya sh. 1,000 kila mwanafunzi na kwa darasa zima lenye wanafunzi 120 linalazimika kuchanga kiasi cha sh.120,000/ ikitajwa kuwa ni posho ya Mwalimu na gharama ya kuchapisha mitihani.
Wazazi wamelalamika mbali na hizo gharama, michango mingine mingi ikiendelea hali ambayo inalazimu wazazi kushindwa kumudu gharama.
Walimu wamekuwa wakiitisha vikao kujadili na wazazi huku maoni yanayotolewa na wazazi kulalamikia gharama hizo yakipuuzwa.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Nestory Masunga, amekuwa akitoa vitisho kuwa mzazi asiyechangia, mtoto atatengwa na hatopewa mtihani na anaweza asifanye vyema mtihani wa taifa.
Wazazi wanaiomba serikali kupitia rais Samia S. Hassan kuwasaidia kwani kufanya mtihani kila siku hakutamsaidia mtoto kuelewa badala yake walimu wajikite na kutoa muda wa kutosha kuwafundisha watoto kwenye masomo ambayo hawafanyi vizuri badala ya kuwapa mitihani kila siku mfululizo.
Wanaiomba Serikali iingilie kati na ifuatilie na itoe muongozo kwani michango ni mingi na inazidi kuratibiwa katika shule hii ya Kibesa.