Waisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 40 kwa kuvujisha Mtihani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Meneja Uendeshaji Mitihani, Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Vonensia Sanga ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi Serikali ilivyopata hasara ya Sh40 bilioni baada ya kuvuja kwa mtihani wa darasa la saba wa mwaka 2022.

Pia ameeleza jinsi alivyopata taarifa ya kuvuja kwa mtihani hiyo na hasara ambayo Serikali imepata kutoka na kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao.

Vonensia ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa mashtaka katika kesi ya kuvujisha mtihani wa darasa la saba wa mwaka 2022 inayomkabili washtakiwa 12 wakiwemo walimu.

Shahidi huyo ametoa ushahidi wake leo, Novemba 16, 2023 mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Pamela Mazengo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Jahnson Ondieka(37), Patrick Chawawa, Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nyanyakila na Gladius Roman.

Wengine ni Dorcas Muro, Alcheraus Malinzi, Lloyd Mpande, Ronald Odogo, Jacob Adagi na Joel Ngome.

Washtakiwa hao wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuvujisha mitihani na kutengeneza nyaraka za uongo.

Akiongozwa na mawakili wa Serikali, Roida Mwakamele na Titus Aaron shahidi huyo alidai kuwa taarifa ya kuvuja kwa mtihani aliipata kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji mitihani Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania, Edger Kasuga.

Alidai kuwa Oktoba 13, 2022 saa tatu asubuhi aliitwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Edger Kasuga na kutaarifiwa kuwa mtihani ambao ulifanyika Oktoba 5 na 6 ulikuwa umevuja.

Shahidi huyo alidai kuwa baada ya kuelezwa hayo aliagizwa kwenda kwa Mhasibu Mkuu wa baraza hilo kwa ajili ya kupata jumla ya gharama zilizotumika katika maandalizi ya mtihani huo ili zikasaidie katika kutoa maelezo polisi.

Sanga alidai kuwa alifika kwa Mhasibu na kutajiwa gharama hizo ambazo zinajumuisha gharama za utunzi, uchapaji, ufungaji, usambazaji, usimamizi na usahishaji.

Alidai kuwa alimfikishia Mkurugenzi taatifa hiyo ya gharama na baadae alikwenda Polisi kutoa maelezo.

Alidai kuwa kitendo cha mtihani huo kuvuja Serikali imepata hasara ya Sh 40,460,623,222 pamoja na baadhi ya wazazi kupata usumbufu kwa vijana wao kurudia mtihani baada ya baraza kufuta matokeo ya vituo 24 vya mitihani.

Katika mashtaka yao, mshtakiwa Malinzi inadaiwa kati ya Oktoba 2, 2022 na Oktoba 12, 2022 sehemu isiyojulikana akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa mtihani wa somo la uraia la darasa la saba akijifanya mtihani huo ni halali na umeandaliwa na Necta.

Pia, tarehe hiyo na sehemu isiyojulikana mshtakiwa Malinzi akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa mitihani wa somo la Maarifa ya Jamii wa darasa la saba uliijifanya mwaka 2022, alionyesha kuwa mtihani huo umeandaliwa na Necta.

Katika shtaka tatu, mshtakiwa Adagi na Ngome wanakabiliwa na shtaka moja la kuvujisha mitihani ya Taifa ya darasa la saba, kinyume cha sheria.
 
Back
Top Bottom